Kitilya asota rumande miaka 2


ndege JOHN

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2016
Messages
5,295
Likes
8,154
Points
280
ndege JOHN

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2016
5,295 8,154 280
IKIWA ni zaidi ya miaka miwili tangu aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kufi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wameendelea kusota rumande kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Aprili Mosi 2016, Kitilya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni inayoshughulikia Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (Egma) pamoja na maofisa wawili wa Benki ya Stanbic akiwemo aliyekuwa Miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Sioi Solomon ndio ilikuwa mara ya kwanza kufikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka nane ikiwemo ya utakatishaji fedha.

Hata hivyo, washitakiwa hao wanaendelea kusota rumande kwa sababu mashitaka ya utakatishaji fedha yanayowakabili hayana dhamana kisheria. Jana upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanawasiliana na wachunguzi ili wajue upelelezi umefikia wapi.

Mwita aliieleza mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika kwani wanaendelea kuwasiliana na wachunguzi. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi huyo hadi Novemba 16, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika ama la.

Washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha. Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Chartered Uingereza.

Wanadaiwa kuwa Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia dola za Marekani milioni sita, wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.

Washitakiwa hao wanadaiwa kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka dola za Marekani milioni sita katika akaunti tofauti za benki. Kati ya Machi 2013 na Septemba 2015, wanadaiwa kuwa waliweka fedha hizo katika akaunti mbalimbali zilizomilikiwa na kampuni ya Egma na kwamba walipaswa kufahamu kuwa fedha hizo ni mazao ya uhalifu wa kughushi.
 
K

kakolaki

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2017
Messages
449
Likes
361
Points
80
K

kakolaki

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2017
449 361 80
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
61,283
Likes
29,171
Points
280
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
61,283 29,171 280
Magufuli ni jembe anataka kuset presidency kwamba bila kujali wewe ni nani au ulikua nani unaweza banwa na sheria, that is very good kwa nchi inapunguza gap la wasiogusika na maskini

Sent using Jamii Forums mobile app
presidency = precedence / precedent
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
32,930
Likes
20,382
Points
280
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
32,930 20,382 280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,341
Likes
1,595
Points
280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,341 1,595 280
kweli hela watu hawatosheki.. kwa vyeo na madili aliyopiga kitilya enzi za tra bado anakua mwizi tu hadi uzeeni
Kikwete amewaingiza chaka wote wakina Kitilya , Mattaka na wengine wengi wakati yeye muhusika mkuu anakula BATA huko Msoga!!!
 

Forum statistics

Threads 1,250,115
Members 481,224
Posts 29,721,199