'kwa habari nilizopata tu ni kwamba jamaa alikuwa ni mfungwa wa gereza la butimba alifungwa miaka 30 akatumikia kifungo cha miaka kadhaa ikawa bado kidogo tu atoke yani amalize kifungo chake basi akatoroka wakajaribu kumsaka ikashindikana.
Sasa alivyokamatwa na jezi za polisi wa usalama barabarani kuna aakari mmoja wa magereza akawa amemkumbuka na akatoa report kwa wakubwa na akatambulika kuwa ni yeye hivyo imemlazimu kurudi jela kwanza akatumikie kifungo chake kwa kuwa alitoroka hivyo miaka yote inafutwa anaanza tena 30 na ukijumlisha na kesi ya kukutwa na nguo za serikali pamoja na kesi ya kutapeli na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu sjui atakaa miaka mingapi,pole sana ndugu yetu'
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.