Kituo cha kati cha polisi

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,241
251
NAPENDA KUWASAHIHISHA WOTE WALE WAOPENDA KUSEMA 'KITUO CHA KATI CHA POLISI' KUWA SI SAHIHI, INATAKIWA KUSEMA 'KITUO KIKUU CHA POLISI'. WASIBABAIKE NA KUTOHOA NENO 'CENTRAL' KWA MAANA YA KATI. MAANA ILIYOKUSUDIWA KUTOHOLEWA NI:-
1. having control over parts: controlling the activities of connected, subordinate, or subsidiary parts. eg. a central authority.
2.
dominant: with a major or the principal role.
 
NAPENDA KUWASAHIHISHA WOTE WALE WAOPENDA KUSEMA 'KITUO CHA KATI CHA POLISI' KUWA SI SAHIHI, INATAKIWA KUSEMA 'KITUO KIKUU CHA POLISI'. WASIBABAIKE NA KUTOHOA NENO 'CENTRE' KWA MAANA YA KATI. MAANA ILIYOKUSUDIWA KUTOHOLEWA NI:-
1. having control over parts: controlling the activities of connected, subordinate, or subsidiary parts. eg. a central authority.
2.
dominant: with a major or the principal role.
Kituo cha kati cha polisi = Central Police Station na sio Centre Police Station
 
central committee utaitafsiri ni kamati ya kati?
Na central government utaitafsiri kama serikali ya kati?
Mdau yuko sahihi. Central police station ni kituo kikuu cha poilisi. Lazima usome muktadha wa matumizi ya neno. Ni sawa na wale wanaotafsiri "at the end of the day" kuwa eti "mwisho wa siku"! jamani! Hii inatakiwa iwe "mwishowe". nk
 
Mimi nafikiri wanamaanisha kwamba hicho ni kituo kikuu cha polisi au "central Police station" kwa Dar-es-Salaam chenye kujumuisha idara mbalimbali za polisi kama vile upelelezi, usalama wa barabarani na kuhodhi mahojiano muhimu na watuhumiwa wenye kesi maalum ambao watashikiliwa hapo.

Pia hapo pana osifi za makamanda wote wanaohusika na eneo hilo na ni wakubwa kivyeo. Sijui kwa sasa kwani Dar imegawanywa.

Serikali kuu au "central government" ni pale ambapo maamuzi yenye kuathiri serikali zote ndogondogo zikiwemo za mitaa kwenye maeneo kama vile ruzuku na kodi kubwa yanatoka hapo na maamuzi mengine yanatoka kwenye baraza la mawaziri na sio katibu kata.

Nafikiri nimejitahidi kutoa ufafanuzi.
 
Na central government utaitafsiri kama serikali ya kati?
Mdau yuko sahihi. Central police station ni kituo kikuu cha poilisi. Lazima usome muktadha wa matumizi ya neno. Ni sawa na wale wanaotafsiri "at the end of the day" kuwa eti "mwisho wa siku"! jamani! Hii inatakiwa iwe "mwishowe". nk

Uko sahihi kabisa mzee, unaweza kutumia pia "hatimaye"
 
Back
Top Bottom