Kithuku Waziri Mkuu

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
213
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amemteua Bw Brian Jonathan Yared Kithuku kuwa Waziri Mkuu. Mh Rais pia amemteua Bw Kithuku kuwa mbunge masaa machache kabla. Bw Kithuku ataapishwa kwanza kuwa mbunge huko Dodoma, kisha wabunge watapiga kura ya kumthibitisha. Mh Kithuku anachukua nafasi ya Bw Edward Lowassa ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Somalia.

"Baada ya mabadiliko haya, tarajieni surprises zaidi" alisema Mh Rais.

Mh Kithuku atalazimika kukatisha masomo yake ya shahada ya Uzamivu (PhD) katika Sera na Mipango ili arejee nchini kukabiliana na majukumu yake mapya. Hii ni mara ya kwanza kwa Mh Rais ku............


Mwaonaje hii Wana-JF? Baada ya "kamba" za Bwana Huruma "aliyetuokota" kwamba ati yu jikoni (sijui yuapikani?), na wale waliotusubirisha twapiga miayo kutwa ati "kabineti mpya kutangazwa kesho", ati "majina yako mezani kilichobaki kutangazwa tu" nk, haya bwana miye yangu macho. Wale waliowahi kuota zile "ruya za kupaa angani usiku" wanajua utamu wake. Kama ndicho tulichojaliwa, kwa nini tujinyime? Tujipe raha wenyewe, au vipi?
 
Kithuku huyu Bwana ni Mkenya huyu. Ila kwa Tanzania inawezekana Mkenya akashika madaraka serikalini, hatuangalii uraia sisi bali tunaangalia anaishije na jamii inayomzunguka. Mambo rahisi kabisa.
 
kaaazi kweli kweli
mheshimiwa kithuku usisahau kuwa PM aliyepita hakuwa anakaa ofisini hivyo malizia viporo vya nyaraka (mlima) utakazizikuta mezani na ukome kukubali-kubali madaraka
 
Nauliza Hivi Hii Itatangazwa lini kwenye Vyombo vya habari Bongo au ni Nyepesi isiyo na Uhakika? Pia bwana Kithuku Twataka Mabadiliko Bongo Umaskini mpaka lini?
 
kama kweli vile, sina mbavu! hasahasa kipande cha Lowasa balozi wa TZ nchini Somalia.

Anyway, najua ni utani, lakini inatuambia wale waliotabiri kwamba baraza la mawaziri linavunjwa, oohhh mara PM mwingine anakuja, tafadhari msiseme kama hamna uhakika.
 
Back
Top Bottom