Kituko cha mwaka: Unaweza kumwomba mchepuko wako mchango wa harusi?

Kituko cha mwaka: Unaweza kumwomba mchepuko wako mchango wa harusi?

Mwanaume amwomba Mchepuko wake mchango wa harusi wakati huyo mchepuko ameachika na mume wake. Kaenda mbali zaidi kamkampain awe mwenyekiti wa kamati yake ya harusi, na sisi kama wajumbe tukakubali japo twajua ni mchepuko wake.

Tuambiane kaka/dada unaweza kumwomba mchepuko wako mchango wa harusi?
Je wewe kama mchepuko umeombwa mchango wa harusi wa mke mwenza ilihali wewe ni wa kutumiwa tu utatoa?

Anapokuwa mchepuko haina maana ni adui yako, anaweza kukufanyia mazuri na hata usiamini!! Huo ndio uanaume sasa hahahaaaa!! Ajue kuwa unaoa ili bughudha zipungue alaaa...!!
 
Anapokuwa mchepuko haina maana ni adui yako, anaweza kukufanyia mazuri na hata usiamini!! Huo ndio uanaume sasa hahahaaaa!! Ajue kuwa unaoa ili bughudha zipungue alaaa...!!

inategemea na mchepuko wenyewe' unaweza ukaanzisha ligi coz unajua service zitapungua'
 
Tunafanya jambo kutokana na makubaliano tuliyopeana ... naweza toa....

Busara ni muhimu, na katika nafasi hiyo adimu dalili za mazoea kuzoeana kusikokuwa kwa kawaida kutajitokeza na hapo minong'ono itakaapoanza hata kabla hawajafishana pete rasmi, ndivyo itakavyokuwa ndoa ndoana.
 
Teh kuna maza mmoja hapa nae alikuwa na sendoff ya binti ake wiki kama mbili hivi zilizopita
kwenye kamati kaweka njemba zake nne
katika maongezi si zikajuana kuwa zote zinamla huyo maza!!!!
heee kamati ikawa sio kamati ya sendoff tena ikawa kamati ya ngumi

kuna haja gani ya kuwaweka mahawara kwenye mambo kama haya mxyuuuu

Vikao aina hiyo huwa havikosi mkosi kwa vile watu hujiachia na kuelelezana mengi wayajuayo kuhusu hao wawili katika pilikapilika zao za kufunga ndoa. Paukwa pakawa za hapa na pale haitakuwa vigumu kusoma baadhi ya viashiria vya yaendeleayo huko kunako viunga vya makutano ya mitaa. Maadamu mitaa kadhaa imekutana hapo makutananoni kila uchafu toka mitaa ikutanayo hukuriririkia hapo kunako makutano. Kama kila aliyejiruhusu kuhisi ni yeye tu anaposhtukia amekuwa mwenza nini kitaendelea kama si mtafaruku?
 
Mwanaume amwomba Mchepuko wake mchango wa harusi wakati huyo mchepuko ameachika na mume wake. Kaenda mbali zaidi kamkampain awe mwenyekiti wa kamati yake ya harusi, na sisi kama wajumbe tukakubali japo twajua ni mchepuko wake.

Tuambiane kaka/dada unaweza kumwomba mchepuko wako mchango wa harusi?
Je wewe kama mchepuko umeombwa mchango wa harusi wa mke mwenza ilihali wewe ni wa kutumiwa tu utatoa?


Mchepuko unachuma kwako. Hata makampuni hurudisha sehemu ya faida kwa jamii! Ha ha ha!
 
lingekua jambo la masihara namuweka lakin jambo zito kama hili sithubutu
 
Busara ni muhimu, na katika nafasi hiyo adimu dalili za mazoea kuzoeana kusikokuwa kwa kawaida kutajitokeza na hapo minong'ono itakaapoanza hata kabla hawajafishana pete rasmi, ndivyo itakavyokuwa ndoa ndoana.

Ndiyo tatizo
 
Si kila mahusiano yanaishia kuwa ndoa.kwanza asiyeoa hawi na mchepuko maana bado hajapangiwa route.
 
Back
Top Bottom