Kituo cha Afya Fore Plan Clinic chafungwa

ni kweli, sio msabato ni mwislam anaitwa Juma (J). yeye nilimsikia kwenye tv anasema amesoma degree ya kwanza hapa nchini na ya pili alisoma ya mambo ya kienyeji india. nilimsikia kwa masikio yangu kwenye tv anasema hivyo. alisema amesomea udaktari wa kawaida, akamaliza akaenda kusomea huu wa mimea, hivyo anajua vitu vyote na ni dr halisi. ninyi mnaposema alikuwa anauza mitumba, siamini kwasababu anapoelezea utakuta ni mtu ambaye at least amefika form four au form six and above. pamoja na kwamba, anapoelezea mambo mengine utakuta ni ya layman, si ya daktari bingwa.

all in all, amekusanya hela nyingi sana, ni bilionea, hata wakifunga wanajisumbua kwasababu ameshapata hela nyingi, ataweza kuwekeza kwingine. kama kuchuma ameshachuma za kutosha. jamaa ndi mganga wa tiba asili aliyejimarisha kuliko wote na aliyepata hela nyingi kuliko wote. pale appointments unaenda siku mbili kabla, siku nyingine zote hizi watu wameshabook, na dawa zake ni garmaa sana. malaki. miaka yote hii kila siku amekuwa akikusanya mamiilioni. zaidi ya yote, hawa tfda wanaompinga, huyo jamaa ana hela, atawapa hela kesho tu hapa kituo kitafunguliwa na ataendelea kutoa dawa.

rai yangu ni kwamba, kama kweli hawa watu wawe ni wasababu au waislam, kama wanatoa dawa wakati hawajasomea udaktari, wakamatwe wafungwe kabisa. mke wangu alishawahi kupata tatizo fulani, kaenda sana kwa hao wasababu, kuna msabato mmoja alikuwa kule tabata alikufa tayari, wife alienda sana na kwa hao wote wanaolisha watu malimao na machungwa mia, matokeo yake nilitoa sana hela hakuna kupona, waifu alikuja kuponea kwenye maombi ya kanisani hadi leo mzima. hao majamaa ni waongo ajabu, na wanatisha watu kwa maelezo ya magonjwa wanawapa matumaini ya uongo na kuwapiga hela na kwasababu watu wako kwenye shida mfano ya kupata watoto etc, anaweza kutoa hela yeyote na kwasababu wao wanajua kupata watoto na matatizo ya wanawake ndio mtu anaweza kutoa chochote, basi wanashikilia hapohapo na kuchuma hela za watu.
 
Kimefungiwa kituo? Au zimefungiwa dawa? Ama kafungiwa dr kwa ujuzi wake haba? Hizi ni hoja tatu tofauti. Kama ni kituo labda mazingira yake hayakukidhi vigezo huenda kiusafi ama vifaa. Vitumikavyo..kituo kwa maana ya center. Ama eneo. Kama ni dawa je sio sahihi?! Au hazitibu ?! Au ni sumu.. je hizi dawa hazifai? Au kama ni mtoaji hiyo tiba kuwa hana ujuzi uhitajikao...!? Ni kipi kilichofungiwa kati ya hivi?!!
 
toka aanze kutibu watu mbona sijawahi sikia alopona??????

Labda pia umewahi sikia aliyekufa.. baada ya kutumia hizi dawa!! Ni vema ukatujuza.. japo suala la kupona ama kutopona ajuaye ni mola baada ya watoa tiba kutimiza wajibu wao. Ndo maana madaktari pia humuamini Mungu. Je hakuna walioenda mhimbili hosptali ya Taifa na hawajapona?! Au walioenda Apolo india na wakafa?! Hoja ni Je hizo dawa zinatibu kweli ni vema vikatumika vigezo vya kisayansi kukanusha. Na sio sera na siasa. Sbb kumbukeni pia biashara ya dawa inaendeshwa na makampuni makubwa yenye mkono wake kiuchumi.
 
Timu ya matapeli inashughulikiwa...
 
Mkeo kutokupona na dawa hazifai? Wako hakupona wengine wanapona, ugonjwa wa mkeo ulikuwa wa maombi, wewe unaenda tiba mbadala, angeponaje? Sema hukua umegundua tatizo mapema, hata tiba mbadala inashauriwa upine ujue unaumwa nini, ili wajue unatumia, malimao au mapera. Nahofia kesho hukawii kusema hospitali ya Appolo India ifungwe na madaktari wafungwe kisa Kuna mgonjwa mtanzania kafia huko juzi.
 
Sawa na yule tapeli Isaac Ndodi, yani mtu ana promote huduma ya afya kama anasa, ama babu wa kikombe wanaachaje kufungua hawa watu jamani, ama hakuna sheria ya kutetea haki za wagonjwa jamani
 

duuuh!
 
waache wayafungie hayo madokta . Kazi kuwalandua wagonjwa kwa bei za kufa mtu ! Madawa yenywe hayatibu chochote !

Dah nimegharimika sana kwa huyu jamaa bado wife hakupona, mpaka alipo fanyiwa upasuaji kariuki hospital ndo kapona, Asante Mungu hatimae wamembaini
 
Huyu ni tapeli kama ma tapeli wengine ingekuwa nchi nyingine kashatundikwa
 
Huyu si ndo aliyeanzisha team mgagani
Afungiwe tu!!!
 
mambo yote mazuri yamehamia

**RADTECH DIAGNOSIS OPOSITY NA DR MWAKA WAO WANATUMIA "IVR" KUSAIDIA AKINAMAMA KUPATA UJAUZITO KWA UHAKIKA ZAIDI KULIKO MITI SHAMBA**
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…