Kitu gani unachoweza kumfanyia mtu aliyekufa kwa namna kuonyesha ulimthamini?

Kufata yale mazuri aliyokua anayatenda na kumuombea dua njema huko alipo (sio uende makaburini, hapo hapo home)
 
ya kikibomoka au kubomolewa kutokana na kupitwa na wakati ndipo amali yake inapoishia hapo, tukiamini kwa miaka hiyo kilipokuwa kinatumika kashapata malipo yakumtosha huku alipo.

kwa wale ambao hawana watoto inabidi wajijengee wenyewe wakiwa hao, na wale wenye watoto wanaokuwa wafanya maasi daily wazazi wao pia watapata sehem ya dhambi za watoto wao (kama hawakuwajibika kuwalea kwenye maadili mazuri). Hili linatupa funzo, tuwalee watoto katika maadili mazuri kwa maana wakijua kufanya wema watatusaidia hata kama tutakuwa tushakufa na tukiwalea vibaya tutawajibika kwa mabaya yao pia.

All in all kuwa responsible na kila tendo ulifanyalo, kuanzia kuwalea wanao, kuishi na jamii yako (majiran na nduguzo), mpaka kazini kwako pia
Ahsante kwa ufafanuzi ndugu. Japo kwa mtazamo wangu mtu akishakufa hakuna chochote kinachoendelea kwa upande wake. Hana ufahamu wa chochote kinachoendelea huko ahera au huku duniani hadi siku ya kiama. Hivyo hawezi kuathiri maisha ya ndugu zake walio hai na pia ndugu zake waliobaki hawawezi kuathiri hali yake (ufu wake) aidha kwa kuombewa sana au kutolewa sadaka ili apate thawabu huko aliko na kuondolewa au kupunguziwa makali ya adhabu yake huko ahera. Yeye kama yeye alitakiwa ajisafishie njia yake alipokuwa hai huku duniani na si vinginevyo.

Hivi kweli mtu aliye hai anapokuwa katika usingizi tu wa kawaida anashindwa kuelewa kinachoendelea nje ya usingizi wake iweje aliyekufa ajue yanayoendelea duniani hadi kufikia kuathiri mwenendo wa maisha ya wapendwa wake aliowaacha?

Au kama sisi tulio hai tunashindwa kujua kinachoendelea kwa ndugu zetu waliokufa iweje iwe rahisi tunapokufa eti ndipo tupate uwezo wa kujua yanayoendelea duniani kwa ndugu zetu walio hai?

Hivyo nionavyo katika kuwaenzi wazazi au wapendwa wetu wengine waliotangulia kaburini cha kwanza kabisa ni kuwalindia heshima yao. Mfano kama aliacha deni lolote basi tuwalipie madeni yao kwa kadri inavyowezekana na kwa upendo, kutunza familia yake kwa kutoa ushauri na/au fedha ili kutatua shida mbalimbali za kimaisha kama zipo n.k.

Pili kuchambua mema na mabaya ya huyo mpendwa wako kwa hekima. Kisha kuishi katika mema aliyokuwa akiyafanya au kuyahimiza na pia kuepuka kutenda au kuishi katika yale yalioonekana kama mabaya ya huyo mpendwa wako. Sasa katika kutenda mema ndipo unaweza kupanua wigo kwa kuyafikisha na kunufaisha jamii kubwa zaidi kama vile kujenga msikiti, kanisa, shule, hospitali, kutoa misaada kwa yatima, wajane na wengineo wenye uhitaji halisi.

Pamoja na hayo katika kufanya hayo mema isiwe kwa ajili ya kumtafutia thawabu marehemu bali kwa ajili ya kujisafishia njia sisi wenyewe tulio hai. Hii ni kwa sababu na sisi tukiondoka duniani tusitegemee kwamba kutakuwa na maombi au sadaka kutoka kwa ndugu au rafiki itakayoweza kubadilisha ukweli wa matendo yetu (mema au mabaya) tuliyoyatenda tukiwa hai ambayo ndiyo yatakayoamua adhabu na thawabu yetu siku ya kiama.
 
wakuu heshima kwenu , naomba kuuliza nifanye nini kwaajili mama yangu alieniacha mchanga sana (miezi 3) na bibi yangu alienilea nae alikufa kabla sijawa hata na uwezo wowote, najisikia kuwiwa sana kwaajili yao. nitoe sadaka gani kuonyesha thamani yao
Kwanza nakupa pole sana.wote waja wa mwenyezi mungu na kwake tutarejea.
Pili hakikisha unamuombea dua za kumrehemu kila unapofanya ibada zako
Tayu zuru kaburi lake kila upatapo nafasi na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu
Tatu mtolee sadaka jalia .unaweza kujenga kisima cha maji watu wakateka maji bure au ukajenga darasa moja la watu kupata elimu
Au ukajenga msikiti au kanisa.kwa ujumla sadaka jalia ina nguvu sana kuliko sadaka ya aina yoyote.Kitu endelevu kinachotumiwa na waumini wengi wawe wakiristo auwaislamu ni bora zaidi.
 
Hi ya kuwapa majina watoto ya urithi ni swala la kuangalia sana maana ya majina yenyewe na tabia za wenye majina wenyewe.


Binafsi na amini athari katika majina


Ukipata watoto wa kike wape majina ya hawa wapendwa wako (mama na bibi). Kwa kufanya hivi utakuwa umewarudisha tena hapa duniani.

Na kadri utakavyowahudumia vizuri hawa mabinti zako ndivyo hivyo hivyo utakavyokuwa unawaenzi mama na bibi yako.
 
watend wengne mema ndugu, IKBID TAFTA MTOTO YATIMA UMLEE UKU UKJIAMINISHA KUWA UNAMLPA BIB AKO FADHIRA
 
Chagua shule moja ya msingi kijijini kwenu. Jenga chumba cha darasa and then dedicate the classroom to your loved ones. Itakuwa ni kumbukumbu yako kwa siku zako ambazo Mwenyezi Mungu amekupa hapa duniani. Na vile vile ukifanya hivyo utakuwa umewaenzi kwa kusaidia wale wenye uhitaji. Na hakika hii zawadi itanufaisha wengi kupitia elimu.
 
Yes, umefafanua vema. Watu wengi wanatumia baadhi ya maneno bila kujua maana yake.

Ushirikina in kumshirikisha Mungu na vitu/viumbe wengine.

Mfano, watu wengi wanasema: Mtume Muhammad (SAW) naomba unisaidie/Yesu naomba unisaidie/mizimu ya kwetu nisaidieni.. Huu ni ushirikina. Anayesaidia,anayeokoa ni Mungu pekee na so mwingine.

Au kusema Yesu/hirizi ni kinga..huu ni ushirikina. Kinga ni Mungu pekee
Mkuu Mbavu za Mbwa usimlinganishe YESU na mavitu ya ajabu ajabu!

Kayaulize majini YESU ni nani kama bado hujamfahamu!
 
Pia usisahau ukizaa watoto waite majina ya marehemu kama njia ya kuwaenzi. Hata barabara, viwanja vya ndege, kumbi za starehe huitwa majina ya watu maarufu ili kuwaenzi
 
Mtu aliyekufa ukurasa wake tayari ulishafungwa tenda mema kwa walio hai ukifa na wewe ukumbukwe kwa wema.
Makanisa, misikiti, mahekalu, barabara, madaraja, majengo, nyumba, maghorofa, maeneo, viwanja vya ndege, nk yamepewa majina ya wafu. Jiulize kwa nini vitu vipewe majina ya wafu
 
Waombee dua kwa Mungu awasamehe makosa yao
Hakuna kitu kama hiki, mkuu usiendelee kujiriwadha kwa methali za wahenga. Mara baada ya mauti n hukumu.

Jamaa ajitahd kufanya mambo kwa kiwango kile kile ambacho angetamani awafanyie hao waliotangulia.
 
Makanisa, misikiti, mahekalu, barabara, madaraja, majengo, nyumba, maghorofa, maeneo, viwanja vya ndege, nk yamepewa majina ya wafu. Jiulize kwa nini vitu vipewe majina ya wafu
Hata mimi nimemshauri atende wema kwa walio hai ili siku moja wamkumbuke kwa mema yake, hizo facilities zinazoitwa majina ya wa tenda mema.
 
Idea yako ni nzuri ...ila ss ukimpa mtoto jina la mtu mwingine mfano hvyo jina la bibi au mama wanakua wanatabia sawa na aliyekua na jina hilo...Je unajua tabia zao??? vya kurithi zinazidi
Kwa hiyo ukimpa mtoto wako jina la Yohana Mbatiizaji (John), au mtume Muhammad (SAW), hivi unajua tabia zao zote hawa mitume mpaka kumpa kijana wako jina lao?
 
Utawaambiza mashetani bure. Usithubutu kuchukua ushauri huu
Kwa hiyo ukimpa binti yako jina la Aisha (mke wa mtume) au Mary-Magdalena (mfuasi wa Yesu anaesemekana alikuwa changudoa) utakuwa umewainua mashetani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom