Kiteto: Mwili wa mtu asiyejulikana wakutwa umefukiwa kando ya barabara

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Jeshi la Polisi wilayani Kiteto mkoani Manyara, limefukua mwili wa mtu mmoja ambaye hajafahamika ukiwa umeharibika vibaya huku ukiwa umezungushiwa mfuko aina ya salfeti na kufukiwa chini katika kijiji cha Mbigili, Kata ya Partimbo.

Tukio la kufukua mwili huo limefanyika hii leo Oktoba 12, 2022, katika eneo la Kijiji cha Mbigili Kata ya Partimbo mkoani Manyara, na kwamba mwili huo umekutwa ukiwa umeharibika vibaya tena ukiwa umezungushiwa mfuko wa salfeti mithili ya sanda na kufukiwa pembeni mwa barabara itokayo kijiji cha Mbigili kuelekea Kiteto.

Mabaki ya mwili huo wa marehemu uliofukuliwa yamehifadhiwa chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Kiteto huku ikielezwa kuwa uchunguzi zaidi wa Polisi unaendelea kutambua mwili huo.

Kiteto.jpg

Baadhi ya maafisa wa Polisi wakiwa na mwili walioufukua​
 
Back
Top Bottom