Kitu kidogo analia

Kitu kidogo analia

mutant gene

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
876
Reaction score
326
Habari zenu wakuu

Kuna huyu shemeji yangu (mke wa rafiki yangu) akifanywa kitu chochote yeye analia. Mfano akifanya kosa, jamaa akijaribu kumkanya analia, akiambiwa kitu chochote hata kama ni utani analia, jamaa akichelewa kurudi kazini mke analia! anadai ana mwanamke mwingine ndio maana anachelewa kurudi wakati jamaa hayupo hivyo kabisa, ila ikitokea mke amechelewa kurudi jamaa anauchuna kimya life linaendelea.

Leo jamaa ametualika kwake nikaenda na wife. Sasa wakati wa mazungumzo ya hapa na pale jamaa yake akaropoka kumwambia mkewe" unamuona mwenzio( mke wangu) anafanya mazoezi kila siku sio wewe unakaa unanenepeana hovyo" eeeeee akaanza kulia huku akiongea " najua siku hizi hunipendi ndo mana kila siku unachelewa kurudi unapitia kwa hawara zako" akainuka akaelekea ndani kuendeleza kilio.

Jamaa anasema wakati wa uchumba hakuwa hivyo ila mwanzoni alifikiri ni mapepo akampeleka kanisani kuombewa lakini hakuna mabadiliko. Jamaa naye anasema amechoka hiyo tabia na inamkera.

Me nimemshauri ampe mimba. kwa ushauri wangu huu nipo sawa wakuu? au ni ushauri gani unaweza kumpa jamaa ukamsaidia jamaa?
 
habari zenu wakuhu,

kuna huyu shemeji yangu (mke wa rafiki yangu) akifanywa kitu chochote yeye analia. mfano akifanya kosa, jamaa akijaribu kumkanya analia, akiambiwa kitu chochote hata kama ni utani analia, jamaa akichelewa kurudi kazini mke analia! anadai ana mwanamke mwingine ndio maana anachelewa kurudi wakati jamaa hayupo hivyo kabisa, ila ikitokea mke amechelewa kurudi jamaa anauchuna kimya life linaendelea.

Leo jamaa ametuhalika kwake nikaenda na wife. sasa wakati wa mazungumzo ya hapa na pale jamaa yake akaropoka kumwambia mkewe" unamuona mwenzio( mke wangu) anafanya mazoezi kila siku sio wewe unakaa unanenepeana hovyo" eeeeee akaanza kulia huku akiongea " najua siku hizi hunipendi ndo mana kila siku unachelewa kurudi unapitia kwa hawara zako" akainuka akaelekea ndani kuendeleza kilio.

jamaa anasema wakati wa uchumba hakuwa hivyo ila mwanzoni alifikiri ni mapepo akampeleka kanisani kuombewa lakini hakuna mabadiliko. jamaa naye anasema amechoka hiyo tabia na inamkera. me nimemshauri ampe mimba. kwa ushauri wangu huu nipo sawa wakuu? au ni ushauri gani unaweza kumpa jamaa ukamsaidia jamaa?


kaugonjwa kazuri.....
 
Hakutegemea kuolewa,so ana hallucinate.Fully absent minded wife and it surely (sobbing)catches her without an awareness.
 
Sasa mimba itamfanya aache kulia ama connection ya mimba na kilio iko wapi?

ndio inaweza isiwe na connection yeyote kati ya mimba na kilio ila si unajua mkuu katika kutafuta soln. labda akizaa anaweza akapunguza maana akili yake yote itahamia kwa mtoto.
 
huyo nae ana mambo ya kitoto kulia lia kila saa..mimba inaweza kusaidia akili yake ikatanuka akawa anajielewa.
 
mwambia jamaa kila anapolia amgegede,anamgegeda hivyo hivyo akilia aone kama mpaka mwisho wa gemu ataendelea kulia au atakata kiuno na kugunia utamu
 
mkuu ni kweli huyo wife anamapepo mshauri jamaa abadilishe kanisa coz hilo alilompeleka limeshindwa kuyatoa
 
Katika afya ya akili sio kitu cha ajabu sana, kinatokea kwa baadhi ya watu hasa wanaojikuta katika hali ya kushitukizwa na kitu kwa muda mrefu, kutoamini walichonacho au kuwa na hisia kali za hitimisho. its a delusionism or type of phobia anaweza tibiwa kwa njia ya ushauri kwa wataalamu wa afya ya akili.

Ni kama kitu cha ajabu lakini kipo, na ikiachwa iendelee bila tiba ushauri inaweza kumpa shida hata wakati wa ujauzito kama ulivyo mshauri jamaa yako amchape mimba. Anaweza kushindwa kumsukuma mtoto wakati wa kujifungua na unajua madhara yake. Nenda jukwaa la afya kule atasaidiwa huku ni kituko cha changamoto, kuchekesha au kukosolewa.
 
Mmmhhh makubwa kulialia hovyo sasa akiwa na mimba si ndiyo atalia kila baada ya dakika akijiskia tu vibaya kidogo mume hayupo tayari kilio anajidekeza tu bhana
 
uyo ana afadhali muda utafika kulia lia atawaachia watoto je angekuwa vuvuzela?
 
Ndio ila hakustahiki kumwambia maneno kama hayo mbele yaa mgeni

Si ulikuwa utani tu? Hayo maneno ni ya kawaida sana kama yeye na mke wake wana mahusiano ya kirafiki, na pia kama wageni (mtoa mada) wana mahusiano ya kirafiki na mhanga. Ni kawaida kabisa utani wa namna hiyo. Kuna tatizo la msingi na hilo ndio la kushughulikia.
 
Back
Top Bottom