Kitendo cha viongozi wa CHADEMA kupuuza kushiriki kongamano la dini ni aibu na fedheha kwa chama chao

Wadau,

Recalling back to Kongamano lililoandaliwa na viongozi wa dini zote (wakristu/wakristo na waislamu), Kongamano ambalo pamoja na mada na jumbe mbali mbali zilizowasilishwa, lakini pia ilikuwa na mada moja kuu ambalo ilikuwa ni Kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Hayati Dr. John Pombe Magufuli.

Lile kongamano lilikuwa kubwa, na lilihudhuriwa na viongozi wengi wa dini, viongozi wa serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama yetu Samia Suluhu Hassan aliyeambatana aliyeambatana na Makamu wa Rais Philip Mpango, Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Ibrahim Juma, viongozi wa ulinzi na usalama, mawaziri na manaibu mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na viongozi wengine wengi kwa ujumla wao.

Kongamano pia lilihudhuriwa na viongozi wa siasa walioambatana na msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi. Kwa upande wa viongozi wa vyama vya siasa tulimwona Mh. John Shibuda.

Jambo la kushangaza hatukuwaona wanaojidai chama kikuu cha upinzani Tanzania, tena kwenye tukio muhimu la Kumshukuru Mungu kwa nchi yetu kubaki salama hata baada ya kifo cha Rais Magufuli, na Mama yetu Samia kuapa kuongoza nchi katika mazingira salama na safi.

Kitendo cha CHADEMA kususia kushiriki kongamano kinatuonyesha sisi watanzania tuwaangalie kwa jicho la pili, maana inadhihirisha hawa jamaa hawana uzalendo, na ndiyo wanaocheza ngoma za fitna mitandaoni wengine wanademka huko.

Ushauri wa bure kwa CHADEMA. Kuweni wazalendo, achaneni na siasa za chuki, kubalianeni kutokukubaliana maisha yasonge mbele. Kauli ya mama yetu Samia kwamba ni wakati wa kuungana pamoja na kufutana machozi haitakuwa na maana kama mmejifungia twiter huku mmenuna.

Badilikeni
Kuna makosa mawili yaliyofanyi na hao waandaa kongamano.
AGENDA,KUMSHUKURU MUNGU KWA MAISHA YA MAGUFULI HAPA DUNIANI
1. Mangufuli aliwachukia Sana wapinzani, akawafunga korok8roni, aliwateka, alipiga risasi na kuwaua wengine.
MLITAZAMIA WAPINZANI WAKASHUKURU HILO
KWA HAKIKA WATASHUKURU MUNGU KUMUONDOA

2.Wakati magufuli anawaburuta wapinzani na kuwaua mbona hawakuitisha kongamano la kumwomba Mungu ili uonevu uondolewe?
Leo mlitazamia wapinzani wakusanyike kwa unafiki unaofanywa na hao viongozi wa dini?

HUO NI USHENZI SAWA NA USHETANI TU
 
Walialikwa? Tuanzie hapo

Kwa hao viongozi wa dini tulionao kwenye nchi yetu kwa sasa sitegemei watoe mualiko kama huo.
 
Walialikwa? Tuanzie hapo

Kwa hao viongozi wa dini tulionao kwenye nchi yetu kwa sasa sitegemei watoe mualiko kama huo.
Kongamano lilitangazwa kwenye nyumba za ibada, na viongozi wa kada zote walialikwa. Unless viongozi wa CHADEMA hawana dini, hivyo hawakupata taarifa kwakuwa hawaendi makanisani wala misikitini.
 
Wangekua wenyewe ungesikia serikal ndio imemuua kiongoz wao ndiomana hakwenda mfano kwa Tundulisu alipopigwa Risas waliamua kusema Magufuli ndio Kampiga Risas sabab tu hakwenda kumuona
 
Back
Top Bottom