Kitengo cha Ufuatiliaji katika Radio&TV. (Follow up department) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitengo cha Ufuatiliaji katika Radio&TV. (Follow up department)

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Radio Producer, Apr 28, 2011.

 1. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Hello mwana JF unayesoma,
  Leo nimeamua kuchangia machache katika suala hili. Ninaimani watakaohusika watajifunza. Radio na TV nyingi hapa nchini kwetu zimeshindwa kufanya vizuri zaidi kwa sababu hazina vitengo vya Ufuatiliaji ya Follow up de...... Ninaposema zimeshindwa kuboresha nina maanisha kila kukicha radio zetu na TV zetu zinafanya mambo yale yale, ubunifu wao haukui, makosa ni yale yale utafikiri hawayaoni kabisa. Mfano mzuri katika TV zetu kubwa ITV, StartTV, TBC kumekuwa na tatizo katika usomaji wa taarifa mtangazji akisema tupate taarifa zaidi pana kaa kimya taarifa haiji mara tunakuomba radhi kwa kuwa taarifa hiyo haijawa tayari kwa sasa..... sasa uliitangaza kwa nini kama haijawa tayari?? Wakati mwingine Tele prompter wanayosomea habari huwa ina loose mtangazaji analazimika kusoma kwenye karatasi. Haya matatizo hayana uvumbuzi?? Yatakuwepo mpaka lini? Mbona TV kama za CNN hakuna vioja kama hivyo? Hii inatokana na ukosefu au mapungufu ya kitengo cha ufuatiliaji.

  Kitengo cha ufuatiliaji kinatakiwa kuwasiliana na audience na kusikiliza maoni yao, Kisha kuyafanyia kazi. Kama watazamaji au wasikilizaji wanakosoa jambo fulani ni vizuri likatatuliwa na kuisha kabisa. Kuna barua nyingi, sms nyingi, email nyingi za wadau mbalimbali hutuma kwenye stations zetu lakini respond ni ndogo sana.

  * Kitengo cha ufuatiliaji kinatakiwa kurespond feedback zote: Negative na Postive ili kuimprove radio au TV.
  * Lugha nzuri kwa wasikilizaji wa aina zote inatakiwa.
  * Kushughulika na matatizo ambayo wasikilizaji wanaomba kusaidiwa.
  * Kuheshimu maoni ya msikilizaji, aidha awe targted audience au bonus audience.
  * Kukusanya maoni ya wasikilizaji kuwa nini wanapenda kifanyike na mfumo wa matangazo wanaoupenda ili kuweza kuboresha mtangazo yao.

  KATIKA RADIO&TV TUNASEMA: Faida ya Radio/TV ni kusikilizwa. Msikilizaji ndiye mwenye maamuzi ya kukusikiliza au la, je unafanya nini kumuridhisha??

  Wahusika jitahidini kuweka vitengo vya ufuatiliaji katika stations zenu.

  Nawasilisha
  Radio Producer.
   
 2. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thank you Radio Producer! Hivi wewe unaishi wapi Radio Producer? Unafanya kazi wapi? make mambo yako yanasomeka kwanini usingemwambia JK akutupie TBC uwe TIDO? teh teh teh God bless you
   
 3. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  JF is good has connected me with many people! Now i am doing good, ur welcome
   
 4. F

  Ferds JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  tatizo vyombo vyetu vya habari vipo kisiasa zaidi, wao hawaangalii mengine ndio maana hivyo vitengo havipo, na pale amabapo vipo haviwajibiki ipasavyo
   
 5. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  RP unaongea kweli kabisa lakini ndugu Kama una kumbukumbku nzuri Radio/ TV/Magazeti huanzishwa kipindi tunaelekea uchaguzi mkuu, so they establish those projects not because they real want to earn money from those media directly ila wa- earn money pale watakapochaguliwa baada ya kupiga kampeni kwa kutumia vyombo vyao. na ndio maana media nyingi zinakufa miaka michache baada ya uchaguzi hasa wasipofanikiwa kuchaguliwa!!
   
 6. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Umesema kweli ndugu yangu! Asante sana kwa mchango wako!
   
 7. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Natamani kufanya mapinduzi kwenye vyombo vya habari basi tu Mungu nisaidie!
   
Loading...