Kituo cha ITV, kwa hili nimewashusha

Nimeshindwa kabisa kuangalia vipindi katika hz local channels yani siwezi aiseee serious !!!!!! Zaidi ya BBC Swahili siwezi kabisa kungalia local channels
 
Walikata matangazo kwasababu mitambo ilizingua
🏃🏃🏃🏃🏃
 
Sasa mkuu suluhisho la tatizo hili ni lipi. 😏😏
 
Ngosha anatisha
 
Nimeshindwa kabisa kuangalia vipindi katika hz local channels yani siwezi aiseee serious !!!!!! Zaidi ya BBC Swahili siwezi kabisa kungalia local channels
Hiyo BBC nayo inaonyeshwa local channel
 
Mzee mi mwenyewe nilikuwa naangalia, Ila nikasema labda ni coincidence tu, Ila ilipofika Al Jazeera wanarudia habari kwa kifupi, walipofikia ya Tanzania walikatisha tena
Ok nimekupata
nadhan tusiwatupie lawama zote ITV tuangalie na upande wa pili nini kinapelekea haya yote. Hata kama habari hiyo hawajaiandaa wao nao wanaangalia mstakabali wao.

Na hili naamini limewafikia kunamadhara huenda yakatokea ktk tasnia hii kwa wanaojiunga na media za nje, najua wawakilishi hata wa hizo media hapa nchini wameliona so kama kunamikataba ya kimaslahi ni tatizo baina yao.

Na hizi ishu za sikunyingi hizi, Nakumbuka katibu wa kipindi flani alivyo mlalamikiaga Tido enzi akiwa idhaa mmoja huko nnje
 
Kwa experience yangu ndogo ya miaka 8 kwenye vyombo vya habari (Including IPP ) mkiwalaumu ITV mnawaonea tu! Kuna mengi sana nyuma ya pazia, unalijua rungu la kamati ya maudhui ya TCRA? Wanaweza wakatwangwa fine kwa kusababisha 'Taharuki' mtaani pagumu jamani...tunapiga marktime na ajira hakuna! Muacheni kabisa mama wa watu, anapitia mengi ambayo mm na ww hatuyajui..including zile simu za maagizo 'Toka Juu' ! Muacheni kabisa asee! Mungu amtunze!
 


ITV ilishakufa hata kabla ya Mengi kufa kilichobaki ni kushusha kaburini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…