Kitu gani umebeba kwenye wallet chenye kuonyesha utambulisho wako?

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
5,951
23,276
Ngoja nianze na mifano.

Wiki tatu zilizopita kulitokea ajali ya roli na bodaboda maeneo ya kongowe barabara ya Kilwa, licha ya bodaboda kufariki papohapo ila mwili wake ulikuwa kama chapati, sura yake haikujulikana kabisa maana ilipondeka.

Mashuhuda walipofika eneo la ajali wakamkagua maiti hawakukuta na chochote cha maana chenye kumtambulisha yeye ni nani maana simu ilipotea, hakujulikana nani ameiba kwenye lile tukio, kabla hajapata ajali kwenye pikipiki alibeba bango la biashara na kwa bahati mzuri walipodesign lile bango kulikuwa na namba za hapo kwenye biashara linapoenda kufungwa.

Mashuhuda wakaamua kupiga zile namba za kwenye bango simu ikapokelewa "haloo naongea na nani mwenzangu"
Simu upande wa pili ikajibu "kuna mtu alikuwa amebeba bango kwenye bodaboda, isivyo bahati amegongwa na roli na amefariki hapohapo, sasa hili bango wewe ndiyo muhusika?" Jamaa akajibu ndiyo ingawa alikuwa kama amepigwa na butwaa.

Fasta jamaa akafika eneo la tukio maana marehemu alikuwa karibu na destination (bango lilikuwa linaenda Kongowe hapohapo)

Jamaa aliyepigiwa simu na mashuhuda wa ajali alipofika eneo la tukio akamtambua huyu marehemu ni graphics designer ambae wiki iliyopita alimpa kazi ya kutengeneza bango ofisi yake ipo Tandika. So faster wakatoka baadhi ya watu wakaenda tandika kutoa taarifa kwamba ndugu yenu amefariki Kwa ajali..Msiba!!!

Stori nyingine
Umeshawahi kuendesha gari usiku barabara ya kibada-tua Ngoma? Ile barabara ni nyembamba ilijengwa kizamani.Sasa upo kwenye kigari chako sijui Impreza,vitz,Passo au IST usiombe ukutane na roli la mchanga (serera).Wale jamaa ukipishana nao unaweza hisi umekumbwa na kimbunga.

Kwanza magari Yao ni mapana sn alafu wanapita katikati ya barabara na kukuachia nafasi kidogo sn ya kupishana nae.Kiufupi ukikutana na serera ongeza umakini maana ukigongana nalo moja Kwa moja unaenda kuamkia mbinguni Kwa baba

Kwa kifupi nataka niseme kwamba;ukigongana uso Kwa macho na roli la mchanga(mtaani tunayaita serera),uwezekano wa kupona ni mdogo sana,pia uwezekano wa kutotambulika utakuwa ni mkubwa Sana maana utapondwa wewe na gari

R.I.P MAUNDA ZORO.Nasikia alikuwa ktk vitz akakutana na serera-roli la mchanga(ingawa kuna tegesi kwamba alikuwa anaendesha huku akiwa amelewa kisha akalivamia roli)..so sad!!

Mifano ni mingi sn.nimewahi kushuhudia mtu kaanguka kwenye daladala la kivukoni-mbagala,alizimia Kwa kukosa pumzi maana alisimama sana,foleni haitembei na amebanwa..akafaint

Abiria walipomkagua Kama ana simu au kitambulisho chochote watoe taarifa Kwa ndugu,hakuwa na chochote,hata simu hakuwa Nayo!! Sijui nn kiliendelea maana nilishuka zangu njiani

My point is; Hakuna watu wazembe Kama watanzania

Unakuta Mdada anatoka zake Bunju anaenda kutoa utelezi gongo la mboto,amebeba vitu vyote anavyoona vina umuhimu kwenye kibegi chake,Hadi tishu kwenye handbag ameweka,lkn amekosa kubeba kitu kinachomtambulisha!!

Kutoka Bunju to gomz hapo Kati likitokea la kutokea Nani atakusaidia my friend? Siyo lazima ugongwe na gari au pikipiki,kuna kuzimia ghafla!!

Mwanangu alitoka zake home tegeta anaenda kujenga bagamoyo kabeba 20k kwenye wallet kisha akachukua smartphone yake huyo anasepa,nikampa ushauri wa kubeba chochote chenye kumtambulisha..now somo amelielewa

Unaweza Kusema simu si nimebeba na nimesave namba ya Baba au kuna watu muhimu nimewasave..ndugu yangu kuna watu siku hizi hawana ubinadamu hata kidogo.Mtu anakuchukulia simu na anatoa line na kutupa kisha anatokomea bila taarifa..

Mwili wako utaishia kufanywa km specimen maabara Kwa wanafunzi wa muhimbili maana ulipookotwa haukuwa na utambulisho wowote.Umekaa mochwari zaidi ya mwezi mwishowe unazikwa makaburi ya city pale buza!! Ndugu hawana taarifa

Nimeshuhudia watu kibao wasiofahamika wakizikwa pale makaburi ya city ambao walikaa mochwari muda mrefu hawakujitokeza ndugu zao.wanachimba shimo yanazama magoti Tu kisha wanakufukia,usiku wanakuja mbwa kufukua maana umeshakuwa mzoga!! Ndugu wansema umepotea kumbe umeliwa na mbwa!!

Mimi haijalishi naenda wapi,ukiachana na simu,kwenye wallet yangu nimeweka picha ndogo ya passport size ambayo huku nyuma nimeandika namba tatu za watu wa muhimu ambao wananijua vizuri.Ambao ukipiga simu ukimuuliza kuhusu Mimi atatoa maelezo yaliyonyooka

Pia Ninatembea na copy ya kitambulisho cha utaifa na leseni ya udereva ila sina gari...gari litakuja mbele Kwa mbele

Unatembea na kitu chochote chenye kukutambulisha?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja nianze na mifano.

Wiki tatu zilizopita kulitokea ajali ya roli na bodaboda maeneo ya kongowe barabara ya Kilwa, licha ya bodaboda kufariki papohapo ila mwili wake ulikuwa kama chapati, sura yake haikujulikana kabisa maana ilipondeka.

Mashuhuda walipofika eneo la ajali wakamkagua maiti hawakukuta na chochote cha maana chenye kumtambulisha yeye ni nani maana simu ilipotea, hakujulikana nani ameiba kwenye lile tukio, kabla hajapata ajali kwenye pikipiki alibeba bango la biashara na kwa bahati mzuri walipodesign lile bango kulikuwa na namba za hapo kwenye biashara linapoenda kufungwa.

Mashuhuda wakaamua kupiga zile namba za kwenye bango simu ikapokelewa "haloo naongea na nani mwenzangu"
Simu upande wa pili ikajibu "kuna mtu alikuwa amebeba bango kwenye bodaboda, isivyo bahati amegongwa na roli na amefariki hapohapo, sasa hili bango wewe ndiyo muhusika?" Jamaa akajibu ndiyo ingawa alikuwa kama amepigwa na butwaa.

Fasta jamaa akafika eneo la tukio maana marehemu alikuwa karibu na destination (bango lilikuwa linaenda Kongowe hapohapo)

Jamaa aliyepigiwa simu na mashuhuda wa ajali alipofika eneo la tukio akamtambua huyu marehemu ni graphics designer ambae wiki iliyopita alimpa kazi ya kutengeneza bango_Ofisi yake ipo Tandika. So faster wakatoka baadhi ya watu wakaenda tandika kutoa taarifa kwamba ndugu yenu amefariki Kwa ajali..Msiba!!!

Stori nyingine
Umeshawahi kuendesha gari usiku barabara ya kibada-tua Ngoma? Ile barabara ni nyembamba ilijengwa kizamani.Sasa upo kwenye kigari chako sijui Impreza,vitz,Passo au IST usiombe ukutane na roli la mchanga (serera).Wale jamaa ukipishana nao unaweza hisi umekumbwa na kimbunga.

Kwanza magari Yao ni mapana sn alafu wanapita katikati ya barabara na kukuachia nafasi kidogo sn ya kupishana nae.Kiufupi ukikutana na serera ongeza umakini maana ukigongana nalo moja Kwa moja unaenda kuamkia mbinguni Kwa baba

Kwa kifupi nataka niseme kwamba;ukigongana uso Kwa macho na roli la mchanga(mtaani tunayaita serera),uwezekano wa kupona ni mdogo sana,pia uwezekano wa kutotambulika utakuwa ni mkubwa Sana maana utapondwa wewe na gari

R.I.P MAUNDA ZORO.Nasikia alikuwa ktk vitz akakutana na serera-roli la mchanga(ingawa kuna tegesi kwamba alikuwa anaendesha huku akiwa amelewa kisha akalivamia roli)..so sad!!

Mifano ni mingi sn.nimewahi kushuhudia mtu kaanguka kwenye daladala la kivukoni-mbagala,alizimia Kwa kukosa pumzi maana alisimama sana,foleni haitembei na amebanwa..akafaint

Abiria walipomkagua Kama ana simu au kitambulisho chochote watoe taarifa Kwa ndugu,hakuwa na chochote,hata simu hakuwa Nayo!! Sijui nn kiliendelea maana nilishuka zangu njiani

My point is; Hakuna watu wazembe Kama watanzania

Unakuta Mdada anatoka zake Bunju anaenda kutoa utelezi gongo la mboto,amebeba vitu vyote anavyoona vina umuhimu kwenye kibegi chake,Hadi tishu kwenye handbag ameweka,lkn amekosa kubeba kitu kinachomtambulisha!!

Kutoka Bunju to gomz hapo Kati likitokea la kutokea Nani atakusaidia my friend? Siyo lazima ugongwe na gari au pikipiki,kuna kuzimia ghafla!!

Mwanangu alitoka zake home tegeta anaenda kujenga bagamoyo kabeba 20k kwenye wallet kisha akachukua smartphone yake huyo anasepa,nikampa ushauri wa kubeba chochote chenye kumtambulisha..now somo amelielewa

Unaweza Kusema simu si nimebeba na nimesave namba ya Baba au kuna watu muhimu nimewasave..ndugu yangu kuna watu siku hizi hawana ubinadamu hata kidogo.Mtu anakuchukulia simu na anatoa line na kutupa kisha anatokomea bila taarifa..

Mwili wako utaishia kufanywa km specimen maabara Kwa wanafunzi wa muhimbili maana ulipookotwa haukuwa na utambulisho wowote.Umekaa mochwari zaidi ya mwezi mwishowe unazikwa makaburi ya city pale buza!! Ndugu hawana taarifa

Nimeshuhudia watu kibao wasiofahamika wakizikwa pale makaburi ya city ambao walikaa mochwari muda mrefu hawakujitokeza ndugu zao.wanachimba shimo yanazama magoti Tu kisha wanakufukia,usiku wanakuja mbwa kufukua maana umeshakuwa mzoga!! Ndugu wansema umepotea kumbe umeliwa na mbwa!!

Mimi haijalishi naenda wapi,ukiachana na simu,kwenye wallet yangu nimeweka picha ndogo ya passport size ambayo huku nyuma nimeandika namba tatu za watu wa muhimu ambao wananijua vizuri.Ambao ukipiga simu ukimuuliza kuhusu Mimi atatoa maelezo yaliyonyooka

Pia Ninatembea na copy ya kitambulisho cha utaifa na leseni ya udereva ila sina gari...gari litakuja mbele Kwa mbele

Unatembea na kitu chochote chenye kukutambulisha?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Unajitabiria mabaya japo ukweli ni kuwa uko na point kwa hili.
 
Kwenye ndege kuna parachute,na ardhini ikitua Tu kuna magari ya zimamoto yapo stand by

Kwenye panton pale ferry kuna maboya ya kuogelea endapo itatokea ajali

Kwenye gari kuna airbags

Km watu wangekuwa na mawazo km yako ya endapo utachukua tahadhari ya kitu basi utakuwa umejitabiria mabaya kukutokea,basi matokeo yangekuwa mabaya zaidi ya huko kujitabiria mabaya

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye ndege kuna parachute,na ardhini ikitua Tu kuna magari ya zimamoto yapo stand by

Kwenye panton pale ferry kuna maboya ya kuogelea endapo itatokea ajali

Kwenye gari kuna airbags

Km watu wangekuwa na mawazo km yako ya endapo utachukua tahadhari ya kitu basi utakuwa umejitabiria mabaya kukutokea,basi matokeo yangekuwa mabaya zaidi ya huko kujitabiria mabaya

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Ndiyo maana mwishoni nilisema ni muhimu kuchukua kitambulisho. Au hukuona mstari wa mwisho mkuu
 
Nina kahirizi kadogo kamefungwa na uzi mwekundu kanapumua

Umenikumbusha jamaa aliyekuwa na irizi ndani ya mwili wake,eti endapo ataiba kisha atapigwa na watu hawezi kufa

Siku moja kamwambia mkewe ajaribu kumkata na shoka km anachanja kuni maana alimwambia ukipiga itadunda kwenye mwili.Mke akajipinda kisawasawa,akapiga shoka Ngoma ikakubali..damu hizi hapa

Jamaa badala ya kuugulia maumivu,cha ajabu akawa anashangaa akamuuliza mkewe "shoka limeingia kweli?" ...mganga alimwingiza cha kike akafa Kwa ujinga wa kutegemea irizi

Mkuu mshnaa Wewe siku jichangaje kwenye 18 za serera na Hilo gari lako wakati unatoka zako kilingeni unakuja mjini kutembea ndy utajua serera halichagui mwenye hirizi au asiye Nayo

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma stori zote tatu nimeona wahanga wote ni wenye magari

Watembea kwa ngoko bado tuko safe

Na kama tunafikiria kununua magari cha msingi ni ku deal na hayo malori ili kujiweka salama maana uki stick kwenye IST unazidi kujiweka kwenye risk
Kuna demu mmoja alikuwa anaumwa kifafa.Kama ujuavyo kifafa kinaweza kukuletea amsha amsha popote pale

Siku moja alienda beach kupunga upepo.Akavua nguo aoge,wakati yupo kwenye maji anaogelea kifafa kikaamka

Kufupisha Stori ni kwamba alikufa Kwa kunywa maji mengi..bahati alijulikana maana alitmbea na vitu vinavyomtambulisha

Huyu hakuwa na IST mkuu😅😅
 
Back
Top Bottom