Kitendo cha viongozi wa CHADEMA kupuuza kushiriki kongamano la dini ni aibu na fedheha kwa chama chao

Apr 12, 2021
31
22
Wadau,

Recalling back to Kongamano lililoandaliwa na viongozi wa dini zote (wakristu/wakristo na waislamu), Kongamano ambalo pamoja na mada na jumbe mbali mbali zilizowasilishwa, lakini pia ilikuwa na mada moja kuu ambalo ilikuwa ni Kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Hayati Dr. John Pombe Magufuli.

Lile kongamano lilikuwa kubwa, na lilihudhuriwa na viongozi wengi wa dini, viongozi wa serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama yetu Samia Suluhu Hassan aliyeambatana aliyeambatana na Makamu wa Rais Philip Mpango, Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Ibrahim Juma, viongozi wa ulinzi na usalama, mawaziri na manaibu mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na viongozi wengine wengi kwa ujumla wao.

Kongamano pia lilihudhuriwa na viongozi wa siasa walioambatana na msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi. Kwa upande wa viongozi wa vyama vya siasa tulimwona Mh. John Shibuda.

Jambo la kushangaza hatukuwaona wanaojidai chama kikuu cha upinzani Tanzania, tena kwenye tukio muhimu la Kumshukuru Mungu kwa nchi yetu kubaki salama hata baada ya kifo cha Rais Magufuli, na Mama yetu Samia kuapa kuongoza nchi katika mazingira salama na safi.

Kitendo cha CHADEMA kususia kushiriki kongamano kinatuonyesha sisi watanzania tuwaangalie kwa jicho la pili, maana inadhihirisha hawa jamaa hawana uzalendo, na ndiyo wanaocheza ngoma za fitna mitandaoni wengine wanademka huko.

Ushauri wa bure kwa CHADEMA. Kuweni wazalendo, achaneni na siasa za chuki, kubalianeni kutokukubaliana maisha yasonge mbele. Kauli ya mama yetu Samia kwamba ni wakati wa kuungana pamoja na kufutana machozi haitakuwa na maana kama mmejifungia twiter huku mmenuna.

Badilikeni
 
Kwani bado wapo maana hata kigoma hawajashiriki uchaguzi mdogo, walitegemea kitu wamekosa wanendelea kusubiri mtelemko mwingine nao watakosa yaani haya majamaa yatasubiri sana, labda karne ijayo.

Eti katiba mpya, wakati wa mchakato waliingizwa mkenge la ze la professee wakakimbia mchakato, sembuse mchakato wa kesho. Akili ndogo
 
Mleta mada amekosea au? Kwani Chadema ipo, si ilishajifia? Maana tunasikia wananchi wa Tanzania waliikataa Chadema kwenye sanduku la kura na wakawapigia kura za ndiyo sisiemu wakajazana bungeni. Sasa watu hawatakiwi na wananchi, huko kwenye kongamano waje kama nani? Jamaa wanateseka sana
 
Chama kimekufa lkn wanachama bado wapo hai, kwahiyo wangefika hata wanachama isingekuwa mbaya.
 
Wadau,

Recalling back to Kongamano lililoandaliwa na viongozi wa dini zote (wakristu/wakristo na waislamu), Kongamano ambalo pamoja na mada na jumbe mbali mbali zilizowasilishwa, lakini pia ilikuwa na mada moja kuu ambalo ilikuwa ni Kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Hayati Dr. John Pombe Magufuli.

Lile kongamano lilikuwa kubwa, na lilihudhuriwa na viongozi wengi wa dini, viongozi wa serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama yetu Samia Suluhu Hassan aliyeambatana aliyeambatana na Makamu wa Rais Philip Mpango, Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Ibrahim Juma, viongozi wa ulinzi na usalama, mawaziri na manaibu mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na viongozi wengine wengi kwa ujumla wao.

Kongamano pia lilihudhuriwa na viongozi wa siasa walioambatana na msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi. Kwa upande wa viongozi wa vyama vya siasa tulimwona Mh. John Shibuda.

Jambo la kushangaza hatukuwaona wanaojidai chama kikuu cha upinzani Tanzania, tena kwenye tukio muhimu la Kumshukuru Mungu kwa nchi yetu kubaki salama hata baada ya kifo cha Rais Magufuli, na Mama yetu Samia kuapa kuongoza nchi katika mazingira salama na safi.

Kitendo cha CHADEMA kususia kushiriki kongamano kinatuonyesha sisi watanzania tuwaangalie kwa jicho la pili, maana inadhihirisha hawa jamaa hawana uzalendo, na ndiyo wanaocheza ngoma za fitna mitandaoni wengine wanademka huko.

Ushauri wa bure kwa CHADEMA. Kuweni wazalendo, achaneni na siasa za chuki, kubalianeni kutokukubaliana maisha yasonge mbele. Kauli ya mama yetu Samia kwamba ni wakati wa kuungana pamoja na kufutana machozi haitakuwa na maana kama mmejifungia twiter huku mmenuna.

Badilikeni
Hivi wale wanaodemka bungeni ni wa Chama gani vile? Umenena vema, hawa Chadema hawafai kabisa. Tumewapeleka bungeni kwa wingi kabisa halafu badala ya kujadili maslahi ya Taifa wao wanademka na Mwendazake.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom