Kitilya wa TRA kupelekwa TANESCO ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitilya wa TRA kupelekwa TANESCO ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wimbi la mbele, Jul 15, 2012.

 1. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Taarifa za hapa Dar mchana huu zinasema kuwa KITILYA wa TRA anaweza kupelekwa TRA kuokoa jahazi la TANESCO lisizame

  swali; Je Kitilya anafaa au hafai kupelekwa Tanesco? sababu ni zipi?
   
 2. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hivi kuna mahali wanatoa degree ya umbeya na kukurupuka?
   
 3. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,385
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  katafute bwana akuoe mbeya mkubwa wewe
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kinachotakiwa tanesco ni serikali ifanye yafuatayo

  kuondoa kodi ya mafuta inayofikia 80bn kama alivyosema mhando
  kudhamini tanesco kukopa kwenye mabenk, syndicate loan ili kuwalipa wadai wao ili kuepusha mgao

  hata akienda kikwete pale kuwa MD haitasaidia, hatuhitaji kuuza sura bali kufanya kazi, na kufanya kazi ni pesa inatakiwa siyo barua na siasa
   
 5. M

  MAFISADI KOMENI New Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeyapata wapi haya, haya tusubiri tuone
   
 6. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Kwanini kodi iondolewe? Unadhani Tanesco ndio wanaolipa kodi au ni wananchi?

  Serikali iwadhamini wakope walipe deni!, haya ni mawazo yako au ni mawazo ya bia!

  Ili twende sawa lazima turudi nyuma tuulizane kwanza hela zote inazokopa na zile ambazo serikali imetoa kwa miaka mingi, zimepotelea wapi? Kumbuka kila senti inayokopwa wananchi tumeilipa kupitia bili za umeme
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hafai, ni wale wale tu.

  TANESCO apewe S. S. Bakhresa kuiendesha.
   
 8. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ina maana huyo kitilya ndo mtu pekee aliyebaki Tanzania, anayeweza ku-manage haya mashirika? manake katika nchi hii kuna professional CEO kama masebu, mattaka, idrisaa rashid, hawa vijana wetu wanaosoma ni bure kabisa?
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,610
  Trophy Points: 280
  ...Yale yale!!! Kwa mafanikio yepi aliyoyapata TRA hadi apelekwe TANESCO? Si ndiye huyu aliyeshindwa kubuni mikakati ya kuongeza mapato ya Serikali na pia aliyeisababisha nchi kupoteza shilingi bilioni 500 pale kampuni ya kihindi ilipoamua "kuwekeza" nchini!?
   
 10. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mkuu tulishachelewa hayo madeni si ya tanesco bali yale mambo ya rich mond, agrreko, symbions, dowans ambayo serikali kupitia mafisadi wali-drag tanesco hapo ilipo. mkakati huo hapo juu ni wa kuinasua tanesco na taifa lisiingie gizani madhali wale waliolifikisha tanesco hapo mkuu wa magogoni hataki wachukuliwe hatua
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Tanesco na makampuni mengi ya ummah yanahitaji wazungu tu kuiendesha....

  nchi ya ajabu hiiii
  tunaajiri wazungu kwa mpira
  lakini hatutafuti wataalam wa kutoka nje kwa menejiment.....
   
 12. Raiamwematz

  Raiamwematz Senior Member

  #12
  Jul 15, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wapo wengi wazuri, wapewe tu ushirikiano!!!!!!!!!!!!!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,610
  Trophy Points: 280
  BOSS si walikuwepo wale makaburu wauza stationeries toka South Africa ambao waliingizwa na Mkapa kwa mtutu wa bunduki lakini kazi ikawashinda? Hata Wazungu pia hufanya madudu mengi tu.

  Mie naamini wako Wabongo ambao wanaweza kabisa kuiendesha TANESCO ila tu wawe huru kuachiwa kuiendesha bila kuingiliwa na Serikali (Wizara ya Nishati) Angalia matatizo mengi sasa hivvi ya TANESCO (Dowans, IPTL, mikataba ya Gas n.k.) Chanzo chake kikubwa ni Serikali (Nishati) Kwa mfano baada wataalamu wa TANESCO kuitathmini kampuni ya Richmond kabla haijaingia mkataba na Serikali wataalam wa TANESCO waliishauri Serikali kwamba Richmond haina uwezo wa kufua umeme hivyo isipewe mradi ule, lakini Serikali haikusikia ushauri wa wataalam wa TANESCO na yaliyotokea wote tunayajua.

   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  BAK please usipende sikiliza radio mbao
  kwanza hao makaburu ndio walioiambia serikali ubovu wa kampuni ya Richmond
  soma vizuri ripoti ya Mwakyembe...
  CEO kaburu ndio aliepinga zoezi zima la Richmond....

  halafu nikisema wazungu sina maana mzungu Rangi tu
  awe qualified na uzoefu unaohitajika

  wazungu ndio wana ubavu wa kukataa 'siasa' na presha za viongozi dhaifu wa nchi hiii....
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  naunga hoja mkuu maana tangu aichukue NMC hatujawahi kosa ngano,maji,mkate!hata sasa serikali inategemea uwanja wake chamazi,boat za kwenda zanzibar,ana viwanda msumbiji,malawi,rwanda,uganda
   
 16. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni mikataba mibovu ya POWER PURCHASE ambayo tunaingia na hawa wazungu bila kuwa na uilewa tunaingia mikataba ya aina gani!! Ndio maana tunajikuta TANESCO inadaiwa na hayo makampuni fedha ambazo yenyewe haikusanyi kutoka kwa wateja wake, hivyo kama gharama inazidi mapato lazima utakuwa na madeni [ deficit] . Tatizo liko kwenye hiyo mikataba na hivyo hivyo tutajikuta makampuni ni kuchimba GAS yatatuingiza mkenge kwa ujinga wa kuingia mikataba kichwa kichwa bila kuwatumia wazalendo WALIOTUKUKA kuihakiki vizuri.[sio wakina CHENGE na RASHID]!!
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,610
  Trophy Points: 280
  Hakuna chochote nilichoandika hapa ni cha kutoka redio mbao. Hizo ni info kutoka kwa close friends ndani ya TANESCO ambao wako kwenye position za juu. Waliofanya tathmini kama Richmond/Dowans wanastahili kupewa mkataba wa kufua umeme wakati ule nchi imegubikwa na giza nene na Wabongo wa kuzaliwa, CEO kaburu hakuwa na uwezo wowote wa kufanya tathmini ile kwa sababu alikuwa hajui chochote kuhusiana na ABC za ufuaji wa umeme.

  Wazungu makaburu walikuwa pale TANESCO lakini hawakuweza kukataa chochote kuhusu "siasa" na hivyo kusign mkataba wa kifisadi na kampuni ya wizi ya Mkapa "Kiwira" ya mkataba wa $326 millioni.   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kama makaburu waliletwa na Mkapa
  wasingeshindwa kukataa 'oder' ya Mkapa

  alikataaa siasa, CEO wa kwanza kabisa wakamuondoa...

  bottomline hao rafiki zako ndio hao hao kina Mhando in waiting.....

  Wazungu ndo solution ya kampuni za ummah za TZ..

  hawapendi kuchafuliwa.hawaogopi kuanika kitu
  na hawaogopi kufukuzwa...na hawawezi kuonewa sababu wanalindwa na sheria hadi za kimataifa...

  tutafute CEO wa kizungu from U S A...utaniambia....
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,610
  Trophy Points: 280
  Kutoka ripoti ya Mwakyembe

  Mheshimiwa Spika, kama nilivyodokeza awali, Kamati Teule ilishindwa kubaini moja kwa moja chanzo cha ujasiri wa kiburi ndani ya Wizara ya Nishati na Madini kiasi cha kupindisha maamuzi ya Baraza la Mawaziri bila wasiwasi wowote, kukaidi ushauri wa kitaalamu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma mara tatu mfululizo na kinyume na maagizo ya Baraza la Mawaziri yaliyotaka Sheria ya Ununuzi wa Umma izingatiwe, kukiuka sheria kwa makusudi kwa kuingilia mchakato wa zabuni wa taasisi nyingine ya ununuzi, kuvipuuza vyombo vya ndani vya maamuzi vya TANESCO (Bodi ya Wakurugenzi, Bodi ya Zabuni n.k), kuilazimisha Bodi ya Menejimenti ya TANESCO kuridhia maamuzi yaliyofanywa na Wizara ya kuibeba Richmond Development Company LLC kinyume cha sheria na taratibu, n.k. Aidha Kamati Teule ilishangazwa na Ofisi ya Waziri Mkuu iliyokuwa ikifuatilia kwa karibu mchakato huo, kushindwa kukemea ukaidi huo wa Wizara ya Nishati na Madini.
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  kuendesha Tanesco sio lazima ujue taaluma ya umeme
  MENEJIMENTI peke yake ni TAALUMA..
  ndio maana Idrisa Rashid alikuwa better CEO kuliko Engineer Mhando

  na ndo maana ma CEO mfano wa TBL hawajui 'taaluma ya kutengeneza beer'
  lakini wanaweza..
   
Loading...