Kitwanga aikosoa Serikali ujenzi wa Reli

Kitwanga aikosoa Serikali ujenzi wa Reli

Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga ameikosoa Serikali ya awamu ya tano na kuitaka iwe na mipango inayoeleweka na si kufanya maamuzi au mipango ya zimamoto.

Kitwanga.jpg

Kitwanga amesema hayo bungeni na kudai kuwa Serikali haina haja ya kujenga reli nusu nusu ikiwa inaona haina mpango endelevu wenye tija na kuleta matumaini kwa wafanyabiashara na watu wa viwanda.

"Tunahangaika kutengeneza reli na reli inajengwa kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro inawekwa reli ya umeme ila ukishafika Morogoro kuja Dodoma utofauti wa reli kati ya hiyo standard gauge na ya kawaida unatofautiana, sijui sasa unaanza kupakua hiyo mizigo uanze kupakua kwenye ile reli nyingine ya zamani? Mimi nadhani kuwe na mipango ambao unakuwa ni wa jumla utachukua muda lakini unajua tunajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma au Dar es Salaam mpaka Mwanza" alisema Kitwanga

Kitwanga aliendelea kusema kuwa

"Lazima kuwa na mipango thabiti tunasema kwamba hicho ni kipindi cha mpito ambacho kitakuwa kinaeleweka kwa wafanyabiashara na watu wenye viwanda nchini ambapo watakuwa na matarajio yanaoeleweka na mipango hii ifuatwe hakuna sababu ya kuanza kujenga nusu nusu wakati hujui kinachofuatia na huna mpango wa kupata hela, ni vyema ukawa umejipanga kwamba nikitoka Dar es Salaam kufika Morogoro nitakuwa nimepata fedha kutoka Morogoro kwenda Dodoma, Tabora tusiwe na mipango ya zima moto" alisisitiza Kitwanga

Chanzo: Eatv.

Kaishauri Serekali acha Upimbi wewe Ngomb
 
Tumeingia chaka awamu hii!!

Hivi ni nani mshauri wa haya mambo au ni maamuzi ya mtu mmoja tu?

Treni ya kuungaunga!!
Kwa hakika mi sijui hawa watu walitumia ubongo au uji kufikiri,bilions zinatumika kujenga reli km200 !!!!?????? Kuna mizigo gani inapelekwa morogoro,na anafikirije akiondoka ajae ata prioritize kuendelea na ujenzi!!?si ndo itakuwa mwisho morigoro na saaana dodoma?sithole bana.mnashindwa kuwa na plan.unasema unajenga SGR kwa hela za ndani sasa umeenda kukopa ili watanzania wajao waendelee kunyonywa kulipa kisa mkurupuko,hiyo SGR itakuwa MV DSM nyingine
 
Hahaha jpm we twente tuuu. Kanyaga twente.
Kesho wape mipango ile ya reli toka Dar to Zanzibar, who cares!
 
Mimi ni mchumi na nimekuwa nikifuatilia mambo ya nchi hii. Nimekutana na wasomi na waelewa wa mambo ya uchumi kwa kweli lipo jambo linaumiza sana. Wanasema kwa nn Tz tumeamua kujenga reli hadi Rwanda na sio Kigoma kwanza. Nikawaambia hata mimi sijui kwa nn. Wakasema wanashindwa hata kutoa maoni binafsi kwa sababu hawajui kama wasipoeleweka basi watatishwa. Ukweli walinieleza faida mara mia ambazo Tz tungepata kiuchumi,, kidiplomasia, kiushawishi na hata kiusalama kwa kujenga reli ya kisasa hadi Kigoma kwanza na sio Mwanza-Rwanda kama bwana mkubwa anavyowaza.

Hivi unajua Rwanda kwa nn anakomalia reli hiyo.. Nguvu ya Rwanda itaongezeka mara milioni mia juu ya Tz ikiwa atakamilisha reli hiyo..

Halafu naona hali ikibadilika kabisa. Mengine siwezi kusema hapa

Sijaona tatizo hapo. kote tutajenda, siyo kufika Kigoma tu, tutafikisha na Mpanda. Pia tuko mbioni kuanza ujenzi wa SGR ya Tanga-Arusha-Musoma.
Tatizo Watanzania siku hizi hatujiamini completely. Tumejaa infirity complex. Tunaiogopa hadi ka nchi ka Rwanda.
 
Alkuwa kalewa

Hata kama alikuwa kalewa hoja yake ni ya msingi sana.

Hiyo SGR kama itaishia Morogoro au Dodoma haitakuwa na manufaa yo yote kiuchumi kwa hii nchi.

Ni muhimu sana ikamilike hadi Mwanza, pamoja na kuwa Reli ya kati inapaswa kuishia Kigoma. Tabora - Mwanza ni branch line.
 
huwa najiuliza hawa jamaa wakiwa ndani kama huwa zinakauka zote ila akitoka zinavia akili na wale walio inje akiingia ndani zinakauka kaukau kama dk kisamvu leo
 
Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga ameikosoa Serikali ya awamu ya tano na kuitaka iwe na mipango inayoeleweka na si kufanya maamuzi au mipango ya zimamoto.

Kitwanga.jpg

Kitwanga amesema hayo bungeni na kudai kuwa Serikali haina haja ya kujenga reli nusu nusu ikiwa inaona haina mpango endelevu wenye tija na kuleta matumaini kwa wafanyabiashara na watu wa viwanda.

"Tunahangaika kutengeneza reli na reli inajengwa kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro inawekwa reli ya umeme ila ukishafika Morogoro kuja Dodoma utofauti wa reli kati ya hiyo standard gauge na ya kawaida unatofautiana, sijui sasa unaanza kupakua hiyo mizigo uanze kupakua kwenye ile reli nyingine ya zamani? Mimi nadhani kuwe na mipango ambao unakuwa ni wa jumla utachukua muda lakini unajua tunajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma au Dar es Salaam mpaka Mwanza" alisema Kitwanga

Kitwanga aliendelea kusema kuwa

"Lazima kuwa na mipango thabiti tunasema kwamba hicho ni kipindi cha mpito ambacho kitakuwa kinaeleweka kwa wafanyabiashara na watu wenye viwanda nchini ambapo watakuwa na matarajio yanaoeleweka na mipango hii ifuatwe hakuna sababu ya kuanza kujenga nusu nusu wakati hujui kinachofuatia na huna mpango wa kupata hela, ni vyema ukawa umejipanga kwamba nikitoka Dar es Salaam kufika Morogoro nitakuwa nimepata fedha kutoka Morogoro kwenda Dodoma, Tabora tusiwe na mipango ya zima moto" alisisitiza Kitwanga

Chanzo: Eatv.
I love this! Mh Kitwanga, haya si yalianza bado wewe ukiwa ndani ya Serikali, ina maana mpango huu haukujafiliwa na kupitishwa ndani ya Baraza? Tatizo ninaloliona mimi kwa approach hii tutaishia kutumia fedha nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa ya kujenga yote moja kwa moja.
 
Kukosoa mipango na maamuzi ya mtukufu raisi ni uhaini, nashauri Kitwanga afukuzwe bungeni ili ashughulikiwe uku uraiani
 
Kuna ukweli hapa!!! Wanaosifia sifia haya madudu nao mazwazwa
 
Haya ndio mambo tunataka, sio kisa uko ccm ndio kila kitu kiwe hewala, Kitwanga ajibiwe kwa hoja.
 
Kabla ya kuingia ndani sana kwenye huu uzi tujihakikishe kwanza kama alikuwa hajatumia TBL,bungeni wameshaleta vile vibrethiraiza?
...Kwa nini msijadili kwanza hoja yake?
 
Back
Top Bottom