kituko cha askari moroko mataa

kituko cha askari moroko mataa

Yaani uanenda mbele hatua tano then unarudi nyuma hatua 13,,,,,,,pangilia maneno khaaa utafikri movie ya kibongo tena ya kichawi
 
Wakuu acheni kuumiza kichwa, kuijadili thread ya mhamiaji haramu ni kujipotezea muda!
 
Kituko cha askari hapo kiko wapi...
kuvua kofia na kuiacha kwenye gari la mtu asiye mfahamu ni sawa na kuacha silaha, pingu nk. labda ikutokee wewe umepaki gari (kama unalo) halafu ukakuta kofia ya polisi juuvya gari lako (narudia tena kama unalo) wakati wakuondoka, ukaichukua na kumuulizia mwenyewe wakaja askari wakakupiga kisha wakakuweka lock up.
 
pale moroko mataa kama una tokea shopaz mkono wa kushoto kuna mabanda ya mama ntilie ambapo wafanyakazi wengi wa ofisi za jirani huwa wanakwenda kula mchana, hapo hapo huwa askari wa usalama barabarani, na hawa wa pikipiki al maarufu kama tigo huwa wanajikusanya wakiwa katika shughuli zao siku ya janaa tarehe 3/3/16 saa sita na dakika kadhaa nilienda kupata lunch, wakaja jamaa fulani na kagari chao wakapaki nao wakajumuika kupata chakula cha mchana, akaja askari wa kike akavua kofia yake na kuweka juu ya gari hilo bila kujua gari ni la nani (nadhani alikwenda msalani) wale jamaa walipomaliza kula wakaingia kwenye gari tule dereva akaichukua ile kofia na kuingia nayo kwenye gari huku akimuulizia mwenye kofia, askari waliokuwepo eneo la tukio waliinuka na kuanza kumshambulia kwa matusi, wakati hio wote yule mwezake aliyekuja na gari alikuwa anachukua video kwenye simu walipomgundua walimpora simu na kumpiga sana kisha kumpeleka oyster bay police walihamaki kugundua kumbe jamaa waliyemkamata ni mtu anayejielewa sijui hii imekaaje.
Sijaelewa unataka tujadili kitu gani hapo?au ulikuwa una maanisha kitu gani?
 
Dah...mkuu rudi shule kidogo ukamalize hata darasa LA saba
 
Kosa lake hapo ni kuwarekodi video ya nn? Yy asingeingia na kofia ndani ya gari, angeichukua na kuwauliza ni ya nani? Unaona sasa kalazwa jela bila sababu na kutoka ni mpaka hela, duuu kayataka mwenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom