Kitimtim comedy imulikwe

Kitimtim comedy imulikwe

Sijui hata kama umeelewa mada inahusu nini,
Isome tena kwa utulivu
Pointi ni kwamba hata serikali huwa hawafungii kila kitu,

Mpaka unaona kipindi kwenye TV ni kwamba kimepitishwa na bodi ya filamu.

Hapo kazi ni kwako mtazamaji kuhakikisha nyumbani kwako vipindi hivyo inatazamwa na kundi sahihi
 
Vipindi vyote vya tivi tunavyoona na filamu zinazotoka za kitanzania huwa lazima zipate vibali vya bodi ya filamu
Aagh wapi..!! Filamu inayofuata process ndefu YES, Lakini kipindi kupata kibali cha bodi ya filamu kweli..!! I doubt
 
Siku hizi sanaa na kila kitu ni kuganga njaa tu! Ukitaka kufanya kitu hakikisha una idea ukiachilia mbali na kipaji...,Vilevile usiisahau nidhamu.

Ukifuatilia maigizo kadhaa ya miaka kenda yaliyokuwa yakiandaliwa na wizara na mabaraza mengine ya lugha na tamaduni basi ungegundua utofauti mkubwa sana na hawa walamba midomo na wapenda maisha mazuri wa sasa. (Watazame kina mzee Jangala, wale wa siri ya mtungi na wengineo)

Inaonesha wazi vijana hawataki kujishughulisha miili na akili kwenye mambo mengine yatakayowasaidia wao, vizazi vyao na taifa kwa ujumla... wanakimbilia kuonekana kwenye luninga wapate umaarufu halafu basi! Waulize "what's next sasa?!" Hana la kujibu anahunyahunya... baadae anasema "blaza au faza yule hater" Masenge sana haya matoto ya sasa hivi. Yapoyapo tu maskini!

NOTED! Ahsante kwa taarifa na uzalendo.
 
We acha tu kilichonikuta jana nilikua na Mama na dogo mmoja, nilinyanyuka nikaenda tu chumbani,

Na kuna ile scene askari wa kiume amemfunga pingu Pili halafu wanavutana vutana yaan askari wa kiume anamshika maungoni na kumpapasa juu mtuhumiwa wa kike ilikua kichefu chefu kuangalia, nikasema mbona wanadhalilisha jeshi la polisi? Sijakaa sawa ndio yule mshenzi anaomba ngono kwa mke wake na wengine kusema waingie ndani wamalizane!
Binafsi naona kimepoteza mvuto, siangalii kabisa siku hizi
 
Ukishaona kipindi mwanaume anaigiza kama Mwanamke ujue hicho kipindi na waigizaji wote hawajielewi, watazamaji, na hata hicho chombo kinaruhusu hayo madudu
 
Alafu ile eti inaitwa comedy,dah na kuna watu wanaangalia kabisa...upuuzi.
 
Hiko kipindi huwa sikupendi!!
Upuuzi mwingi sana
 
Hiki kipindi nilikua namashaka nacho tokea kitambo kidogo.... Kunawakati wife alikuwa akiipenda sana kitimtim na watoto nao nikaanza kuwasikia story za masantula sijui Huba,, nikasema ngoja niitafute siku nione na Mimi... mambo niliyoyaona ni aibu sana mbele ya familia. Palepale nikapiga mkwala mzito mama na watoto yaani wote walikuwa watoto kuwa Sitaki kuona ujinga huu wa Huba na kitimtim. Baadaye wakawa wanaangalia marudio nikiwa sipo. Nikaona isiwe shida nikang'oa DStv nikafunga dish la CANAL channel za ndani ni mwendo wa ZUKU..

HALF DICTATOR AND HALF DEMOCRAT
Chai
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom