miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,805
- 49,104
Kuna mfanyakazi tuliletewa kutoka singida basi nikaenda kumpokea stand then nikawa nampeleka ofisn kwa maza hapo ppf tower ili amuone, atupe na lift ya kwenda home,ile tumefka kwny lift imeanza kupanda juu,nikaona yule dada amechuchumaa lift ilivofunguka nikamuuliza kwann ulichuchumaa akasema nilijua tunapimwa uzito ndo mana nilichuchumaa,hahah!sitamsahau
Ha ha ha nimefurah sana
hahah! Yani mi ningekuwa mamako ningekucharaza
Hahah punguza hasira mkuu!
Sio kwamba najidai wala nini ila ki ukweli sikumbuki kitu chochote ambacho nimewahi kuwa mshamba, ninikumbuka nitakitupia!
Kuna siku jamaa mmoja mgeni kutoka shamba alikuja kwetu kuingia chooni na kuflash sasa yale flash tank huwa
yalikuwa yanapiga kelele wakati maji yanatoka Duh! jamaa alipiga yowe moja alipambana na mlango akitaka kutoka
toi kwa nguvu mwishowe alikuja kupandishia suruali sebuleni.
teh teh! Ningekuchapa tu, huwezi kunitia aibu kiasi hicho, siku nyingine ukiona hizo ndizi unapita mbali kama umemuona simba vile
Usijali sana kwamba hujawahi kukutana na kitu ambacho unaweza kuchangia kama ushamba , yani hivi ulivyochangia kwenye huu uzi tayari nishajua uko mshamba kiasi gani.
Hahah lkn asubuh dingi alivoenda kazin nilipewa kichapo na maza cha kufa mtu afu nikaambiwa ole wako umwambie baba ako!haha
Niliendaga ugenini na ndugu yangu,kufika usiku tukajibaraguza hatukula.Usiku wa manane njaa ikazidi nkajikuta niko jikoni,purukushani za masufuria nikamsikia mwenye nyumba anauliza "nani wewe?"nkajibu nyauuuuuuuuu.Nilpotoka ndugu yangu naye akaingia mwenye nyumba akarudia tena "nani huyo?"jamaa likajibu "nyauuu mwingineee".Nakumbuka enzi hizo nilikuwa sijawahi kuingia Hotelini wala mgahawani,
sasa one day rafiki yangu akanipa offer ile kufika kwenye mgahawa wa kisasa kimtindo si nikaanza kupiga hodiii, hodiiii wacha rafiki yangu aangue kichekoooooo, wewe ulifanya yepi enzi za ushamba