101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,057
- 2,244
#HABARI Vijana wawili ambao ni wezi wa simu kwa kutumia pikipiki maarufu kama 'Vishandu' ambao majina yao hayajajulikana mara moja wamenusurika kuuawa na wananchi katika eneo la Barabara ya Lenana Kilimani Nairobi nchini Kenya baada ya kukwapua simu kutoka kwa mwanamke mmoja na kushindwa kutoroka
Wawili hao waliokuwa kwenye pikipiki walinaswa na wananchi na waendesha bodaboda ambao waliwazunguka na kuwashukia kipigo kabla ya askari wa Kituo cha Polisi Kilimani kufika eneo la tukio na kuwaokoa.
Mashuhuda wanasema watuhumiwa hao walimpokonya simu lakini walipokuwa wakijaribu kukimbia, mwendesha bodaboda mmoja aliwarushia gogo la mbao kwenye njia yao na kusababisha waanguke.
Inaelezwa kuwa eneo hilo limekuwa na visa vingi vya wizi wa vijana wanaotumia pikipiki wanaokwapua simu na kutoweka jambo ambalo limefanya wananchi wa eneo hilo kuwa na hasira na vijana hao #EastAfricaTV.