Kitwanga aikosoa Serikali ujenzi wa Reli

Mimi naona bado anapiga pori. sijaona pointi yake hapo. Pia tatizo Watanzania tunapenda sana ushabiki hata kama mtu kasema pumba tupu. Standard Gauge Railway imepangwa kujengwa kwa awamu, awamu ya kwanza ndo hiyo ya Dar-Moro na kazi ilishaanza. Awamu ya pili ni Moro-Makutopora (Dodoma) na Mkataba unasainiwa Februari hii. wakati kazi ya hizi zinaendelea tunajipanga na Dodoma-Tabora-Kigoma, Tabora-Mpanda, Tabora-Mwanza na Tabora Isaka. Hapo tatizo lipo wapi? Na taarifa imeshatolewa kuwa ujenzi wa toka Isaka-Kigali kwa ubia kati ya TZ na Rwanda unaanza Mwakani.

Hivi mnaokosoa sana humu mnalipa kodi kweli? au mnashabikia tu wakati hata kodo stahiki hamlipi.
 
Tena hazifanani, kama alivyosema, ndiyo!!! utapata reli ya SG kutoka Dar hadi Moro. Upakie mizigo yako kwenye behewa ukifika Moro ni mwisho wa safari, mzigo wa Mwanza uupakue uuweke kwenye locomotive; bichwa lake huchukua siku 6 kufika Tabora. Hayo maembe si yeshaota?? Tutulie tujipange. Maendeleo hayaji kwa kelele kwani weshasema kuwa; Maneno hayauvunji mfupa.

Hapo tatizo lipo wapi? Kwa sasa hivi tunasafirishaje? tutakuwa tunatumia njia tunayotumia kwa sasa wakati tukiendelea na vipande vilivyobaki.
 
Kwa maneno mengine tusitegemee kuifaidi hiyo SG hadi ifika Isaka??
 
Kila kipande kinachokamilika tunaendelea kukifaidi. Hapotatizo lipo wapi? hata barabara ya kati ya Dar-Dodoma-Singida-Mwanza haijajengwa ndani ya siki moja. Dar-Moro ilijengwa miaka ya mwazo kabisa ya Uhuru. Moro-Dodoma tukajenda 1986. awamu ya Mkapa tukaanza kipande cha Dodoma-Singida-Mwanza. hadi Mkapa anaondoka tulikuwa na kipande hakijakamilika pale kati ya Manyoni na Dodoma, hatimaye tukakamilisha. sijaona tatizo. tatizo Watanzania washabiki sana. Hata Mjerumani hii reli iliyopo hakukamilisha ndani ya mwaka moja na kwa kila kipande kilichokamilika kilianza kutumika. ndo maana kuna stesheni za katikati.
 
Tatizo lenu kurukia treni bila kujua iendako. Unawezaje kufananisha barabara na reli?? Reli ya SG sio sawa na hii iliyopo. Hata behewa lake sio ka hili lililopo. Ukiupakia mzigo lazima uushushe Moro ndio uupakue na kuupakia tena kwenye hizi zilizopo.
 
Ki
20352458-hands-are-pounding-spices-in-a-mortar-stone.jpg
 
Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga ameikosoa Serikali ya awamu ya tano na kuitaka iwe na mipango inayoeleweka na si kufanya maamuzi au mipango ya zimamoto.

Kitwanga.jpg

Kitwanga amesema hayo bungeni na kudai kuwa Serikali haina haja ya kujenga reli nusu nusu ikiwa inaona haina mpango endelevu wenye tija na kuleta matumaini kwa wafanyabiashara na watu wa viwanda.

"Tunahangaika kutengeneza reli na reli inajengwa kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro inawekwa reli ya umeme ila ukishafika Morogoro kuja Dodoma utofauti wa reli kati ya hiyo standard gauge na ya kawaida unatofautiana, sijui sasa unaanza kupakua hiyo mizigo uanze kupakua kwenye ile reli nyingine ya zamani? Mimi nadhani kuwe na mipango ambao unakuwa ni wa jumla utachukua muda lakini unajua tunajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma au Dar es Salaam mpaka Mwanza" alisema Kitwanga

Kitwanga aliendelea kusema kuwa

"Lazima kuwa na mipango thabiti tunasema kwamba hicho ni kipindi cha mpito ambacho kitakuwa kinaeleweka kwa wafanyabiashara na watu wenye viwanda nchini ambapo watakuwa na matarajio yanaoeleweka na mipango hii ifuatwe hakuna sababu ya kuanza kujenga nusu nusu wakati hujui kinachofuatia na huna mpango wa kupata hela, ni vyema ukawa umejipanga kwamba nikitoka Dar es Salaam kufika Morogoro nitakuwa nimepata fedha kutoka Morogoro kwenda Dodoma, Tabora tusiwe na mipango ya zima moto" alisisitiza Kitwanga

Chanzo: Eatv.
 
Kudaadek kumbe hawanaga mipango wanakurupukaga haya bombaider lkn lisu nilimsikiaga akiwapondaga na bombaidaga yao sasa mtabir yupo ubelgij utabir umetimia lait angekuwpo da tungekuwa tushapewa milion50 kila kjj
 
Tatizo lenu kurukia treni bila kujua iendako. Unawezaje kufananisha barabara na reli?? Reli ya SG sio sawa na hii iliyopo. Hata behewa lake sio ka hili lililopo. Ukiupakia mzigo lazima uushushe Moro ndio uupakue na kuupakia tena kwenye hizi zilizopo.

hapo tatizo lipo wapi? Morogoro kuna stesheni ya reli, tena kubwa hadi gereji ya reli ipo pale. Tutashusha mizigo Morogoro, then za kwenda kanda ya ziwa zitapakiwa katika treni ya zamani, za kwenda mikoa ya kusini itachukuliwa kwa malori. Tutakuwa tumenusuru uharibifu wa barabara kwa kipnade cha Dar-Chalinze-Moro wakati tukiendelea na ujenzi wa vipande vingine. watanzania kwa kushabikia hamjambo. Kwa hiyo mnataka tusitumie kipande cha Dar-Moro hadi tukamilishe hadi Kigoma na hadi Mwanza. Kumbekeni SGR siyo kwa ajili ya mizigo tu, itasafirisha na abiria. Kwa mantiki hiyo Watu wanaweza kuishi Moro, wakafanya bishara Dar maana itakuwamwendo wa chini ya masaa mawili.
 
Tena hazifanani, kama alivyosema, ndiyo!!! utapata reli ya SG kutoka Dar hadi Moro. Upakie mizigo yako kwenye behewa ukifika Moro ni mwisho wa safari, mzigo wa Mwanza uupakue uuweke kwenye locomotive; bichwa lake huchukua siku 6 kufika Tabora. Hayo maembe si yeshaota?? Tutulie tujipange. Maendeleo hayaji kwa kelele kwani weshasema kuwa; Maneno hayauvunji mfupa.
Basi tuna hasara sana!!
 
Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga ameikosoa Serikali ya awamu ya tano na kuitaka iwe na mipango inayoeleweka na si kufanya maamuzi au mipango ya zimamoto.

Kitwanga.jpg

Kitwanga amesema hayo bungeni na kudai kuwa Serikali haina haja ya kujenga reli nusu nusu ikiwa inaona haina mpango endelevu wenye tija na kuleta matumaini kwa wafanyabiashara na watu wa viwanda.

"Tunahangaika kutengeneza reli na reli inajengwa kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro inawekwa reli ya umeme ila ukishafika Morogoro kuja Dodoma utofauti wa reli kati ya hiyo standard gauge na ya kawaida unatofautiana, sijui sasa unaanza kupakua hiyo mizigo uanze kupakua kwenye ile reli nyingine ya zamani? Mimi nadhani kuwe na mipango ambao unakuwa ni wa jumla utachukua muda lakini unajua tunajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma au Dar es Salaam mpaka Mwanza" alisema Kitwanga

Kitwanga aliendelea kusema kuwa

"Lazima kuwa na mipango thabiti tunasema kwamba hicho ni kipindi cha mpito ambacho kitakuwa kinaeleweka kwa wafanyabiashara na watu wenye viwanda nchini ambapo watakuwa na matarajio yanaoeleweka na mipango hii ifuatwe hakuna sababu ya kuanza kujenga nusu nusu wakati hujui kinachofuatia na huna mpango wa kupata hela, ni vyema ukawa umejipanga kwamba nikitoka Dar es Salaam kufika Morogoro nitakuwa nimepata fedha kutoka Morogoro kwenda Dodoma, Tabora tusiwe na mipango ya zima moto" alisisitiza Kitwanga

Chanzo: Eatv.
Siijui taaluma ya Mh. Kitwanga lakini nadhani ana mawasiliano na wahandisi.

Behewa la treni linaweza kuwekewa DUAL AXLE inayoweza kutembea kwenye reli ya Standard Gauge na Narrow Gauge kwa wakati mmoja.

Kwa hiyo mabehewa ya abiria na mizigo hayahitaji kubadilishwa yakifika Morogoro. Yataendelea na safari kutoka SG ya DSM-MORO na kuingia Narrow Gauge ya MORO-DDM-TBR-MWANZA bila ya kubadilisha chochote kile.

Hizi hoja nyingine hawa waheshimiwa wangekuwa wanazifanyia utafiti kabla ya kuzileta Bungeni. Inatia aibu.
 
Atakuwa alikuwa tungi, kumjibu mlevi ni kupoteza muda, ila nani kamwambia ni ya kuungaunga? Kwahiyo alifikiri ni koti kuwa lazima uvae na suruali yake?
 
Tumeingia chaka awamu hii!!

Hivi ni nani mshauri wa haya mambo au ni maamuzi ya mtu mmoja tu?

Treni ya kuungaunga!!
Mimi ni mchumi na nimekuwa nikifuatilia mambo ya nchi hii. Nimekutana na wasomi na waelewa wa mambo ya uchumi kwa kweli lipo jambo linaumiza sana. Wanasema kwa nn Tz tumeamua kujenga reli hadi Rwanda na sio Kigoma kwanza. Nikawaambia hata mimi sijui kwa nn. Wakasema wanashindwa hata kutoa maoni binafsi kwa sababu hawajui kama wasipoeleweka basi watatishwa. Ukweli walinieleza faida mara mia ambazo Tz tungepata kiuchumi,, kidiplomasia, kiushawishi na hata kiusalama kwa kujenga reli ya kisasa hadi Kigoma kwanza na sio Mwanza-Rwanda kama bwana mkubwa anavyowaza.

Hivi unajua Rwanda kwa nn anakomalia reli hiyo.. Nguvu ya Rwanda itaongezeka mara milioni mia juu ya Tz ikiwa atakamilisha reli hiyo..

Halafu naona hali ikibadilika kabisa. Mengine siwezi kusema hapa
 
Huyu lazima atakuwa ameyatwanga!
Mtoto wa jongoo alimuuliza mama yake, "Mama mbona nina miguu mingi sana, nianze na mguu gani kutembea?". Mama jongoo alimujibu mtoto wake, "Anza na wo wote tu utafanikiwa kutembea". Na sisi ni hivyo hivyo. Tumeanza na mguu wo wote na hatimaye tutatembea tu. Kitwanga asiwe na wasi wasi, tumeshaanza. Naye apunguze tu kuyatwanga, anaweza kuanza na kinywaji cho chote kile hatimaye atafanikiwa kuacha vinywaji vyote!
 
Back
Top Bottom