Kitendo cha Juma Nature kumkejeli na kumdhihaki Diamond ni ishara ya wivu

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,511
2,000
JF....!
Hivi sasa kuna wimbo mpya wa msanii Juma Nature feat Jay Dee unaioitwa "kama jana" wimbo huu ni mzuri sana pia una maudhui mazuri ya kuwahasa wasanii kufanya mziki kiubunifu kama wa bongo flava ya zamani ambao ulidumu.

Lakini kilichonisikitisha ni verse ya Juma nature ambapo kuna maneno ya kumdhihaki na kumkejeli msanii Diamond Platinumz kuwa mkata mauno na limbukeni wa umaarufu" hali hii imenifanya nijulize maswali mengi kama Nature aliwaza nini hadi kuimba hivyo? au ndio kusema huu ni muendelezo wa fustration za wasanii wa zamani baada ya kuona mziki wao umezidiwa soko na vijana wa sasa wanaochipukia?
 
Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
1,231
2,000
shangaa sasa yeye wala hana time nae...wao si waliendekeza bangi na ulevi wacha wafulie tu

Nadhani ni kama wanavyoendekeza wanawake na kujisifia kusiko na ukweli. Ngoja tuone baada ya miaka 3 kutoka leo kama wataendelea kuwa hawa hawa tunaowasikia leo, kwangu mimi wanapita mule mule walimopita watangulizi wao, hawana jipya!
 
theki

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
2,724
1,195
We unauhakika gani ndio daimondi katajwa au upo kwenye mwendelezo?ile ni ushairi tuu ila huu mtazamo wangu tuu.
 
CHAZA

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
7,431
2,000
We unauhakika gani ndio daimondi katajwa au upo kwenye mwendelezo?ile ni ushairi tuu ila huu mtazamo wangu tuu.

Nilijaribu kurudia kuusikiliza wimbo huo sjasikia jina la Diamond kutajwa. Nilisikia neno Dada Mondi tu, kisheria hata ukienda Mahakamani Dada Mondi na Diamond ni vitu/ watu tofauti kabisa!
 
Muuza Sura

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,988
1,250
Nadhani ni kama wanavyoendekeza wanawake na kujisifia kusiko na ukweli. Ngoja tuone baada ya miaka 3 kutoka leo kama wataendelea kuwa hawa hawa tunaowasikia leo, kwangu mimi wanapita mule mule walimopita watangulizi wao, hawana jipya!

mkuu huyu diamond ni miongoni mwa wanamuziki wenye discipline ya hali ya juu katika maisha!hapo alipo hajafika kwa kubahatisha ila ni juhudi,kujituma na heshima kwa kazi yake na wanaomzunguka!nna uhakika watu wengi wanaomchukia diamond hawajabahatika kukaa nae na kumsoma fresh
 
Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
1,231
2,000
mkuu huyu diamond ni miongoni mwa wanamuziki wenye discipline ya hali ya juu katika maisha!hapo alipo hajafika kwa kubahatisha ila ni juhudi,kujituma na heshima kwa kazi yake na wanaomzunguka!nna uhakika watu wengi wanaomchukia diamond hawajabahatika kukaa nae na kumsoma fresh

Mkuu, kwa haraka haraka unadhani pesa anayotamba kuwa nayo jamaa ni muziki anaofanya ndo unampatia na anayo kweli? Hakuna shoo wala mikataba ya ela yote hiyo kwa muziki huu wa bongo. Nidhamu aliyonayo ni ipi haswa mkuu? Ngono anayoendekeza au sifa? Si juhudi, kujituma wala nidhamu katika kazi vilivyomfikisha hapo; muulize vizuri pengine atakueleza siri ya mafanikio. Nadhani hata ile nyumba tuliyoambiwa itamgharimu 260mil bado haijaisha mpaka leo tangu itangazwe, gari la mil 90 nafikiri; alishindwa kulipa. Kila mara tunaona anavyotudanganya na mafanikio yake kimuziki nje ya bongo; hapo Nigeria tuu mkuu hawamjui, si yeye wala marehemu Kanumba. Yapo wanayoyafanya nyuma ya pazia pengine lakini si muziki tuu.

Zipo juhudi unaweza kukubali kuwa zinaendana na pesa aliyonayo mtu kulingana na hali halisi ya maisha nchi kwetu lakini si kihivi anavyotaka kutuaminisha jamaa. Kama wewe ni muumini unaweza hate kurejea kitabu chako cha imani kikakueleza kuwa hamna mafanikio yasiyolingana na kazi/juhudi uifanyayo.

Chukua nyimbo yoyote ya bongofleva iliyotengenezwa pengine kuanzia mwaka 1997 mpaka 2004, kisha fananisha na zilizotengenezwa baada ya hapo, utakubaliana na mimi kuwa hapo awali walikuwa na juhudi zaidi kuliko sasa.

Mkuu, sina ushabiki kwa msanii yoyote, mimi ni mshabiki wa muziki kidogo na baadhi ya wanamuziki na si wasanii.
 
mwakibete

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,987
2,000
Mkuu hebu tusiandikie mate, tafuta huo wimbo usikie mwenyewe.

Kama nitakuwa nimemsikia vizuri na kukumbuka vizuri, kaimba ".....usiwe limbukeni we dada mond.........". Kama wewe umejua aleimbwa ni diamond, ujumbe utakuwa umefika. Mimi pia namjua huyo dada mond.
 
serio

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
6,931
2,000
mkuu huyu diamond ni miongoni mwa wanamuziki wenye discipline ya hali ya juu katika maisha!hapo alipo hajafika kwa kubahatisha ila ni juhudi,kujituma na heshima kwa kazi yake na wanaomzunguka!nna uhakika watu wengi wanaomchukia diamond hawajabahatika kukaa nae na kumsoma fresh

It aint good if they aint hating... Nimekuja kugundua hilooo
 
Aquatic

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
715
225
Juma Nature Bado anamawazo yale ya miaka ile kwa kupendwa kupitia nyimbo zake alizokuwa akiimba ,kwasasa hatuaangalii uliimba nini tuangalia unaimba nini,BANGE MBAYA SANA pamoja na madawa wasanii wengi wamepotea walichobaki ni kuhisi zile zama zinaweza kujirudia,hilo halitowezekana kwasasa hatulie tu km inawezekana akatafute pori alime BANGE zake vizuri nafikiri zitamtoa..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom