MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 20,709
- 42,796
Na kimsingi aliwapa siku saba wadau watoe sababu kwa nini mfumo wa GPA uliwekwa na sababu za kitaalam za mabadiliko hayo wadau wote walishindwa kutoa sababu na hivyo akarudisha kilicho halali na kuondoa haramu yao!!Tafiti ya nini kama ile iliyotenguliwa haikuja na tafiti mujarabu si unarudi kule ulikokuwa mpaka ije tafiti nyingine ya kubadilisha hii ya DIVISHENI.
Waliulizwa siku ile mbele ya press na umma wakawa wanajiumauma tu.
Tumemwelewa ndalichako zaidi kwa kuwa ameturudisha kwenye ukweli maana hapo ndipo tutaona kwa uwazi ubovu wa elimu yetu na kuanza kujipanga upya kutoka kwenye kiini cha tatizo maana tatizo si upimaji, Elimu kwa hakika imeoza na mfumo wa GPA uliochakachuliwa kwa sababu za kisiasa ili kufikia malengo ya MATOKEO MAKUBWA SASA ulitumika ili walau kuficha uozo huo kwa muda maana athari zake za uozo zimeonekana vyuoni na mtaani kwa hao waliofaulu kutokuwa na uwezo hata wa kuandika insha ya kiingereza walau kujitambulisha au hata kushindwa kujaza fomu za udahili wa chuo. Huko mtaani ndio hawana la ziada zaidi ya kuwa madereva wa bodaboda na wa dada kujisalimisha kwenye kuolewa, kukaanga vitumbua na ile biashara isiyo na utu!Kwa msiokua na fikra za mbali ameshindwa kumwelewa Prof Mkumbo! Kinachozungumzwa hapa ni hakuna consistance! Kila awamu ni kubadili mfumo tu, kila waziri na lake! Kilichotakiwa hapa ni kuboresha mfumo hasa kupanfisha alama za ufaulu badala ya kuzishusha.
Hatupotezi Muda tunataka kuweka Sawa haya ili huyo mwanafunzi mwenye akili atambulike vyema na huyo mwenye akili lakini viwango vyake viko chini atambuliwe pia haina maana kuwa na mfumo wenye kutoa matokeo ya mwenye uwezo na asiye na uwezo wote waonekane na uwezo!!!Tunapoteza muda kubishana mambo yasiyo na msingi. Kama mwanafunzi Ana akili hata uweke mfumo gani atafaulu tu.
Kila mtu anauelewa wake juu ya jambo hili,kitila anaelezea umuhimu wa kuwa na sera ya elimu katika taifa ambayo itazuia mihemko ya viongozi wetu katika maamuzi,miaka michache iliyopita tuliitangazia dunia tumetoka katika division kwenda GPA mfumo ambao mataifa mengi wanautumia, badala ya kuuboresha kiongozi anauondoa kwasababu ambazo hazina mashiko .eti anataka majibu ya kisayansi wakati ameshakamia kuundoa.viongozi wetu katika hili wameongozwa na chuki na visasi kwahiyo lazima tutafute njia ya kuweza kudhibiti haya yasitokee tena.Hivi umekisoma alicho kiandika Kitila? ni wapi wana tofautiana na Ndalichako? Anacho hitaji Kitila ni msimamo na Debate! Muulize Kitila atupe mifano ya nchi iliyo andaa Debate ili kujadili mfumo wa elimu au upangaji matokeo!
Mimi ninachojua hapa kinacho hitajika ni utafiti wa kisayansi na sio kelele za kwenye Debate!
Tafiti zilifanyika zikaona mfumo wa division ndio unafaa na kama kuna tafiti zilifanyika kuonesha GPA ndio mfumo mzuri na pia kwa kushusha marks vile basi walitakiwa wawe wametuonesha na kueleza..! Wameshindwa kuitetea GPA ndio maana tumerudi kule tulipokuwa.
Hatuhitaji Debate kwenye mambo ya msingi bali tunahitaji tafiti!
Pengine hujui kinacho endelea kuhusu huo mfumo wa GPA unao tumiwa na baraza! Baraza wameenda mbali na kushusha viwango vya ufaulu...hivi hii ndio kuboresha? Waziri aliwapa siku saba watoe sababu za kisayansi za kutumia mfumo wa GPA dhidi ya mfumo wa Division wakashindwa ulitegemea nini?Kila mtu anauelewa wake juu ya jambo hili,kitila anaelezea umuhimu wa kuwa na sera ya elimu katika taifa ambayo itazuia mihemko ya viongozi wetu katika maamuzi,miaka michache iliyopita tuliitangazia dunia tumetoka katika division kwenda GPA mfumo ambao mataifa mengi wanautumia, badala ya kuuboresha kiongozi anauondoa kwasababu ambazo hazina mashiko .eti anataka majibu ya kisayansi wakati ameshakamia kuundoa.viongozi wetu katika hili wameongozwa na chuki na visasi kwahiyo lazima tutafute njia ya kuweza kudhibiti haya yasitokee tena.
Sababu ya Kitila ni anaogopa kuwaambia watu kuwa tulikuwa division tukaenda GPA na sasa tumerudi tena Divion.Sasa huyu Prof naye shida tu naye anataka kuwa profesa wa siasa. Tulikuwa na mfumo wa Division akaja mwingine akauondoa akaleta mfumo wa GPA huyu wa sasa ka-restore system, hivi ku-restore ni kufanya kitu kipya? Mimi nadhani sasa ni nafasi kwa huyu profesa kutoa maoni yake kwanini anadhani tuhame kwenye division na kwenda kwenye GPA maana kwa jinsi nilivyomsoma ni kwamba waziri wa elimu aliyeondoa division na kuleta GPA hakushrikisha wadau kwa hiyo huyu sasa ame-restore sysytem ili mtoe mawazo yenu
Nchi zote walishusha marks kama walivyo fanya baraza? Tatizo kubwa hapa ni kitendo cha Necta kushusha viwango vya ufaulu...! Halafu bado hatujawa na mfumo mzuri wa kutumia GPA kupanga matokeo kwa level ya chini!...Ruta, ngoja tusubiri tuone. Utakumbuka kuwa kipindi wanaanzisha GPA serikali ilisema kwamba wameamua kutumia GPA kwa sababu ni mfumo unao tumika katika nchi nyingi duniani. Hivyo kuepuka usumbufu kwa watahiniwa wetu kufanyiwa ulinganifu wa division vs gpa wanapo taka kujiunga na elimu ya juu au kazi nje ya Tanzania.
Nadhani hatujaelewana! Mimi ninaufahamu mfumo huu wa GPA vizuri tu, Kama dada joice angeondoa mihemko,angeuboresha mfumo huu pendwa wa nchi nyingi duniani ungeleta tija kwa taifa.ukweli kutoka moyoni mwake alishapania kuuondoa mfumo wa GPA, kuwapa siku saba NECTA ni geresha tu kwa wananchi ili wamuunge mkono, hatakama NECTA wangepewa miaka kumi wasingeweza kubadili adhma ya moyo wake juu ya jambo hili kwasababu alishapania.jiulize? majibu aliyopewa na NECTA aliwasomea yote?.alama za maendeleo zilitimika hata wakati wa division,na zitaendelea kutumika.Pengine hujui kinacho endelea kuhusu huo mfumo wa GPA unao tumiwa na baraza! Baraza wameenda mbali na kushusha viwango vya ufaulu...hivi hii ndio kuboresha? Waziri aliwapa siku saba watoe sababu za kisayansi za kutumia mfumo wa GPA dhidi ya mfumo wa Division wakashindwa ulitegemea nini?
Mfumo wa GPA sio mbaya lakini mbaya kutumiwa na elimu ya chini hasa wanapo ongeza na kushusha viwango vya ufaulu!
Isitoshe kutumia marks za maendeleo kama kigezo bado ni kujidanganya kabisa maana walimu wanaweza kumjazia tuu mwanafunzi marks zozote...!
Hivi kuwambia watu warudishe mfumo wa zamani kwa kuwa uliopo hauna tija ni mihemko? Nikwambie tuu mfumo wa GPA kamwe haufai kwa muundo wetu wa elimu ya chini..zaidi unatumika kuwabeba watu kwa marks za kupewa bure na walimu wao....hakuna chombo cha kupima kama kweli hizo marks za maendeleo wanazopewa ni halali...mfumo huo ni wakuwapumbaza watu tuu!Nadhani hatujaelewana! Mimi ninaufahamu mfumo huu wa GPA vizuri tu, Kama dada joice angeondoa mihemko,angeuboresha mfumo huu pendwa wa nchi nyingi duniani ungeleta tija kwa taifa.ukweli kutoka moyoni mwake alishapania kuuondoa mfumo wa GPA, kuwapa siku saba NECTA ni geresha tu kwa wananchi ili wamuunge mkono, hatakama NECTA wangepewa miaka kumi wasingeweza kubadili adhma ya moyo wake juu ya jambo hili kwasababu alishapania.jiulize? majibu aliyopewa na NECTA aliwasomea yote?.alama za maendeleo zilitimika hata wakati wa division,na zitaendelea kutumika.
wewe umesoma habari ipi? kama ni hiyo hapo juu inaelezea aliyebadili mfumo bila kushirikisha wadau ni mungai aliyeunganisha hesabu na civics, biology na kiswahili, physics na historia na chemistry na arabic.Sasa huyu Prof naye shida tu naye anataka kuwa profesa wa siasa. Tulikuwa na mfumo wa Division akaja mwingine akauondoa akaleta mfumo wa GPA huyu wa sasa ka-restore system, hivi ku-restore ni kufanya kitu kipya? Mimi nadhani sasa ni nafasi kwa huyu profesa kutoa maoni yake kwanini anadhani tuhame kwenye division na kwenda kwenye GPA maana kwa jinsi nilivyomsoma ni kwamba waziri wa elimu aliyeondoa division na kuleta GPA hakushrikisha wadau kwa hiyo huyu sasa ame-restore sysytem ili mtoe mawazo yenu