Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
Mabinti wengi hutafakari kiu ya kidume ni nini haswa?
Wakitaka kufumbua kitendawili cha kiu bila ya majibu!
Wengi hugharimia mengi lakini majibu huwa haba….
Wengi hufikiria kiu ya kidume ni kuuchimbua utupu wao!
Kiu ya kidume kwa binti ni fumbo nami kulifumbua.
Kiu ya binti siyo kificho kwani hadharani huimwaga!
Akikutupia jicho la mahaba huhitaji kujiuliza ataka nini!
Akikuongelesha wajua sauti yake mwororo ina jambo!
Hata kama umejificha atakutoa pangoni na pendo lake!
Kiu ya kidume kwa binti ni fumbo nami kulifumbua.
Mwanumme kueleweka siyo rahisi hata chembe.
Kwani rekodi yake huwa ni kizungumkuti kabisa.
Rekodi yake humsuta kama mpita njia asiye masikani.
Mabinti kuchukua tahadhari majanga yasije kuwadhuru.
Kiu ya kidume kwa binti ni fumbo nami kulifumbua.
Kijuujuu utafikiri kiu ya kidume ni uchi!
Lakini ukizama hiyo ni dalili ya kiu yake!
Kiu ya kidume ni utii wa binti na siyo uchi!
Binti hudhani uchi ndiyo wenyewe kumbe la!
Kiu ya kidume kwa binti ni fumbo nami kulifumbua.
Kwa niaba ya wanaume, Pongezi kwa kufunguka on our behalf
Kijuujuu utafikiri kiu ya kidume ni uchi!
Lakini ukizama hiyo ni dalili ya kiu yake!
Kiu ya kidume ni utii wa binti na siyo uchi!
Binti hudhani uchi ndiyo wenyewe kumbe la!
Kiu ya kidume kwa binti ni fumbo nami kulifumbua.
Ruta kwa hili:Kiu ya kidume ni utii wa binti na siyo uchi! :whoo:
You made my day!! Nitafute Raskazoni baa nikuchomee nusu kilo ya nyama ya ng'ombe!!
PetCash.....wenzetu hudhani bakora tukiwacharaza ndiyo kiu yetu kumbe kiu yetu ni kuona wanatutii na bakora inakuwa ni kithibitisho cha dalili ya utii wao kwetu wao hawatuelewi kabisa................
Rutashubanyuma:kama kweli ni utii na wale wanaofata mabint kule corner bar hao wanafataga utii?
PetCash wanatakiwa hiyo siri waikumbatie na mizozano isiyo ya lazima itafifia................na kwisha kabisa.....Ni kweli mkuu @Rutashubanyuma, Submission of a woman is how to love a man, Ndivo tulivyoumbwa (We all need that). Na ndio maana chanzo kikubwa cha ndoa kuvunjika ni lack of that...
unakuta mdada akikupa tu anakuwa anakuganda mpaka basi sijui ndio maana ya kufikiri kiu yetu ni uchi au ili mradi usimsumbue baadae mpaka sasa sijapata jibu..
hahaha ruta umewaza nn? mm sifahamu kiu ya mwanamme kama n utii wa binti ,mbona kuna wanaume wanapelekeshwa na wanawake humu na bado wana wang'ang'ania , mm nadhani kiu yao n muonekano na mvuto wa mwanamke alivyo kama na quality gani na aki walk nae mitaan watu watamsifia una chombo ,na ilo la uchi sijui