Kitu gani kinakupa nguvu ya kutafuta pesa kwa bidii zote kwa umri uliokuwa nao?

proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,468
1,329
Ndugu zangu poleni kwa msiba wa mpendwa wetu JPM ambaye tumempumzisha leo kwenye nyumba yake ya milele. Nije moja kwa moja kwenye mada.

Hivi ni kitu gani kinakupa nguvu ya kutafuta pesa kwa bidii zote kwa umri uliokua nao? Mimi binafsi kinachonisukuma na kunipa nguvu ni kwamba pesa zinisaidie baada nitakapokuwa sina uwezo wa kufanya kazi.

Lakini pia ili niweze kusaidia wengine wasiojiweza. Binafsi najisikia vibaya ninapoona mtu akiteseka kisa tu hana pesa ya kujikimu. Vipi wewe nini kinakusukuma na kukupa nguvu ya kutafuta pesa kwa nguvu zote?
 
Nataka nimiliki hii ndinga.

0987.jpg
 
Ila kiukweli kama mtu mzima 30 mpaka 55 huu umri ukiwa huna pesa unadharaulika sana kwenye jamii, husikilizwi popote pale.

Nimeona hayo kwenye jamii yangu.

Hili ndilo linalonipa nguvu ya kutafuta pesa.

Hakuna kitu kibaya kama kutokusikilizwa.

"Huyu nae anaongea nini" nilisikia wakisema.
 
Nikiangalia mtaani kuna degree zimesota miaka 17 bila ajira na mpaka leo zinaapply, kila mwaka degree mpya zaidi ya laki moja zinaingia mtaani, nawaza watoto walio shule ya msingi na sekondari wakimaliza hizo degree miaka 10+ ijayo itakuwaje.

Ni lazima nijitese nitafute hela nyingi na kuwekeza miradi ya muda mfupi na mrefu ili waje kupata ajira kwa baba, uncle.. inaumiza kuona binti graduate anaomba kazi ya uhausigelo na graduate wa kiume anaomba kubeba zege na bado hapati
 
majuku
Ndugu zangu poleni kwa msiba wa mpendwa wetu JPM ambaye tumempumzishaleo kwenye nyumba yake ya milele. Nije moja kwa moja kwenye mada.

Hivi ni kitu gani kina kupa nguvu ya kutafuta pesa kwa bidii zote kwa umri uliokua nao? Mimi binafsi kinachonisukuma na kunipa nguvu ni kwamba pesa zinisaidie baada nitakapokuwa sina uwezo wa kufanya kazi.

Lakini pia ili niweze kusaidia wengine wasio jiweza. Binafsi najisia vibaya ninapoona mtu akiteseka kisa tu hana pesa ya kujikimu. Vipi wewe nini kinakusukuma na kukupa nguvu ya kutafuta pesa kwa nguvu zote?
1. Majukumu yangu kwa mama yangu mzazi na wadogo zangu wawili,
2. Kustawisha uchumi wangu mwenyewe ili niweze kununua na kumiliki kitu nitakochokihitaji kwa uewzo nitakoa kua nao
3. Pia mungu akibariki nina malengo ya kuwa na familia kwa hiyo ni jukumu la kupambana haswa ili waje kuishi maisha ya angalau na unafuu
4. Kuwekeza sana Mungu akiniwezesha kufika uzeeni basi nisiwe nategemea watoto niweze kupumzika na kuwa mzee
 
Ila kiukweli kama mtu mzima 30 mpaka 55 huu umri ukiwa huna pesa unadharaulika sana kwenye jamii, husikilizwi popote pale.

Nimeona hayo kwenye jamii yangu.

Hili ndilo linalonipa nguvu ya kutafuta pesa.

Hakuna kitu kibaya kama kutokusikilizwa.

"Huyu nae anaongea nini" nilisikia wakisema.
😅😅..mie nikachonifanyaga nitafute hela kwa hali na mali ni dharau za mzee wangu kwa mtoto wa kike basi! Yaan ukiwa huna hela hata mchana unaweza ambiwa panda gari tuna shida na ww...huulizwi je una muda..hushirikishwi jambo unaona kaka zako wanashirikishwa hadi unajiuliza mie nimezaliwaga hii family??..
Sasa hv mie nawacheki tu kaka zangu nasema nhiiiiiii
 
Nikiangalia mtaani kuna degree zimesota miaka 17 bila ajira na mpaka leo zinaapply, kila mwaka degree mpya zaidi ya laki moja zinaingia mtaani, nawaza watoto walio shule ya msingi na sekondari wakimaliza hizo degree miaka 10+ ijayo itakuwaje.
Ni lazima nijitese nitafute hela nyingi na kuwekeza miradi ya muda mfupi na mrefu ili waje kupata ajira kwa baba, uncle.. inaumiza kuona binti graduate anaomba kazi ya uhausigelo na graduate wakiume anaomba kubeba zege na bado hapati
Acha kuwaza kuajiriwa, jiajiri mwenyewe kupitia maarifa uliyoyapata hicho ndio kipimo cha kuwa umeelimika.
 
Jifunze kusoma alichoandika mtu ndio uandike Mkuu
Sina muda wa kufuatilia nina mambo mengi ya kufanya mkuu, siwezi kufuatilia upuuzi. Jambo la msingi ni kutoa mentality ya kuajiriwa kwa vijana badala yake wajiajiri ili tuone uwezo wao uliopo kichwani.
 
Back
Top Bottom