SaaMbovu
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 6,028
- 5,359
Habari wana JF hasa katika jukwaa hili.
Kweli kama unapenda kitu ni vigumu sana kujizuia. Katika mechi ya Simba na Yanga kiukweli nilipata kusikiliza kupitia radio station anayo tangaza Kitenge. Kama ni unazi na Yanga kweli anao maana goli linapofungwa na Yanga utajua tu jinsi anavyoweka manjonjo yake. Ila nilimuonea huruma pale goli la 3 liliporudi ikabidi aseme tu "Yanga hawaamini ndugu msikilizaji" Bora angesema yanga hatuamini. Halafu goli lilitangazwa kinyonge sana. Then wakati wa kipindi cha michezo akihojiwa na mtangazaji mwenzio kwa kweli aliongea kwa masikitiko sana utadhani yeye ndio kocha wa Yanga.
Jamani Watangazaji Wa Soka Punguzeni Ushabiki Hasa Wakati Wa Kutangaza Mpira Wa SIMBA NA YANGA.