Kituo cha Mabasi Ubungo kutokuhamishwa

Kituo cha Mabasi Ubungo kutokuhamishwa

ELX

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
328
Reaction score
379
Ni katika taarifa ya habari ya saa 2 usiku, Meya wa jiji la Dar katoa tamko kuwa kituo cha Mabasi Mikoani na nchi jirani cha Ubungo hakitahama.

Sababu kuu ni ukosefu wa hela. Hela waliyotarajia kuendeleza kituo kipya cha Mbezi zilipelekwa kwenye mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART).

Chanzo: ITV

SWALI: Je, jiji kuvunja vibanda na miundo mbinu ya Ubungo huku wakijua hawana fedha za kukihamisha si dhuluma, au ni ulimbukeni na kukurupuka?
 
Meya wa Jiji la Dar-es-salaam,bwana Didas Masaburi ametangaza kufutwa kwa mpango wa kuhamisha kituo cha Mabasi Ubongo na kukipeleka Mbezi jijini Dar-es-salaam baada ya Jiji kushindwa kukihamisha kituo hicho licha ya kukibomoa.

Meya huyo pia ameomba radhi kufuatia uamuzi huo alioutangaza leo hii.

CHANZO:ITV
 
Mawazo yangu tu....kituo kibinafsishwe kwa mwekezaji wa ki Tanzania mwenye taaluma ya usafirishaji.Awe na uwezo wa kukijenga na kukiendesha..Taboa kama wamejipanga wanastahili kupewa nafasi ya kwanza,Scandanavia express,kilimanjaro bus,azam hao wafikiriwe kama Taboa hawatakuwa tayari.
 
Hizo hasara nani atalipa? Maccm haiki hakuna yamekaa kimasaburi saburi tu
 
Wajinga kweli kwa nini sasa walibomoa kabla hicho kingine hakijajengwa,ndo zao hawa tumewachoka,waliuza nyumba za serikali,leo watumishi wa umma wanaishi guest houses.
 
Wanataka kura tu,ngoja uchaguzi umalizike utawaona,hawana tofauti na CDA dodoma,
 
Wajinga kweli kwa nini sasa walibomoa kabla hicho kingine hakijajengwa,ndo zao hawa tumewachoka,waliuza nyumba za serikali,leo watumishi wa umma wanaishi guest houses.

Walibomoa kuwazuga Watz alafu pesa ya mpango inaingia matumboni mwao
 
Hii nchi huwa haina mipango kabisa...nimesikia eti ela zilizotakiwa kutumika huko eti zimeongezewa katika mradi wa magari ya mwendo kasi...huwa hatuna mpango hata wa miaka mitatu mbele...kweli hili lichama watendaji wake wengi wameishiwa mipango wakilala na kuamka wanafikiria wapi watapiga ela
 
Mawazo yangu tu....kituo kibinafsishwe kwa mwekezaji wa ki Tanzania mwenye taaluma ya usafirishaji.Awe na uwezo wa kukijenga na kukiendesha..Taboa kama wamejipanga wanastahili kupewa nafasi ya kwanza,Scandanavia express,kilimanjaro bus,azam hao wafikiriwe kama Taboa hawatakuwa tayari.

Wazo nzuri naliunga mkono wapewa wawekezaji wakiboreshe kisha wachukue kodi na serikali apate sehemu ya kodi yake
 
Serikali ya kukurupuka haya ndiyo matokeo yake. For a responsible government nadhani wahusika wangewajibishwa kwa kulitia Taifa hasara. Haiingii akilini unavunja nyumba yako huku ukijua huna uhakika wa kujenga mpya. Ni upuuzi usiopaswa kuvumiliwa hata kidogo.

Nimekuwa nikiingia Ubungo kupokea na kusafirisha ndugu zangu lakini hali ni mbaya sana. Hakuna pahala salama pa mapumziko, hakuna mpangilio wowote na baadhi ya huduma za kijamaii kama dispensary hakuna. Au wasafiri hawana haki ya afya wawapo stand? Vyooni ni aibu tupu lakini charges/ushuru wanachukua.

Kuwa mwanachama wa mshabiki wa ccm ni sawa na mtu aliyetupiwa jini na mtupaji kafa!
 
Tatizo ni siasa kuingilia taaluma za watu, mambo yanakwenda kulingana na Matakwa (o) ya wanasiasa.Kwani hawakufanya tahmini kabla ya kuanza mipango ya kukihamisha?? Poor tz
 
Back
Top Bottom