Kitila Mkumbo na Issa Shivji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitila Mkumbo na Issa Shivji

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Amanikwenu, Jan 17, 2011.

 1. A

  Amanikwenu Senior Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kazi yenu miliyoifanya kama UDASA siku ya Jumamosi ya tarehe 15/01/2011 ni nzuri na inastahili pongezi za kipekee.
  Kama mlivyoahidi inatia moyo kuona kuwa mtakuwa na mijadala mingi ya aina hiyo na kwa nchi nzima kama ikiwezekana. Binafsi naamini kuwa mmeishaanza kutafakari kuhusu mpango wenu wa utekelezaji ili kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anashiriki katika kuhakikisha kuwa nchi yetu inapata katiba mpya na iliyo bora.

  Pamoja na kile mtakachopanga katika kufanikisha lengo lenu kuu, naomba nami nipendekeze yafuatayo:-

  1. Baada ya kuwa na mpango kamili wa utekelezaji itisheni mkutano maalumu na vyombo vya habari ili kila chombo cha habari kitoe nafasi maalumu katika kufikisha moja kwa moja kile kitakachokuwa kikijadiliwa katika kila mdahalo katika siku husika--Ombi hili ni hasa kwa vituo vya Redio na Televisheni. Pia ziombeni Televisheni na Redio zetu zitenge muda maalumu wa angalau saa moja kila siku kwa ajili ya kuuelimisha umma wa Watanzania kuhusu katiba na njia ipi bora inafaa kutumika ili kupata katiba nzuri na iliyo bora. Kwa upande wa magazeti yaige mfano wa RaiaMwema ambalo limeanza kuichapisha katiba kuanzia toleo lake la tarehe 12/01/2011. Ni matumaini ya Watanzania wengi kuwa itawezekana kuwa na mdahalo angalau mmoja kila wiki ifikapo mwezi Machi mwaka huu.

  2. Kwa kuwa shughuli nzima ya kuzunguka nchi nzima na kuendesha Midahalo mbalimbali kuhusu katiba itahitaji fedha tunaomba muanzishe utaratibu maalumu ili Watanzania tuweze kuuchangia mpango huu kupitia njia mbalimbali kama vile simu zetu za mkononi. Mkumbuke kuwa kwa mwezi mmoja tu matumizi yetu kupitia simu za mkononi ni zaidi ya shilingi bilioni 185 (www.tcra.go.tz).

  3. Tengenezeni Timu Maalumu ya Wataalamu ambayo itazunguka nchi nzima kuendesha midahalo na kutumia ipasavyo vyombo vya habari katika kuelimisha Watanzania haja ya kuwa na Katiba mpya na ni mambo gani ya msingi yanapasa kuzingatiwa katika uandikaji wa katiba mpya.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  naunga mkono hoja ya haja
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Naunga mkono hoja.
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Naunga mkona Hoja, mimi nitakuwa wa kwanza kuchangia
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nami naunga mkono hoja.
   
 6. i

  ibange JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ni hoja nzuri. na pia kwa jambo hili kama udasa mkiwa approach donors ni rahisi kupata fedha za kutosha kueneza elimu kwa watz
   
 7. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good idea
   
 8. Innobwoy

  Innobwoy JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 980
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  Hakuna pingamizi
   
 9. a

  arasululu Senior Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I salute you sir/madam........ Mpango mzima
   
 10. A

  Amanikwenu Senior Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni muhimu sana wakaanza na sisi Watanzania. Kama tutawaangusha na wakakwama basi wanaweza kwenda kwa Wafadhili japo binafsi nachukia sana kwenda kwa Wafadhili kwa jambo ambalo liko ndani ya uwezo wetu. Kwa mfano kila simu ya mkononi ikichangia shilingi 25 tu kwa wiki (shilingi 100/= tu kila mwezi) wana uhakika wa kupata zaidi ya shilingi milioni 2000 kila mwezi. Hizi shilingi bilioni 2 zitafanya kazi kubwa sana kama tukiweka mbele moyo wa kujitolea ambao UDASA ndiyo wanautumia zaidi katika kufanikisha mambo yao. Kutoka kwangu wategemee kupata angalau shilingi elfu 20 kila mwezi wa muda wote watakaoendesha hiyo midahalo katika sehemu mbalimbali hapa nchini.
   
 11. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  siungi mkono, serikali itenge na kutumia rasilimali zetu, hakuna haja ya kuwabebesha mzigo wa tz wachache au labda serikali iwalipe hawa walimu kama konsaltants.
   
 12. t

  togo Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  siungi mkono hoja kwa nini kupoteza muda na hela hizo bilioni ulizotaja itakuwa dowans nyingine kama sio kagoda kengine,kama ulifuatilia mjadala wa jmosi pale nkrumah kuna mchangiaji mmoja alisema serikali sio sikivu tutaandaa semina, warsha ,kongamano ,kigoda,mikutano,mbongi nk lakini hiyo yote haitasaidia ,cha msingi tunajua tunataka nini basi serikali ikileta ujanja ni kuandamana tu wacha wafyatue risasi tufe kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu,kilichotokea nkruma juzi kimeshasahulika zamani lakini kilichotokea arusha tarehe 5 january hakitasahulika kamwe kimeishaingia wenye kumbukumbu za dunia so solution na peples power,
  nawasilisha
   
 13. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  unakubalika mkuu, kama pendekezo lako angeliandika kwenye magazeti lingekuwa bora na lingepunguza gharam, tuangalie tuwe na tume bora nayo isije kutuingiza ufisadi mwingine, maana CCM ukiwapa nafasi wanakumaliza
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  kila la kheri, mtakapo kuwa mnawazika watoto wa masikini ambao ndio huwa chambo mnapoandamana kama ilivyokuwa Arusha, mimi nitakuwa home na watoto wangu tunaangalia cartoon ya wacky races, mkipata hicho mnachokitafuta kama kinafaida na mimi nitakuwa mstari wa mbele katika kufaidi.
   
 15. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  naunga mkono hoja... JF inarudisha hadhi sasa kwa kuleta hoja zenye msingi na kujenga... na siyo kueneza chuki na kuwagawa wananchi
   
 16. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  You have a point there.Naunga mkono.
   
 17. z

  zamlock JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  naunga mkono nitachangia
   
 18. k

  kingtuma Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja na wanaokatisha tamaa ni mashetani hawatufai
   
 19. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mwanzo mzuri, naunga mkono..
   
 20. E

  Elifasi Senior Member

  #20
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa kabisa... kwanin tukae na madigrii yetu, na marasilimali mengine kibawo na bado tuendekeze kwenda omba omba kila tunapotaka fanya kitu? Mfano yaani hata kondomu za ku**na na wapenzi wetu mpaka tufadhiliwe...Ndo maana hatutilii maanan kudai matokeo maana hayatuumi!
  HIli la katiba ili limguse kila mtanzania, hela itoke kwetu ituume!ILA MKUU IYO INAITWA BILIONI MBILI, SIOmilioni elfu mbili, tehteh...najua unajua, ila nataka tuelewe vizuri zilivo nyingi!!

   
Loading...