Kitu gani unachoweza kumfanyia mtu aliyekufa kwa namna kuonyesha ulimthamini?

Mbona wanao umewapa majina ya kigeni? Je huo ni ushirikina?
nItawapa majina mazuri ninayoyapenda, yanayopendwa, hata liikiitwa watu wanafurahi, sio majina ya watu wema waliopita halafu mnayatumia vibaya, au watoto warithi mizigo ya watu waliopita.

Kwa mfano tutegemee mtoto aitwe nyerere afanye yalifanywa na nyerere? asipofanya kama nyerere ndio mnaanza kuroga hapo.

Elimu iwasaidie jamoni
 
Hi ya kuwapa majina watoto ya urithi ni swala la kuangalia sana maana ya majina yenyewe na tabia za wenye majina wenyewe.

Binafsi na amini athari katika majina
Kwa hiyo majina yote ya dini ya watakatifu (wafuasi wa mtume) wa zamani ni vibaya kuwapa kwa sababu ukisoma historia zao wengi walikuwa na tabia za ajabu ajabu sana maishani mwao.
Kutenda yale ambayo angependa utende, mfano kuwa na furaha na kuendelea na maisha
in real mtu alo kufa anakuwa hayupo, hasikii, haoni, hapumui so haipo haja sana ya kumuonesha una mthamini ikiwa akiwa hai ulishndwa kumuonesha hivo.
tujitahid kuwaonesha watu tuna wathamini wakiwa hai na wakitangulia tuwaache wapumzike
 
nItawapa majina mazuri ninayoyapenda, yanayopendwa, hata liikiitwa watu wanafurahi, sio majina ya watu wema waliopita halafu mnayatumia vibaya, au watoto warithi mizigo ya watu waliopita.

Kwa mfano tutegemee mtoto aitwe nyerere afanye yalifanywa na nyerere? asipofanya kama nyerere ndio mnaanza kuroga hapo.

Elimu iwasaidie jamoni
Huyu Nyerere si aliitwa Julius? Sio kila Julius ni Nyerere na sio kila Nyerere ni julius. Mwanao Kumwita Julius kuna kosa gani?
 
nItawapa majina mazuri ninayoyapenda, yanayopendwa, hata liikiitwa watu wanafurahi, sio majina ya watu wema waliopita halafu mnayatumia vibaya, au watoto warithi mizigo ya watu waliopita.

Kwa mfano tutegemee mtoto aitwe nyerere afanye yalifanywa na nyerere? asipofanya kama nyerere ndio mnaanza kuroga hapo.

Elimu iwasaidie jamoni
Akifanya aliofanya Nyerere ndio itakuwa sawa? Unajuwa Nyerere aliwatia kizuizini wapinzani wake bila kuwapeleka mahakamani (preventive detentions) kwa muda mrefu sana. Kwa hiyo ukimpa mtoto wako jina la Nyerere unadhani atarithi kila kitu au atarithi hizi mystical sifa za baba wataifa asiepokea rushwa?

Yaani watu nyie ni very superstitious. Kumpa mtoto jina la mtu ni kumrithisha hata tabia zake nzuri na mbaya?

Kama ni hivyo basi watoto wangu wote (wakike na wakiume) ningewaita ALBERT EINSTEIN ili niwe na mjiniasi watupu. Acheni fikra za kichawi hizo.
 
Hapana mkuu.

Kumuenzi mama yako kwa kumpa binti yako jina lake ni ushirikina? Sidhani kama unajua maana ya ushirikina.

Hii ni kuweka kumbukumbu ya mama yako iwe hai siku zote unapomuona binti yako. Kila unapomuita binti yako inakukumbusha mama yako.

Ni dini gani hiyo inayosema huu ni ushirikina? Ihame dini hiyo tafuta dini nyingine. Dini hiyo inakupotosha kiasi cha kwamba hata kuwaenzi wahenga zako inakuwa shirk.

Maana ya SHIRK
Katika dini ya Kiislamu SHIRK ni kushirikisha kitu au mtu yeyote na uwezo wa Mungu. Mfano kuweka nadhiri kaburini kwa marehemu kuwa akusaidie kitu fulani.

Nilikwisha elezea kirefu hapo nyuma humu humu JF kuhusu SHIRK na KAFARAH.
Tufikirikie ki THINKERS, hIVI UMEZAA WATOTO WAnne, MMOJA ukishamuita jina la mamako, hawa wengine utawadharau?utawa nini?

Kikubwa ni kwamba tumche mwenyezi mungu, hata mama etu akifariki unapaswa kumfanyia makubwa sio kurithisha jina kwa mwanao, kama unazungumzia dini nimezama zaidi, wew kama mtoto kwa kidini mzazi ana vitu vikuu kutendew directly sio kumpa mwanao jina, mpe mwanao jina alipende, kama ni bibiake fine, mpe....tatizo .com imewapumbaza
 
Akifanya aliofanya Nyerere ndio itakuwa sawa? Unajuwa Nyerere aliwatia kizuizini wapinzani wake bila kuwapeleka mahakamani (preventive detentions) kwa muda mrefu sana. Kwa hiyo ukimpa mtoto wako jina la Nyerere unadhani atarithi kila kitu au atarithi hizi mystical sifa za baba wataifa asiepokea rushwa?

Yaani watu nyie ni very superstitious. Kumpa mtoto jina la mtu ni kumrithisha hata tabia zake nzuri na mbaya?

Kama ni hivyo basi watoto wangu wote (wakike na wakiume) ningewaita ALBERT EINSTEIN ili niwe na mjiniasi watupu. Acheni fikra za kichawi hizo.
tawire
 
Tufikirikie ki THINKERS, hIVI UMEZAA WATOTO WAnne, MMOJA ukishamuita jina la mamako, hawa wengine utawadharau?utawa nini?

Kikubwa ni kwamba tumche mwenyezi mungu, hata mama etu akifariki unapaswa kumfanyia makubwa sio kurithisha jina kwa mwanao, kama unazungumzia dini nimezama zaidi, wew kama mtoto kwa kidini mzazi ana vitu vikuu kutendew directly sio kumpa mwanao jina, mpe mwanao jina alipende, kama ni bibiake fine, mpe....tatizo .com imewapumbaza

Utamaduni wa kuwapa watoto wetu majina ya wakina mama, baba, wajomba, mababu na mabibi ni utamaduni wa kitanzania au niseme wa kiafrika. Sijui una asili ya mkoa gani lakini jina la mama yangu mzazi au mama-shangazi siku zote litakuwa linanipendezea sana kuliko majina ya mitume na manabii wa zamani.

As a great thinker utajua kuwa familia au koo zina wahenga wengi wa kuenziwa. Ukishampa mtoto jina la mama yako, basi kuna ndugu zake wengi tu walibaki ambao ungependa kuwaenzi pia kwa kutumia majina yao.

Sio lazima uwape watoto majina ya wazee wako wa ukoo lakini ukifanya hivyo utakuwa imewapa heshima kubwa sana.

Unaweza kumpa kijana wako jina la nabii Issa (bin Mariam) au ukampa jina la babu yako Mihayo. Ukiniuliza mimi ningechagua Mihayo badala ya Issa.

Tusiwadharau wahenga wetu eti tu kwa kuwa kuna majina mengi ya kizungu au kiarabu.
 
Kitu cha kwanza ambacho marehemu amekiacha duniani ni Mtoto Mwema mwenye kumuombea dua. Kama huwezi unawaona Viongozi wa Dini.

Pia kuna vitu vinaitwa Sadakati jalia yaani kufanya kitu chenye kutoa dhawabu za kudumu kwa kunuia Gawio la Dhawabu zifike kwako mwenyewe au kwa Marehemu uliowakusudia mfano :

1. Kama umejaaliwa pesa mingi mkuu fungua kituo cha kulea watoto yatima kwa haki Kabisa na mwambie Mungu kwamba unapenda dhawabu zote zitokalo katika kituo hicho ziwafikie hao mama na bibi au unakiita Kituo kwa Majina yao kuwaenzi.

2. Kulipia Ada Yatima, Masikini na Mafukara.
3. Kujenga Misikiti
4. Kununulia watu vitabu vya elimu inayowaletea manufaa.
5. Kujengea nyumba masikini na mafukara
6. Kuweka utaratibu wa kulisha masikini na kusaidia wasiojiweza
7. Kununulia Mavazi Yatima, Masikini na Mafukara.
n. k, n. k.
 
Utamaduni wa kuwapa watoto wetu majina ya wakina mama, baba, wajomba, mababu na mabibi ni utamaduni wa kitanzania au niseme wa kiafrika. Sijui una asili ya mkoa gani lakini jina la mama yangu mzazi au mama-shangazi siku zote litakuwa linanipendezea sana kuliko majina ya mitume na manabii wa zamani.

As a great thinker utajua kuwa familia au koo zina wahenga wengi wa kuenziwa. Ukishampa mtoto jana la mama yako, basi kuna ndugu zake wengi tu walibaki ambao ungependa kuwaenzi pia kwa kutumia majina yao.

Sio lazima uwape watoto majina ya wazee wako wa ukoo lakini ukifanya hivyo utakuwa imewapa heshima kubwa sana.

Unaweza kumpa kijana wako jina la nabii Issa (bin Mariam) au ukampa jina la babu yako Mihayo. Ukiniuliza mimi ningechagua Mihayo badala ya Issa.

Tusiwadharau wahenga wetu eti tu kwa kuwa kuna majina mengi ya kizungu au kiarabu.
Cha kuwa makini nacho tu ni kwamba jina linaathiri tabia za mtoto hivyo tuangalie tabia za watu tunaowapanga majina watoto hata kama ni wazazi au ndugu.
 
Kwa hiyo mkuu nikimpa mtoto wangu jina la Isaac Newton, au Galileo Galilei, au Hubble, n.k. basi yeye atakuwa jiniasi kama hao namesake wake? Sidhani!

Atakuwa na weledi na uwezo kadri mimi kama mzazi nitakavyomuwezesha. Nothing more, nothing less.
 
Sijasema majina tote nielewe Mkuu.

Unazani kwanin watu hawawapi watoto wao jina kama FARAO badala yake wanawaita DAUD IMANUEL SELEMAN JOSHUA MUSA n.k?

Binafsi naamin wanaamin ndan ya jina Farao kuna matokeo mabaya.

Mama aliitwa Sikujua tangu udogoni ameishi maisha ya mateso ujanani amekuwa kahaba uzeen amekuwa mganga wa jadi atimaye amezikwa hali ya kuwa jamii imefurahi bora amefariki.

Bila shaka yoyote atabaki ni mama yangu kipenz lakin sitafika hatua ya kumrithisha mwanangu jina Sikujua.

KUMBUKA:mimi binafsi

Kwa hiyo majina yote ya dini ya watakatifu (wafuasi wa mtume) wa zamani ni vibaya kuwapa kwa sababu ukisoma historia zao wengi walikuwa na tabia za ajabu ajabu sana maishani mwao.
 
Sijasema majina tote nielewe Mkuu.

Unazani kwanin watu hawawapi watoto wao jina kama FARAO badala yake wanawaita DAUD IMANUEL SELEMAN JOSHUA MUSA n.k?

Binafsi naamin wanaamin ndan ya jina Farao kuna matokeo mabaya.

Mama aliitwa Sikujua tangu udogoni ameishi maisha ya mateso ujanani amekuwa kahaba uzeen amekuwa mganga wa jadi atimaye amezikwa hali ya kuwa jamii imefurahi bora amefariki.

Bila shaka yoyote atabaki ni mama yangu kipenz lakin sitafika hatua ya kumrithisha mwanangu jina Sikujua.

KUMBUKA:mimi binafsi
Lakini mkuu huoni kuwa una-generalize sana. Yaani wazazi wote watakuwa na tabia hizo mbaya kufikia kutofaa kupewa watoto majina yao (mabibi au mababu)?

Kumbuka mleta mada amewakumbuka mama na bibi yake kwa wema waliomfanyia katika maisha yake. Nani atakaesema hawa wanawake (mama na bibi) hawana sifa za kurithishwa mabinti zake?

Yaani aache kumuita binti yake kwa jina la huyu bibi na badala yake ampe jina la Mary-Magdalen, mfuasi wa Yesu aliekuwa changudoa maishani mwake?
 
Hah hah hah Mkuu hapana siwezi kamwe kuwahusisha wazazi wote katika tabia hizo.

Ila nilitoa angalizo la MTU mwenye kuamini kama ninavyoamin Mimi ya kuwa endapo unataka kumpa mwanao jina LA urithi LA MTU ambae tena ni marehemu ni vizuri ukajiridhisha na tabia ambazo alizikumbatia ama zilimkumbatia huyo marehemu.

Hii nazan hata mwanao akiambiwa hili jina ni la bibi ama nyanya yako atajihisi nafsin mwake kwa namna ambayo atasimuliwa walikuwa ni watu wa namna gani.

Lakini mkuu huoni kuwa una-generalize sana. Yaani wazazi wote watakuwa na tabia hizo mbaya kufikia kutofaa kupewa watoto majina yao (mabibi au mababu)?

Kumbuka mleta mada amewakumbuka mama na bibi yake kwa wema waliomfanyia katika maisha yake. Nani atakaesema hawa wanawake (mama na bibi) hawana sifa za kurithishwa mabinti zake?

Yaani aache kumuita binti yake kwa jina la huyu bibi na badala yake ampe jina la Mary-Magdalen, mfuasi wa Yesu aliekuwa changudoa maishani mwake?
 
Kwa hiyo mkuu nikimpa mtoto wangu jina la Isaac Newton, au Galileo Galilei, au Hubble, n.k. basi yeye atakuwa jiniasi kama hao namesake wake? Sidhani!

Atakuwa na weledi na uwezo kadri mimi kama mzazi nitakavyomuwezesha. Nothing more, nothing less.
Jaribu kumwita Shida, masumbuko, Sikujua, Walivyo, Vituko,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom