Kitillya na wenzake wataka upelelezi uharakishwe

Kitillya na wenzake wataka upelelezi uharakishwe

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
UPANDE wa utetezi katika kesi inayowakabili Harry Kitillya, aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shose Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, mwanasheria wa benki hiyo, umeutaka upande wa Jamhuri kuwahisha upelelezi.

Alex Mgongolwa, wakili wa watuhumiwa hao. Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Respecious Mkeha amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo una muda wa miezi sita bila kukamilika.

Awali, wakili wa serikali Kishenyi Mutalemwa alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kwamba Mkurugenzi wa Mashtaka ameeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) inaendelea na upelelezi.

Hakimu Mkeha ameitaka Jamhuri kukamilisha Upelelezi wa shauri hilo kwa wakati huku akitangaza kuahirisha kesi hiyo mpaka terehe 4 Novomba, Mwaka huu.

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo kwa kosa la kuhujumu uchumi wakidaiwa kughushi nyaraka na kufanikisha uhalifu huo kati Agosti 2012 na Machi 2013 jijini Dar es Salaam.

Kosa la pili, linadaiwa kufanywa na Sinare, tarehe 2 Agosti mwaka 2012 kwa kughushi hati ya mkopo wa Dola za Marekani 550 milioni katika Benki ya Stanbic ya Tanzania na Benki ya Standard ya Uingereza akiiombea fedha Serikali ya Tanzania.

Sinare anatuhumiwa kwa kosa la tatu alilotenda tarehe 13 Agosti 2012, la kupeleka hati ya kughushi kwenye Wizara ya Fedha iliyoonesha kuwa Serikali ya Tanzania itapewa mkopo wa Dola za Marekani 550 milioni kutoka Benki ya Stanbic ya Tanzania na Standard ya Uingereza.

Washitakiwa hao pia wote wanakabiliwa na kosa la kutengeneza mkataba bandia tarehe 5 Novemba, mwaka 2012 jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Benki ya Stanbic kupitia Kampuni ya Enterprise Growth Market Advisor (EGM).

Shitaka lingine linalowakabili watuhumiwa wote ni utakatishaji fedha wanalodaiwa kulitenda kati ya mwezi Machi 2013 na Septemba 2015.
 
Sasa edo si amuone mkuu ili huduma za mtoto zipatikane? Maana nimeona leo wamebeba miili ya jela kabisa.

Ila tujifunze kupiga dili si dili tena.
 
Uchunguzi uharakishwe ili Iweje? Wao wasubirii jamhuri inaendelea na kazi yake ya uchunguzi kama kanuni zinavyotaka. Kwani hawa wanyonge wasio kuwa na wanasheria mbona wao husubiri uchunguzi ukamilike.

Wasubiri.
 
Dhamana ni haki ya msingi ya raia katika nchi za watu wenye upeo wa kujitungia katiba zinazowajali na kuwalinda wakati wa matatizo kama ya shutuma. Sio hapa Afrika
 
Hivi kwa nini wabongo wana roho mbaya sana kwa matajiri? Naona wengi mnafurahia kwamba vigogo wapo ndani bila kujali kama wana hatia au la.

Matajiri au wezi ,muulize Tundu lisu amesema huko sio kuzuri kabisa
 
Dhamana ni haki ya msingi ya raia katika nchi za watu wenye upeo wa kujitungia katiba zinazowajali na kuwalinda wakati wa matatizo kama ya shutuma. Sio hapa Afrika

Duniani kote, sio kila kosa lina dhamana kisheria.

Kuna baadhi ya makosa hayana dhamana kabisa, mtuhumiwa atakaa mahabusu mpaka pale hukumu ya kesi itaposomwa.

Mfano kwa hapa Tanzania, makosa yafuatayo HAYANA dhamana:

murder, drugs trafficking, human trafficking, Armed robbery, Money laundry, Treason, kukamatwa na nyara za serikali, etc.

N.B: Hata kwa makosa yenye dhamana kisheria (bailable offences), still kuna some circumstances Mahakama imeruhusiwa kisheria kunyima dhamana. Circumstances hizo ni kama vile:
-Seriousness of the offence;
-Safety of the offender, kwamba endapo mtuhumiwa akipewa dhamana inawezekana akauawa au akadhurika huko uraiani;
-Possibility for the offender to interfere with investigation;
-Past criminal record of the offender whereas s/he had ever jumped bail in another past criminal case.

-Kaveli-
 
Uchunguzi uharakishwe ili Iweje? Wao wasubirii jamhuri inaendelea na kazi yake ya uchunguzi kama kanuni zinavyotaka. Kwani hawa wanyonge wasio kuwa na wanasheria mbona wao husubiri uchunguzi ukamilike.

Wasubiri.
Kuchelewesha kesi sio sawa hasa mtuhumiwa akiwa ndani.... miezi sita upelelezi unaendelea, kulikuwa na sababu gani ya kuwawahisha kuwapeleka mahakamani kama upelelezi bado?.. kumbuka hamna anae jua ukweli kihalisi mpaka watakapo hukumiwa.... kuchelewesha upelelezi wakati wako ndani means wameisha hukumiwa.....
 
Duniani kote, sio kila kosa lina dhamana kisheria.

Kuna baadhi ya makosa hayana dhamana kabisa, mtuhumiwa atakaa mahabusu mpaka pale hukumu ya kesi itaposomwa
Mfano kwa hapa Tanzania, makosa yafuatayo
HAYANA dhamana:

murder, drugs trafficking, human trafficking, Armed robbery, Money laundry, Treason, kukamatwa na nyara za serikali, etc.

N.B: Hata kwa makosa yenye dhamana kisheria (bailable offences), still kuna some circumstances Mahakama imeruhusiwa kisheria kunyima dhamana. Circumstances hizo ni kama vile:
-Seriousness of the offence;
-Safety of the offender, kwamba endapo mtuhumiwa akipewa dhamana inawezekana akauawa au akadhurika huko uraiani;
-Possibility for the offender to interfere with investigation;
-Past criminal record of the offender whereas s/he had ever jumped bail in another past criminal case.

-Kaveli-
Hayo yote Sawa.... ila kuna haja gani ya kuwakimbizia mahakamani washitakiwa ukijua upelelezi haujakamilika? Miezi sita kweli una faili la watu mezani kwako unajua watu hawa wako mahabusu kwa sababu ya wewe kuto kamikisha
upelelezi? Na unaenda kusali kweli? Yes kama makosa hayana dhamana basi kesi ianze...
 
Hata Mimi najiuliza hilo Hilo. Kama mnajua upelelezi haujakamilika, ni kitu gani kinachomsukuma huyu dpp kuwafungulia watu mashtaka

Pili taasisi ya dpp inashindwa vipi kukamilisha upelelezi wa watuumiwa kwa miezi 6 tokea wafungue kesi?
 
Hivi kwa nini wabongo wana roho mbaya sana kwa matajiri? Naona wengi mnafurahia kwamba vigogo wapo ndani bila kujali kama wana hatia au la.
waajiriwa wanakuwaje matajiri ? ,.................vigogo !
 
Hata mie nashangaa.
Kwanza serikali inafunguaje mashtaka kwanza kisha eti ndio upelelezi unafuata na miezi sita haujakamilika?
Kuna neno hapo tutasikia tuu
Aisee, kwahyo ulitaka wawaache kwanza? Daah mahaba yamewapofusha mnatetea hadi wezi
 
Hayo yote Sawa.... ila kuna haja gani ya kuwakimbizia mahakamani washitakiwa ukijua upelelezi haujakamilika? Miezi sita kweli una faili la watu mezani kwako unajua watu hawa wako mahabusu kwa sababu ya wewe kuto kamikisha
upelelezi? Na unaenda kusali kweli? Yes kama makosa hayana dhamana basi kesi ianze...
Upelelezi ni kwenda tandale kukamata vibaka pale eeh?
 
Back
Top Bottom