Kitwanga aikosoa Serikali ujenzi wa Reli

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,291
Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga ameikosoa Serikali ya awamu ya tano na kuitaka iwe na mipango inayoeleweka na si kufanya maamuzi au mipango ya zimamoto.

Kitwanga.jpg

Kitwanga amesema hayo bungeni na kudai kuwa Serikali haina haja ya kujenga reli nusu nusu ikiwa inaona haina mpango endelevu wenye tija na kuleta matumaini kwa wafanyabiashara na watu wa viwanda.

"Tunahangaika kutengeneza reli na reli inajengwa kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro inawekwa reli ya umeme ila ukishafika Morogoro kuja Dodoma utofauti wa reli kati ya hiyo standard gauge na ya kawaida unatofautiana, sijui sasa unaanza kupakua hiyo mizigo uanze kupakua kwenye ile reli nyingine ya zamani? Mimi nadhani kuwe na mipango ambao unakuwa ni wa jumla utachukua muda lakini unajua tunajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma au Dar es Salaam mpaka Mwanza" alisema Kitwanga

Kitwanga aliendelea kusema kuwa

"Lazima kuwa na mipango thabiti tunasema kwamba hicho ni kipindi cha mpito ambacho kitakuwa kinaeleweka kwa wafanyabiashara na watu wenye viwanda nchini ambapo watakuwa na matarajio yanaoeleweka na mipango hii ifuatwe hakuna sababu ya kuanza kujenga nusu nusu wakati hujui kinachofuatia na huna mpango wa kupata hela, ni vyema ukawa umejipanga kwamba nikitoka Dar es Salaam kufika Morogoro nitakuwa nimepata fedha kutoka Morogoro kwenda Dodoma, Tabora tusiwe na mipango ya zima moto" alisisitiza Kitwanga

Chanzo: Eatv.
 
Kuna uwezekano mkubwa hii miradi mikubwa mikubwa tunayoisikia kugeuka kuwa white elephant projects ambazo mafisadi watapiga hela kimya kimya.

Natamani sana serikali ifanikiwe ili na sisi tuonyeshe misuli yetu ya kiuchumi hasa kwenye jumiya ya Afrika Mashariki. Muda utatoa majibu ya kweli na sahihi.
 
Magufuli zee la kukurupuka na mradi utamshinda tu kama ilivyomshinda elimu Bure[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Ametoa ahadi nyingi ambazo kwa uwezo nchi yetu ni ngumu kutekelezeka. Sasa anakazana kwa gharama yeyote kuhakikisha anatekeleza bila kujali Athari za kiuchumi katika muda wa kati na muda mrefu. Anajaribu kushindana na 'ego' yake mwenyewe bila kujali maumivu ya walio wengi!
 
Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga ameikosoa Serikali ya awamu ya tano na kuitaka iwe na mipango inayoeleweka na si kufanya maamuzi au mipango ya zimamoto.

Kitwanga.jpg

Kitwanga amesema hayo bungeni na kudai kuwa Serikali haina haja ya kujenga reli nusu nusu ikiwa inaona haina mpango endelevu wenye tija na kuleta matumaini kwa wafanyabiashara na watu wa viwanda.

"Tunahangaika kutengeneza reli na reli inajengwa kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro inawekwa reli ya umeme ila ukishafika Morogoro kuja Dodoma utofauti wa reli kati ya hiyo standard gauge na ya kawaida unatofautiana, sijui sasa unaanza kupakua hiyo mizigo uanze kupakua kwenye ile reli nyingine ya zamani? Mimi nadhani kuwe na mipango ambao unakuwa ni wa jumla utachukua muda lakini unajua tunajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma au Dar es Salaam mpaka Mwanza" alisema Kitwanga

Kitwanga aliendelea kusema kuwa

"Lazima kuwa na mipango thabiti tunasema kwamba hicho ni kipindi cha mpito ambacho kitakuwa kinaeleweka kwa wafanyabiashara na watu wenye viwanda nchini ambapo watakuwa na matarajio yanaoeleweka na mipango hii ifuatwe hakuna sababu ya kuanza kujenga nusu nusu wakati hujui kinachofuatia na huna mpango wa kupata hela, ni vyema ukawa umejipanga kwamba nikitoka Dar es Salaam kufika Morogoro nitakuwa nimepata fedha kutoka Morogoro kwenda Dodoma, Tabora tusiwe na mipango ya zima moto" alisisitiza Kitwanga

Chanzo: Eatv.
Alikuwa yuko sober wakati anasema hayo??
 
tatizo watu wenyewe ni waongo wa kutupwa
mwanzo walituaminisha reli inajengwa kwa hela zetu
ghafla wamebadilika wanaenda kukopa za watu
prezidaa kamba sana huyu
Na zile za kwetu wanazipeleka wa pi hawa watesi?
 
Tumeingia chaka awamu hii!!

Hivi ni nani mshauri wa haya mambo au ni maamuzi ya mtu mmoja tu?

Treni ya kuungaunga!!

Tena hazifanani, kama alivyosema, ndiyo!!! utapata reli ya SG kutoka Dar hadi Moro. Upakie mizigo yako kwenye behewa ukifika Moro ni mwisho wa safari, mzigo wa Mwanza uupakue uuweke kwenye locomotive; bichwa lake huchukua siku 6 kufika Tabora. Hayo maembe si yeshaota?? Tutulie tujipange. Maendeleo hayaji kwa kelele kwani weshasema kuwa; Maneno hayauvunji mfupa.
 
Back
Top Bottom