Kitilya wa TRA kupelekwa TANESCO ?

dr.idris aliacha ma super dealer wa kuuza vocha za luku kama za simu,mhando kaingia kavuruga plan zote za kuikuza tanesco!pia hata ma bank yalikua na imani na idris rashid ndio maana walikuwa wanaikopesha
Mhando karahisisha zaidi unanunua Umeme kupitia simu. Idrissa ndio katuletea balaa lote hili anafanya tanesco ni gulio lakuuza matunda yake
 
Taarifa za hapa Dar mchana huu zinasema kuwa KITILYA wa TRA anaweza kupelekwa TRA kuokoa jahazi la TANESCO lisizame

swali; Je Kitilya anafaa au hafai kupelekwa Tanesco? sababu ni zipi?
Ptuuuuuu!!! Umbeya tu wa vijiwe vya kahawa na kashata.
 
Tanesco na makampuni mengi ya ummah yanahitaji wazungu tu kuiendesha....

nchi ya ajabu hiiii
tunaajiri wazungu kwa mpira
lakini hatutafuti wataalam wa kutoka nje kwa menejiment.....

Kabla ya kufikiria wataalam toka nje, kwanza punguza madaraka ya Raisi KIKATIVA la sivyo itafika siku wote watatakiwa kufanya RAISI atakavyo.
 
Fisadi wewe unataka kuamini kwamba Richmond ni kampuni tofauti na Dowans lakini ukweli ni kwamba Richmond ndiyo pia Dowans. Kutokana na kuwa na Serikali DHAIFU inayoongozwa na mafisadi, Mafisadi Rostam na Al Alawi hawakupata shida kuizuga Serikali eti mkataba wa Richmond umechukuliwa na kampuni mpya iitwayo Dowans. Richmond na Dowans ni Baba mmoja mama mmoja.

https://www.jamiiforums.com/habari-...-cag%92s-ruling-on-who-should-pay-dowans.html

However, it is not clear who is supposed to shoulder the burden, with Tanesco saying the government had the final say on the contract. Mr Utouh says in a letter to the Finance and Economic Affairs ministry that he had studied developments leading to the agreement, and concluded that the government should take responsibility for the compensation after interfering in Tanesco's contract mandate and obligations.

The CAG has also suggested that the government reviews Tanesco's debt portfolio and ease the burden on the public utility arising from contracts in which the State is involved."This will enable Tanesco to be evaluated on fair grounds and be held accountable for its own decisions," says the CAG.

Sisi hatufati unazi usio na mpango. Kesi za Kimataifa zinasema Dowans wewe unasema Richmond, sasa hapo fisadi ni nani? Mbona Symbion huitaji?

Richmond walishindwa kutimiza masharti na mkataba ukauzwa kwa Dowans ni kipi usichokielewa hapo? kwanini utake kulazimisha kuwa ni kitu kimoja?

Mitambo ile ile hata kesi haijaisha Symbion wameichukuwa na hakuna aliyesema hata "kwi" vipi leo Richmond iwe Dowans na Dowans isiwe Symbion?

Unachoshindwa kuelewaa ni kuwa hata Tanesco ni mali ya Serikali.

Sasa hiyo report ya CAG ndio nini, unajuwa kuisoma lakini? maana sasa hata uelewa wako unanitia mashaka. Huelewi kuwa Tanesco imefilisiwa (kama ada ya mashirika ya umma) kiasi hawawezi kujiwekea dhamana? mpaka wadhaminiwe? sasa ukidhaminiwa na Serikali unataka deni alipe nani?
 
Labda kwa hela yake ya mfukoni...maana pale ni shamba la bibi. Kila mtu anavunia pale and we all know!

Kwa pesa hizohizo inazokusanya Tanesco kwa wateja, zikipangiliwa zitaleta tija kubwa kabisa.

Wizi kwenye mashirika ya umma ni ada na hautokoma wala hayatoendelea mpaka yahamishiwe kwa watu binafsi. Kwa mtu binafsi ukiiba unapelekwa polisi kwenye mashirika haya unawekewa vikao, hiyo ndio tofauti iliyopo, kila mmoja anaogopa kumshitaki mwenzake.
 
Kwa pesa hizohizo inazokusanya Tanesco kwa wateja, zikipangiliwa zitaleta tija kubwa kabisa.

Wizi kwenye mashirika ya umma ni ada na hautokoma wala hayatoendelea mpaka yahamishiwe kwa watu binafsi.

Too many antagonistic forces...sijui atafanyaje
 
kinachotakiwa tanesco ni serikali ifanye yafuatayo

kuondoa kodi ya mafuta inayofikia 80bn kama alivyosema mhando
kudhamini tanesco kukopa kwenye mabenk, syndicate loan ili kuwalipa wadai wao ili kuepusha mgao

hata akienda kikwete pale kuwa MD haitasaidia, hatuhitaji kuuza sura bali kufanya kazi, na kufanya kazi ni pesa inatakiwa siyo barua na siasa

[MENTION]
Mwikimbi[/MENTION] acha kutuhadaa..................money is not everything.............................matatizo ya Tanesco ni ufisadi umekithiri sana hata upeleke trilioni 15 za bajeti ya serikali pale viwavi jeshi watazitafuna zote.........................wazo la kazi ya huduma kwenda kukopa kwenye mabenki ina harufu kali ya kifisadi....................muulize huyo fisadi Mhando marejesho yake yatakuwaje kwa viwango vya kutisha vya riba za mabenki tajwa kama siyo kumsukumia mynonge zigo tajwa?

Yawaje serikali iwe kiguu kwa njia kukopesha mabenki kwa madai ni "stimulus package" ya trilioni 1.7 khalafu serikali hiyohiyo irudi kwenye mabenki kukopa fedha zake yenyewe kama siyo upumbavu usio na mipaka...............................kwa kifupi ni kuwa mgao TZ wa umeme ni laana ya kudumu hadi pale tutakapomrudia Mwenyezi Mungu na kuchukia dhambi hasa ulafi wa pesa na madaraka..................
 
On a serious note, hilo shirika lenu Tanesco hata akipewa malaika atachemsha.

Shirika lina madeni kama nini mimi nilitegemea Mhando akatae kubebeshwa huo mzigo kama alivyofanya Dr Rashidi akaamua kukaa zake pembeni. Kwanza serikali ilete consultant aangalie upya shirika lote na kushauri na kufanya mabadiliko maana hilo shirika linaenda likifa, madeni lukuki ya umeme wa mafuta , makusanyo madogo. Kinatotakiwa ku restructure punguza wafanyakazi, vunja vunja vipande vipande (NMB - NBC style) serikali chukua mzigo lipa madeni ya nyuma japo kwa 50%. Weka CEO mpya aanze kazi.
 
Tanesco wanipe mimi niongoze japo umri bado hautoshi nitajikongoja nayo.:happy:

Haaahaaa! Usije ukaingia na nywele nyeusi baada ya wiki moja ukawa na mvi tupu. Inataka moyo kweli kweli kurekebisha mambo kwenye sehemu kazi inafanyika kwa mazoea
 
Haaahaaa! Usije ukaingia na nywele nyeusi baada ya wiki moja ukawa na mvi tupu. Inataka moyo kweli kweli kurekebisha mambo kwenye sehemu kazi inafanyika kwa mazoea

Ukiingia pale dawa yake wale wazee wazee ambao wanajifanya ni wa pale pale unawapunguza kidogo kidogo halafu unaanza kuingiza fresh graduates una wa train maana naona utendaji pia unasua sua kutokana na hawa ma ALWATAN!!
 
Pengine huu ni wakati muafaka wa kuligawa vipande vipande lile shirika na kama unavyosema, wale waliolizoea shirika waanze kuonyeshwa mlango wa kutokea
 
Pengine huu ni wakati muafaka wa kuligawa vipande vipande lile shirika na kama unavyosema, wale waliolizoea shirika waanze kuonyeshwa mlango wa kutokea

Exactly! tukishakata vipande vipande itakuwa rahisi hata sisi kujua ni wapi kuna matatizo maana kwa sasa shirika kubwa sana hata CEO sometimes naona inamuwia ngumu kuweka kila kitu kwenye finger tips.
 
Ugumu wake ni kuwa hilo ni shamba la bibi...wenye kuvunia hapo watakubali? Maana haiingi akilini kila siku serikali ina bail out na kila wakati wanaingia mikataba mingine mibovu. nani anayewawezesha watu kuendelea kufanya hivyo bila kuona aibu? Si tuwafunge wachache ili displine irudi kazini!
 
Ndahani,

Mimi nam support yule mwamba aliyesema wazungu warudi. Kwa kuanzia wanakatia umeme jeshi, Zanzibar , Ikulu nk

Unajua kwanini wana bail out? Serikali inachotoa unaweza kukuta kama 30% ya madeni wanayodaiwa na Tanesco. Maana unakuta serikali kuu kupitia wizara hazilipii umeme, Ikulu hailipii, Jeshi halilipi, Polisi hawalipi, Zanzibar ndio kabisa ukitaka kukata umeme watavunja muungano. Sasa serikali inachofanya hapa danganya toto hamna ku bail out ni kuipa uhai Tanesco angalau isife njaa wakati wao ndio wadaiwa sugu. Na wakitoa hizo fedha Tanesco inaona kama hisani kutok Treasury wakati wao wanaidai serikali pesa kibao. Muhimu Tanesco iwe ya mtu binafsi rudisha makaburu wacha wajilipe mshahara milioni 50 kwa mwezi lakini kazi ifanyike.

Kweli bongo Das'laam noma!
 
Kwani jamani hakuna wengine,hi re cycle kila leo,mbona kuna vijana wazuri tu,angalieni shirika la nyumba NHC lilivyobadilika,tunataka vijana kwenye mashirika sugu kama Tanesco ili watoe ujuzi wao wa dotcom,hawa watu wa makaratasi(Kitilya)umefika muda wao,TRA yenyewe imemshinda(kukusanya ushuru tu)sembuse iwe mambo ya kupambana na mgawo?
 
Ndahani,

Mimi nam support yule mwamba aliyesema wazungu warudi. Kwa kuanzia wanakatia umeme jeshi, Zanzibar , Ikulu nk

Unajua kwanini wana bail out? Serikali inachotoa unaweza kukuta kama 30% ya madeni wanayodaiwa na Tanesco. Maana unakuta serikali kuu kupitia wizara hazilipii umeme, Ikulu hailipii, Jeshi halilipi, Polisi hawalipi, Zanzibar ndio kabisa ukitaka kukata umeme watavunja muungano. Sasa serikali inachofanya hapa danganya toto hamna ku bail out ni kuipa uhai Tanesco angalau isife njaa wakati wao ndio wadaiwa sugu. Na wakitoa hizo fedha Tanesco inaona kama hisani kutok Treasury wakati wao wanaidai serikali pesa kibao. Muhimu Tanesco iwe ya mtu binafsi rudisha makaburu wacha wajilipe mshahara milioni 50 kwa mwezi lakini kazi ifanyike.

Kweli bongo Das'laam noma!

Maundumula,
Duuh mkuu umesema kweli. Kumbe tunajifilisi wenyewe halafu tunashangaa nani anatuloga! Anyway, kuna wakati bora tuwarudishe wazungu maana tunaweza kuwa na aibu kidogo kuliko hivi tunavyoendesha hilo shirika. Uchumi wetu utakuwaje kama kila siku tunawasha vibatari? na hata kama tutaongeza generation, with no displine on payment it is like wasting resources! Nimekupata mkuu and it is a challenge to us all.
 
Back
Top Bottom