Kitilya asota rumande miaka 2


ndege JOHN

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2016
Messages
5,294
Likes
8,154
Points
280
ndege JOHN

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2016
5,294 8,154 280
IKIWA ni zaidi ya miaka miwili tangu aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kufi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wameendelea kusota rumande kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Aprili Mosi 2016, Kitilya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni inayoshughulikia Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (Egma) pamoja na maofisa wawili wa Benki ya Stanbic akiwemo aliyekuwa Miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Sioi Solomon ndio ilikuwa mara ya kwanza kufikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka nane ikiwemo ya utakatishaji fedha.

Hata hivyo, washitakiwa hao wanaendelea kusota rumande kwa sababu mashitaka ya utakatishaji fedha yanayowakabili hayana dhamana kisheria. Jana upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanawasiliana na wachunguzi ili wajue upelelezi umefikia wapi.

Mwita aliieleza mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika kwani wanaendelea kuwasiliana na wachunguzi. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi huyo hadi Novemba 16, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika ama la.

Washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha. Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Chartered Uingereza.

Wanadaiwa kuwa Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia dola za Marekani milioni sita, wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.

Washitakiwa hao wanadaiwa kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka dola za Marekani milioni sita katika akaunti tofauti za benki. Kati ya Machi 2013 na Septemba 2015, wanadaiwa kuwa waliweka fedha hizo katika akaunti mbalimbali zilizomilikiwa na kampuni ya Egma na kwamba walipaswa kufahamu kuwa fedha hizo ni mazao ya uhalifu wa kughushi.
 
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
61,277
Likes
29,157
Points
280
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
61,277 29,157 280
Kikwete amewaingiza chaka wote wakina Kitilya , Mattaka na wengine wengi wakati yeye muhusika mkuu anakula BATA huko Msoga!!!
Shida adabu yako.

Kikwete ndiye Rais pekee aliyefunga mawaziri kwa ufisadi ndiye Rais pekee aliyemtosa waziri mkuu kwa ufisadi. Na ndiye Mwenyekiti aliyeacha roadmap (ilani) inayofatwa sasa hivi.

Koma.
 
gwijimimi

gwijimimi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2011
Messages
6,871
Likes
1,654
Points
280
gwijimimi

gwijimimi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2011
6,871 1,654 280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,334
Likes
1,591
Points
280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,334 1,591 280
Shida adabu yako.

Kikwete ndiye Rais pekee aliyefunga mawaziri kwa ufisadi ndiye Rais pekee aliyemtosa waziri mkuu kwa ufisadi. Na ndiye Mwenyekiti aliyeacha roadmap (ilani) inayofatwa sasa hivi.

Koma
Nilijua utatoka shimoni kwako tu uje umtetee mfadhili wako!! Mbona husemi ufisadi wa HOME SHOPPING CENTRE na jinsi alivyofadhili hawa jamaa kupitisha makontena bandarini bila kulipa kodi; jinsi alivyowalinda wauza madawa ya kulevya mpaka ameingia Magufuli ndio wakapelekwa Marekani; Unajua yeye ndiye aliyemlazimisha Mattaka kuingia mkataba wa kukodisha ile ndege ya AIRBUS kutoka kwa mlebanoni iliyolimbikiza deni la mabilioni kwa serikali!! Halafu unasema alikuwa anapiga vita ufisadi? Unajua gharama ya Barabara ya Bagamoyo mpaka Msata umegharimu kiasi gani na mjenzi akiwa swahiba wake Subash Patel?

Unajua kısa cha yeye kusabotage kukamilika kwa rasimu ya katiba ya Warioba? Aliogopa kama ile rasimu ingepitswa na katiba kukubaliwa yeye hivi leo yangempata yaliyompata Jacob Zuma kule South Afrika!!!

Sasa wewe ndio ukome ukomae.
 
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
61,277
Likes
29,157
Points
280
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
61,277 29,157 280
Nilijua utatoka shimoni kwako tu uje umtetee mfadhili wako!! Mbona husemi ufisadi wa HOME SHOPPING CENTRE na jinsi alivyofadhili hawa jamaa kupitisha makontena bandarini bila kulipa kodi; jinsi alivyowalinda wauza madawa ya kulevya mpaka ameingia Magufuli ndio wakapelekwa Marekani; Unajua yeye ndiye aliyemlazimisha Mattaka kuingia mkataba wa kukodisha ile ndege ya AIRBUS kutoka kwa mlebanoni iliyolimbikiza deni la mabilioni kwa serikali!! Halafu unasema alikuwa anapiga vita ufisadi? Unajua gharama ya Barabara ya Bagamoyo mpaka Msata umegharimu kiasi gani na mjenzi akiwa swahiba wake Subash Patel?

Unajua kısa cha yeye kusabotage kukamilika kwa radium ya katibi ya Warioba? Aliogopa kama ile rasimu ingepitswa na katibi kukbaliwa yeye çivi leo yangempata yaliyompata Jacob Zuma kule South Afrika!!!

Sasa wewe ndio ukome ukomae.
Kasome uzi wao upo humu na michango yangu utakuta.

Huwa sikisii.
 
Tindikali

Tindikali

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2010
Messages
1,064
Likes
961
Points
280
Tindikali

Tindikali

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2010
1,064 961 280
Magufuli ni jembe anataka kuset presidency kwamba bila kujali wewe ni nani au ulikua nani unaweza banwa na sheria, that is very good kwa nchi inapunguza gap la wasiogusika na maskini
Hakuna aliyehukumiwa kifungo awamu ya Magufuli.

Hizi ni hujuma kwa haki za raia kufunga watu bila kesi.

Hakuna “ujembe” wowote hapo bali uonevu na hujuma.
 
sodoliki

sodoliki

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,877
Likes
1,030
Points
280
sodoliki

sodoliki

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,877 1,030 280
Magufuli ni jembe anataka kuset presidency kwamba bila kujali wewe ni nani au ulikua nani unaweza banwa na sheria, that is very good kwa nchi inapunguza gap la wasiogusika na maskini

Sent using Jamii Forums mobile app
Precedence gani kesi inatakiwa iishe siku 90, huu ni uonevu tuu, justice deleyed is justice denied
 
Tindikali

Tindikali

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2010
Messages
1,064
Likes
961
Points
280
Tindikali

Tindikali

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2010
1,064 961 280
100% true, wakilipa ransom money wanatoka
Yes, I agree... na hiyo ransom money ya milioni 200 ninaamini wanayo, ila ku plead guilty inakuwa ngumu kwa mtu mwenye principle na anaeamini amefanyiwa hujuma kwa kiki za kisiasa. Mzee Kitilya na kijana mkwe wa Lowassa wanaishi sehemu maalum pale Keko, ya kulipia na kujilisha, ambayo ipo available kwa yeyote mwenye kujiweza. Gharama za kujitunza pale kwa miaka miwili zishafika milioni 200, trust me, hiyo hela wanayo, there is no way Rugemalila hana 200mil za madafu za kumlipa jiwe ili atolewe.

Hawataki kulipa ransom money as a matter of principle. My gut feeling is wanakataa kuhalalisha hujuma za wanasiasa, wameonewa sana hawa wazee, Kitilya, kijana wa Lowassa, Mzee Noni, Lugemarira, binti wa Sinare, Habinger Singh, na wengine weeengi ambao hawana majina makubwa, so called wanyonge na masikini, waliofungwa miaka nenda rudi bila mashitaka.
 

Forum statistics

Threads 1,250,078
Members 481,222
Posts 29,720,091