Kituko cha karne!

Joined
Oct 22, 2010
Posts
78
Reaction score
0
Kuna baadhi ya watanzania hii leo wamepokea simu inayodaiwa kutoka kwa mh. Kikwete akiomba apigiwe kura itakayomrudisha madarakani kwa kipindi cha pili. Nashukuru Mungu sikupigiwa simu hiyo. Jambo la kuchekesha na kusikitisha ni pale anaposema atajirekebisha katika makosa yote aliyofanya katika kipindi chake cha uongozi kinachoisha. Binafsi nashindwa kumuelewa huyu mheshimiwa. Sidhani kama hata akipewa miaka 100 kuna chochote kitakachoongezeka hasa ukizingatia ubinafsi uliokithiri wa viongozi katika serikali yake. Ubinafsi uliochochea ufisadi papa wa kutisha, rushwa zilizokithiri na matatizo mengine kibao katika jamii. Sielewi kwa nini mheshimiwa hakuyaongelea hayo wakati wa kampeni badala yake akadai serikali yake imefanya makubwa. Kwa nini aombe msamaa wa makosa aliyofanya gizani?(kwa njia ya simu). Njia hii aliyoitumia mheshimiwa huyu inanifanya niamini kuwa ni kweli yeye pamoja na kundi lake wanahusika katika kumchafua Dr. Slaa ambaye pia alichafuliwa kwa njia hii hii ya simu! Hiki ni kituko kikubwa ambacho hata hivyo hakitamsaidia chochote. Watanzania tumechoka, tunataka mabadiliko! Chagua mh. Dr. Slaa, chagua CHADEMA. Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki uchaguzi mkuu Tanzania.
 
Wengi sana wametumiwa ujumbe jana na kupigiwa kabisa.
Ni upuuzi uliokithiri, na hakuna (hata kuku) anayeweza kutekeleza mwito ana ujumbe kama huo!
Narudia kuwa ni UPUUZI(kwa msisitizo)
 
Wengi sana wametumiwa ujumbe jana na kupigiwa kabisa.
Ni upuuzi uliokithiri, na hakuna (hata kuku) anayeweza kutekeleza mwito ana ujumbe kama huo!
Narudia kuwa ni UPUUZI(kwa msisitizo)

Nashukuru sana kusikia hivyo na ninaamini watanzania wote wanamtazamo kama wako.
 
watanzania, kampeni si ziliisha toka jana? mie pia nilipata simu kama hiyo saa 6.20 usiku. Hii inaweza kuwa ushahidi mzuri sana. na kilichobaki ni wanasheria wetu kukusanya ushahidi huu ili kuandaa kesi dhidi ya JK kama mkiukaji namba 1 wa kuvunja katiba na sheria za kampeni na uchaguzi.
 

Umenena! Hili ni wazo zuri sana. Binafsi nakubaliana nawe kwa 100%. Mabadiliko Tanzania ni lazima!
 
Naogopa kusema kama jamaa ni mweledi au wazimu wake tu wa kilevi cha madaraka.
Mimi nimemsamehe ndo maana namtakia mapumziko ya amani baada ya leo kwani anakuja rais anayejali zaidi ya kutupigia simu.
Ila msamaha zaidi utatolewa baada ya hakimu kusoma hukumu
 
Wengi sana wametumiwa ujumbe jana na kupigiwa kabisa.
Ni upuuzi uliokithiri, na hakuna (hata kuku) anayeweza kutekeleza mwito ana ujumbe kama huo!
Narudia kuwa ni UPUUZI(kwa msisitizo)

Mie mke wangu amezipata hizo simu kalibia week nzima mie nimezipata chahce duu makubwa sana

 
Wengi sana wametumiwa ujumbe jana na kupigiwa kabisa.
Ni upuuzi uliokithiri, na hakuna (hata kuku) anayeweza kutekeleza mwito ana ujumbe kama huo!
Narudia kuwa ni UPUUZI(kwa msisitizo)

Mie mke wangu amezipata hizo simu kalibia week nzima mie nimezipata chahce duu makubwa sana
 
Jamani hizo msg ziwekeni msizifute ili wahusika waweze kufuatilia kwa undani. Tujulishani turipoti kwa nani maana ni ushahidi tosha kabisa wa ukiukwaji wa sheria.
 
mimi nimerudi jana.sikuwepo nchini,but kama ningekuwepo natumaini ningeigiwa simu nyingi sana maana nishatumiwa e mails nyingi sana na watu wake wakinitaka niwe kundi lake,nihamasishe vijana waipigie ccm badala ya chadema,but all in vain.nashukuru kwa kutokuwepo!
 

Kesi chini ya Judge yupi? Ramadhani na team yake? Kumbukeni aliwachagua yeye kwa utashi wake. Rejeeni kesi ya Mgombea binafsi na yaukikwaji wa gharama chini ya Tendwa.
 
na mimi nimepigiwa simu majira ya 6pm naona ilikuwa recorded
kinachonipa wasi wasi ni kwamba kumbe simu haina siri? kumbe mtu anaweza kukufanya chochote kwa simu?
Naona waliopigiwa simu ni watu wa mikoa ya wapinzani akina shimbon wapare waarusha and like
 
Peronally niepata SMS toka kwa JK sijui namba yangu nani kampa?
 
Peronally niepata SMS toka kwa JK sijui namba yangu nani kampa?

Kwa nini msiweke hizo msg, maana inaweza ikawa uzushi tu.kil mtu msg msg, inashindikana nini kuiweka hapa tukaiona. Ni kusubiri matokeo sasa hivi hayo mengine hayana nafasi kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…