Precise Pangolin
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 12,998
- 6,659
Wewe si unataka Mzee wa mapishi bakheresa ili ule futari za bure kwi! Kwi! Kwi! Kwi!basi atapewa reginald mengi ufurahi,ingawa katapeli pesa zetu za NICOL
Wewe si unataka Mzee wa mapishi bakheresa ili ule futari za bure kwi! Kwi! Kwi! Kwi!basi atapewa reginald mengi ufurahi,ingawa katapeli pesa zetu za NICOL
dr.idris aliacha ma super dealer wa kuuza vocha za luku kama za simu,mhando kaingia kavuruga plan zote za kuikuza tanesco!pia hata ma bank yalikua na imani na idris rashid ndio maana walikuwa wanaikopeshaAendelee mhando
Mkataba wowote ule ulioingiwa kwa njia za udanganyifu na kisha wahusika kushindwa kutimiza masharti ya mkataba ule ya kufua umeme ni mkataba batili. Kama Serikali ingekuwa makini katika kuipanga kesi yake basi TANESCO ingeshinda katika kesi ile lakini wahusika wakuu toka Serikalini walikuwa wameshahesabu mgao wao toka kwa fisadi Rostam Azizi hivyo hawakuhakikisha umakini katika utetezi wa kesi yao dhidi Fisadi Rostam na mwenzie Al Alawi.
Kama Serikali iliweza kupinga hukumu ya kesi yake dhidi ya Valambhia na kukataa kulipa mabilini ya pesa kwa kampuni hiyo. Basi pia Serikali hii DHAIFU ikiwa makini inaweza kabisa kufanya hivyo. Kumbuka pesa hizo zilitakiwa kulipwa tangu December 2010 lakini kutokana na kupinga kwa Watanzania pamoja na hii Serikali DHAIFU kuridhia kulipa pesa hizo hazijalipwa na kama tukiweza kusimamia zislipwe hadi 2015 na CHADEMA kuchukua nchi basi Mafisadi ndani ya Serikali waliokuwa wanaumezea mate mgao wao haramu toka kwa mafisadi Rostam na Al Alawi hawataona hata senti tano toka hazina.
Wewe wacha pumba, wewe unaijuwa mikataba kuliko majaji wa mikataba ya kibiashara? Hakuna cha chadema wala nini, Nyerere mwenyewe muulize alifanywa nini na Tiny wa LONRHO. Mpaka kafa hana hamu nae alipojidai kutaifisha biashara zilizo na mikataba, alikiona cha mtema kuni.
Hakuna pumba hapo magamba, weye magamba unaona Pumba ili kutetea magamba wenzio kama Serikali ilisharidhia kulipa hiyo pesa tangu 2010 sasa inakuwaje tena wakabadili maamuzi yake ya kulipa pesa na kuanza kujikanyagakanyaga? Kama zingekuwa ni pumba basi Serikali hii DHAIFU ingetamka kwamba tunakubaliana na hukumu ya mahakama ya kibiashara hivyo tutalipa pesa hizo. Walioingia mkataba na Richmond ni Serikali na siyo TANESCO lakini Serikali hii DHAIFU baada ya kupindisha taratibu za kuingia mkataba sasa inaisakizia TANESCO ndio wabebe jukumu la kulipa. Soma hiyo Article hapo juu uone utata kuhusu kizungumkuti cha mkataba huu batili.
TANESCO kuwalipa Dowans giza nene
Mwandishi Wetu
Toleo la 168
12 Jan 2011
RAIA MWEMA
- Uharaka wa Ngeleja, Werema watia shaka
WAKATI Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werama wakiwa tayari kutumia kodi za wananchi kuilipa kampuni ya Dowans, kasi ya kutaka kampuni hiyo kulipwa inatia shaka, Raia Mwema, imebaini.
Shaka hiyo ikiachwa, utata umeendelea kuibuka kuhusu nani hasa atakayelipwa fedha hizo kutokana na mvutano uliopo kuhusiana na wamiliki halisi wa Dowans na mtangulizi wake, Richmond Development LLC.
Ngeleja na Werema wamekuwa na haraka ya kutaka malipo yafanyike huku kukiwa na baadhi ya kesi zilizowahi kutolewa hukumu na Mahakama ya Tanzania ili zifidiwe lakini zikagonga mwamba kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Moja ya kesi hizo ni ile iliyokuwa ikimhusu mfanyabiashara Devram Valambhia, aliyetakiwa kulipwa na Serikali shilingi bilioni 60 katika kesi ambayo iliunguruma kwa muda mrefu huku Serikali ikishindwa kila mara.
Msingi wa kesi hiyo ni mfanyabiashara Valambhia kuidai Serikali dola 55 milioni kutokana na kuiuzia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, magari kutoka Chekoslovakia.
Serikali ilikuwa ikihangaika na kesi hiyo kwa kukata rufaa na kushindwa kila mara huku ikitumia mawakili wa kukodi wanaoelezwa kuwa nao waligharimu shilingi bilioni nane.
Kutokana na Serikali kuhangaika kutokutaka kumlipa mfanyabiashara huyo ililazimika kukata rufaa nyingi na kutumia fedha za kukodi mawakili kiasi cha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutilia shaka mwenendo huo.
Wasiwasi wa CAG ulijikita katika malipo makubwa waliyokuwa wakilipwa mawakili waliokuwa wakisimamia kesi hiyo kwa niaba ya Serikali.
Katika harakati za kuzuia malipo hayo Serikali iliwahi kuielekeza Benki Kuu kutokutoa fedha kwa ajili ya kumlipa Valambhia na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) alikiri kwa baadhi ya vyombo vya habari kuhusu kuelekezwa, hasa baada ya kuwapo ushauri kuwa malipo hayo yafanyike nje ya Mahakama.
Wasiwasi huo unajitokeza katika wakati ambao Serikali imetaja wamiliki wa kampuni ya Dowans Tanzania itakayolipwa mabilioni hayo kama hukumu ya Mahakama ya Kibiashara ya Usuluhishi inavyoelekeza. Mahakama hiyo imetaka Dowans Tanzanaia Ltd ilipwe Sh bilioni 94.
Hata hivyo, rekodi za baadhi ya wamiliki hao ambao wote ni raia wa kigeni hazipatikani moja kwa moja kwenye mtandao wa kompyuta. Wakati Hon Sung Woo anayetajwa kuwa mmiliki wa Dowans kutoka Singapore na Guy Arthur Picard wa Canada, taarifa zao haziko wazi kwenye mtandao.
Tayari mawaziri William Ngeleja wa Nishati na Madini, na Samuel Sitta wa Uhusiano wa Afrika Mashariki ambaye pia alikuwa Spika wa Bunge lililopita, wametofautiana kuhusu kufanya malipo hayo.
Waziri Sitta anaamini kuwa kabla ya waziri kutangaza rasmi kutaka kuilipa kampuni hiyo, uamuzi huo ulipaswa kujadiliwa na Baraza la Mawaziri kwanza lakini pia anaamini kuna mianya ya kisheria kupinga kufanywa kwa malipo hayo.
Kuhusu hukumu hiyo ya Novemba 15 mwaka jana, Ngeleja aliweka bayana kuridhika na uamuzi huo kuwa mkataba wa TANESCO na Dowans ulivunjwa kabla ya wakati na hivyo kustahili kulipwa.
Kwa hatua hiyo, Dowans italipwa dola milioni 65.8 za Marekani sawa na shilingi bilioni 94 na si shilingi bilioni 185 ambazo zimekuwa zikiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Hata hivyo, alisema fedha hizo zitalipwa mara Dowans itakaposajili hukumu hiyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Katika hati yake ya mashitaka, Dowans iliomba kulipwa dola milioni 149 na TANESCO kwa kuvunja mkataba wa kuzalisha megawati 100 za umeme, lakini Mahakama ya usuluhishi ilihukumu ilipwe milioni 65.8.
Wakati hayo yakiendelea, Dowans na Richmond wameshitakiana nchini Marekani baada ya kutofautiana kuhusiana na biashara waliyorithishana na TANESCO.
Mkataba wa Dowans umeusoma, au tukuwekee hapa, ule ulikuwa ni wa Serikali? wacha kuzuwa ulikuwa ni TANESCO.
Hiyo mitambo iko wapi sasa? wacha kuupoteza umma.
Halafu eti Serikali wameisukumia TANESCO wakati hao Dowans ndio walishtaki, waende wakashtaki mtu wasie na mkataba nae si kesi ingetupiliwa mbali?
Soma huu hapa:
ICC Case No. 15947/VR: Dowans (Claimant) and TANESCO (Respondent)
Hakuna cha kuchemsha, mashirika yote ya umma yaliyoshindwa kuendeshwa kifaida na Serikali watu binafsi wameyachukuwa bila ruzuku ya Serikali na wanafanya vizuri tu. Mfano mzuri wa shirika kubwa ni NBC. Ilikuwa ni hasara tupu, sasa tunaona wanalipa kodi nyingi tu. TBL?
Mkuu hayo mashirika unayotolea mfano yanajipangia kila kitu based on market forces, tanesco siyo hivyo, bei zao wanapangiwa na ewura, kiukweli bei ya umeme tunayolipa ni below operating costs, ukitaka uamini ninachokwambia linganisha bei zetu za umeme na za nchi nyingine hata zile ambazo tunalingana nazo kiuchumi. Kifupi suala la tanesco usichukulie kirahisi rahisi hivyo!
Acha uzushi weye fisadi Zomba alias Faiza Foxy weka ushahidi hapa jamvini pale nilipozuwa kama nilikuwa TANESCO.
Mwananchi yeyote yule ambaye anatetea mafisadi na kukandamiza maslahi ya nchi yake hata pale ambapo kuna ushahidi wa kutosha (mkataba wa Richmond/Dowans ulikuwa ni batili utapiga kelele mpaka povu zikutoke, lakini ukweli ndio huo)unaonyesha kwamba nchi yake inadhulumiwa ni wa kuogopwa kama UKOMA....Source BAK.
By BAK
Hakuna pumba hapo magamba, weye magamba unaona Pumba ili kutetea magamba wenzio kama Serikali ilisharidhia kulipa hiyo pesa tangu 2010 sasa inakuwaje tena wakabadili maamuzi yake ya kulipa pesa na kuanza kujikanyagakanyaga? Kama zingekuwa ni pumba basi Serikali hii DHAIFU ingetamka kwamba tunakubaliana na hukumu ya mahakama ya kibiashara hivyo tutalipa pesa hizo. Walioingia mkataba na Richmond ni Serikali na siyo TANESCO lakini Serikali hii DHAIFU baada ya kupindisha taratibu za kuingia mkataba sasa inaisakizia TANESCO ndio wabebe jukumu la kulipa. Soma hiyo Article hapo juu uone utata kuhusu kizungumkuti cha mkataba huu batili.
Below operating cost si kwa kuwa walishindwa kuwekeza on time. Unafikiri umeme wa kukodisha majenereta utaufuwa kama wa maji au wa nuclear? Steigler Gorge ilipendekezwa toka wakati wa Nyerere na gharama zilikuwa ni kama 10% tu ya gharama za leo. Wapi?
Sasa hii Tanesco nayo ipo njiani, sheria za ushindani wa ufuaji umeme Kikwete kisha zi saini, zinafanyiwa maboresho tu na tutaanza kuona likibaki kama ilivyo TTCL wapo kama hawapo.
Hiki hapa nini?
Soma hiyo halafu useme kama sio kupindisha maneno ni nini? Serikali ipi au TANESCO ipi ilikuwa na mkataba na Richmond ulioamuliwa mahakama ya kibiashara? nimekuwekea juu hapo mpaka kesi namba na nani mdai na nani mdaiwa bado tu unakataa? Ni DOWANS walioshtaki si Richmond wacha kuendelea kubisha ujinga. Nakuwekea tena hapa chini:
Soma huu hapa:
ICC Case No. 15947/VR: Dowans (Claimant) and TANESCO (Respondent)
Hiki hapa nini?
Soma hiyo halafu useme kama sio kupindisha maneno ni nini? Serikali ipi au TANESCO ipi ilikuwa na mkataba na Richmond ulioamuliwa mahakama ya kibiashara? nimekuwekea juu hapo mpaka kesi namba na nani mdai na nani mdaiwa bado tu unakataa? Ni DOWANS walioshtaki si Richmond wacha kuendelea kubisha ujinga. Nakuwekea tena hapa chini:
Soma huu hapa:
ICC Case No. 15947/VR: Dowans (Claimant) and TANESCO (Respondent)