Kitendawili kimetegwa - Kikwete Tegua...

kwa hotuba ya leo ameonyesha kwamba hataki utani kwenye mambo ya msingi yenye maslahi kwa taifa na atapambana na yeyote anayeona Rais hana mamlaka hayo
 
Mkuu wangu hili ni swala la logic tu halina sababu ya kubabaishana. Nahodha hawezi kupanga utengenezaji wa meli wala hakuna aliyeshika uchoraji wala utengenzaji wa Meli iwe mpya ama kukuu..

Pengine wewe hujasoma mapendekezo ya Chadema kwani unatakiwa uwe nani ili usikilizwe! Haya ndio mawazo yenu wanaCCM ama kweli hamna tofauti na Madikteta...Ikiwa Jk hajui tatizo la katiba iliyopo ama sisi wananchi tunataka nini, ataweza vipi kuwachagua watu wenye uwezo wa kujenga katiba tuitakayo!

Nimesoma mapendekezo yao..na walikuwa na nafasi pia ya kuyaeleza kufafanua kwenye mjadala walioukimbia??

Sioni tofauti ya chadema na tlp, umd ..wote wana haki sawa..

Wananchi watasikilizwa na kushirikishwa..kama chadema hawataki kushiriki well..
 
hata kama kasema point lakini kwa wanachadema hotuba hii ni mzigo mzito na mwiba mkali
 
ni wapi ukaona wanaccm wakasifia hotuba ya kiongozi wa chadema na wale wa chadema wakasifia hotuba ya kiongozi wa ccm.
 
tutizamo yaliyomo katika hotuba sio tumtizame JK tusiyemkubali

Pipijojo Jk amesimamia maamuzi yenye Tija kwa ccm na serikali yake lakini sio MASLAHI YA TAIFA. Furahia yanayotokea leo na ujivunie kwa hayo kesho usije juta.Angalieni jirani zetu Kenya Jaji wa mahakama anaomba kazi kama anavyoomba IT TECH,sisi bado tunateuana wapi uhuru wa mteule kama si kufuata maagizo ya aliyemteua
 
"Tume itasikiliza maoni hayo na baadaye kutengeneza rasimu ya Katiba mpya ambayo baada ya kukubaliwa na Bunge itafikishwa kwa wananchi kutoa ridhaa yao kwa kupiga kura" - JK

"Ni kutokana na hoja hizo Spika akaamua Muswada uendelee kujadiliwa na Bunge na leo Bunge limeupitisha Muswada huo. Baadae Muswada utaletwa kwangu kwa ajili ya kutiwa saini uwe Sheria. Baada ya hapo itabakia kazi yangu na Rais wa Zanzibar kuunda hiyo Tume ili mapema mwakani kazi ya kukusanya maoni ya wananchi ianze. Lengo letu ni kuwa ifikapo mwaka 2014 zoezi zima liwe limekamilika ili mwaka 2015 tufanye uchaguzi tukiwa na Katiba mpya. Itapendeza tukisherehekea miaka 50 ya Muungano na Katiba mpya. Ni matumaini yangu kwamba wananchi wote watashiriki kwa ukamilifu kutoa maoni yao kwa Tume hiyo" - JK

Hapa ndo pananipa utata sana juu ya dhamira halisi ya kupata kitu/katiba safi yaani mpaka aamue(rais) kuteua watu awatakao, na kuamua yepi yawemo ama yasiwemo
 
Kitendawili tega...... MMJ hataweza kutegua hope atakupa mji tu,
 
Nimesoma mapendekezo yao..na walikuwa na nafasi pia ya kuyaeleza kufafanua kwenye mjadala walioukimbia??

Sioni tofauti ya chadema na tlp, umd ..wote wana haki sawa..

Wananchi watasikilizwa na kushirikishwa..kama chadema hawataki kushiriki well..
unataka chadema waseme nini tena wakati msimamo wao wameshautoa bungeni au ukusikia mjomba. there was no logic kuendelea
kukaa bungeni kwani utakuwa ni kama umeubariki mswada mzima. wanegeedelea tu endapo wangeweza kubadili litu chochote lakini
kitu amabacho kinachofuata ilikuwa ni kupiga kura kuhusu mswada na matokeo sote tunayajua kwahiyo it was wasting of time kukaa
bungeni wakati unajua kuwa unawajengea political legitimancy.
 
Mkuu huwa napenda maelezo yako lakini tatizo huwa unatumia maneno meeeengi yanayojirudiarudia. Yaani hadi mtu unafika katikati hata huelewi paragraph ya kwanza inaongelea nini. Kifupi insha zako hazina muendelezo.
Mwita nilianza kuona umebadilka kumbe ni bomu namna hii!!! Maelezo mengi yakowapi??Ama kweli ukitaka kumumuibia Mtanzania Mwanzoni weka maelezo mazuri katikakati weka vipengengele vyako na mwisho muwekee maneno matamu halafu malizia na signature..Ndio maana tunaiingizwa mikenge kwenye mikataba chungu mzima sababu ya uvivu wa kusoma. Badilika bwana..
 
Mwaka 2007 Professor Watson wa DNA alisema kuwa ngozi nyeusi tuna mapungufu kwenye kufikiri tukampinga kuwa anatudhalilisha.

Ila msomi mmoja akahoji, "je matendo yetu yanafanana na tunavyotaka kusifiwa hata kwa tusiyofanya?". Lengo ni kuhoji matendo yetu kama kweli sisi waafrika ni watu wa kuaminika.
Na historia inaonyesha kuwa waafrika hatujifunzi kutokana na makosa ya wenzetu kisa kila mmoja anatafuta kusifiwa. Mogogoro mingi sana imetokea lakini hatuonyeshi kujifunza. Sasa je tuna legacy ya kukanusha ile kauli ya gwiji wa biologia?
 
Ndugu zanguni hakuna cha katiba mya hapo ni kiini macho. Kinachofanyika ni kuandika katiba ya CCM na sio ya wanachi.
Huu udicteta utaisha lini?
 
Nimesoma mapendekezo yao..na walikuwa na nafasi pia ya kuyaeleza kufafanua kwenye mjadala walioukimbia??

Sioni tofauti ya chadema na tlp, umd ..wote wana haki sawa..

Wananchi watasikilizwa na kushirikishwa..kama chadema hawataki kushiriki well..

Mrs CCM,Kwani CHADEMA sio wananchi? mawazo yenu duni ,hamsomi alama za nyakati.Hamjui supporters wa CCM ni kina nani this time,hamjui age yao na population yao.Wale wazee waliokuwa wanapiga makofi jana hawaelewi kitu na wanaelekea kufa,in four years time wazee wengi watakua wamevuta.Tutabaki sisi vijana tuwaoneshe kazi.Jana angethubutu kwenda kwenye uwanja huru ambao wahudhuriaji ni vijana,badala ya makofi angezomewa.

JK ni rais wa Tanzania,lakini kwa ulegelege wake i will never support him,i will rather hate him forever and ever''''
 
Nimesoma mapendekezo yao..na walikuwa na nafasi pia ya kuyaeleza kufafanua kwenye mjadala walioukimbia??

Sioni tofauti ya chadema na tlp, umd ..wote wana haki sawa..

Wananchi watasikilizwa na kushirikishwa..kama chadema hawataki kushiriki well..
Mkuu bado hata hunielewi kabisa.... Hili sio swala la CDM, CCM,TLP na kadhalika isipokuwa ni swala la Watanzania wote na mimi nazungumza kama Mtanzania na sii CDM wala NCCR.. Hakuna kati yetu mmoja mmoja mwenye mamlaka ya kuunda tume hilo kwanza..

Labda nikuulize wewe, Hivi utaratibu gani hufanyika inapotakiwa kuundwa katiba hata ya Jumuiya au chama? Je hutokea mtu mmoja kuandaa tume, nani ahusike na akapanga nini kifanyike bila kuwasilisha mapendekezo hayo kwanza kwa wanajumuiya au Wanachama!.

Nitarudia tena kusema kwamba CDM hawataki kuwa wao ndio watakao panga tume au washirikishwe wao na sio TLP, CUF au UMD isipokuwa swala hili kwanza lipelekwe kwa wananchi ambao wao wataamua ni tume gani inafaa kuhusishwa. Pengine labda tumuombe sote JK atuulize sisi tunataka taasisi gani zihusishwe na muundo wa tume husika..

Mkuu wangu sina sababu ya kuendelea kubishana juu ya hili ama CDM na CCM..hivi ni vyama ambavyo kesho naweza kuvipinga na kutokuwa mwanachama wa chama chochote lakini siwezi kujivua Uzawa wangu hata kama..JK kaunda tume ngapi? nambie hata moja ilokuja na jibu la kuridhisha. Richmond mtu ameonekana guilty kabisa leo ni mbunge, wengine kina Msabah, Meghji wanakula bata tu. Nahakika hata hilo la Jairo litapita na watu watalisahau maisha yanaendelea...Tazama athari za NEC kuwa chini ya rais, UWT na vyombo vya dola unafikiri JK atachagua kamati inayoweza kweli kuleta matoke halali ambayo mengi yake ni dhidi ya chama chake, serikali namahakama?. Mambo mangapi yamepitishwa hivi hivi mbele ya macho yetu na kudai hakuna ushahidi na tusiwe na jibu isipokuwa kukubali matokeo.

Kama sikosei ingawa najua utabisha, NEC ktk matokeo ya uchaguzi ktk baadhi ya Majimbo Mbunge wa CDM anapata asilimia 70 lakini kwa rais JK alipata 70 tena Mkoa wa Kilimanjaro... Matokeo ya Zanzibar na kadhalika hvi vyote ni vyombo vya rais na hata uanapochagua tume ya kuyachunguza hua hatupati ukweli..Hata kuzama kwa meli majuzi tu huko Zanzibar hatuna hesabu kamili ya walokufa na kina nani wamehusika na hatua gani zimechukuliwa kuhakikisha maafa kama yale hayatokei tena. Hakuna sheria yoyote iloundwa dhidi ya vyombo vya usafiri kwa sababu hatujui hadi leo kilitokea nini?


Labda nimalizie tu kwa kusema hatuna muda wa kupoteza kufikia 2015. JK akichagua tume ambayo mathlan wananchi wengi wamesema moja ya kifungu wanachokitaka ni kuhakikisha rais aliyefanya ufisadi wakati akiwa rais anaweza kufikishwa mahakamani na kushtakiwa!...Je, Unafikiri hiyo tume italiweka swala hili mbele?.. Just curious!..Nina hakika watalichakachua na kuhakikisha linaondolewa hata kama rais wa Zanzibar na bara wamehusishwa kwa sababu elewa tu sababu kubwa ya wananchi kuomba katiba imetokana na nguvu kubwa ya chama tawala na rais kama ilivyoasisiwa wakati wa chama kimoja mwaka 1977. Na wasomi husema tatizo kubwa la UJAMAA ni UDIKTETA na tatizo kubwa la UBEPARI ni UFISADI..na yote haya mawili hutokea kundi dogo la watu kuwa the Elites ambao hujilimbikiza mali kama katiba haitawabana ili kulinda maslahi ya wananchi wake..

Hivyo Tanzania ya leo imebakia na makovu ya Ujamaa ambao yana Udikteta ktk Katiba na sasa Ubepari ulojaa mafisadi, mchanganyiko huu hauwezi kwisha kwa kesi ya Nyani kumkabidhi Ngedele..Lets face the truth - CCM wanajua wazi kwa nini wamepitisha muswada huo na CDM wanajua fika wanayoyataka wananchi hayawezi kupatikana ikiwa kesi atapewa Ngedele (tume). Kukusanya maoni ya wananchi itakuwa formality tu majibu hayawezi kuwa sawa kama tunavyotangaziwa matokeo ya kura za uchaguzi, na hatuwezi kubisha wala kuaminiwa kisheria kwa sababu wananchi hatuna ushahidi wala ubavu wa kushindana na dola..
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ndugu zangu Kitendawili kimetegwa nani atakitegua. Chama cha Mapinduzi kimetaka kutumia madaraka na wingi wake kufanya kile ambacho hakikuwa na hakijawahi kuwa ndani ya ahadi zake. Kimetaka kufanya kitu ambacho hakikupewa ridhaa ya wananchi kukifanya. Sote tunakumbuka vizuri kuwa kampeni nzima ya uchaguzi wa mwaka jana kwa upande wa CCM haikuhusiana KABISA na suala la Katiba Mpya. Katiba Mpya haijawahi kuwa sehemu ya Ilani, ahadi au mipango ya Chama cha Mapinduzi kabla ya Disemba 31, 2010.

Ni uamuzi wa kudandia tena siyo kudandia tu bali kudandia na kushupalia. Leo wanadai kuwa ajenda ya Katiba Mpya ni yao. Lakini wanafanya hivyo wakikataa kabisa kukiri wala kutambua kuwa ajenda hiyo ilikuwa ni ya upinzani kwa miaka ishirini sasa tangu lile kongamano lilillozaa vyama vya upinzani nchini.

Ajenda ya Katiba Mpya imekuwa ni moyo udundao katika mioyo ya wapinzani nchini. Tangu mwanzo ilitambulikana kabisa kuwa mabadiliko ya kweli ya kitaifa hayawezi kutokea kwa kubadili watu tu, kubadili sera tu hata kubadili vyama ilitambulikana kabisa kuwa ni lazima kugusa Kitabu chetu Kitakatifu cha watu wa dini zote ambacho watunzi wake ni sisi wenyewe! Hatuwezi kubadilisha Biblia au Qurani lakini Katiba ni kitu pekee kitukufu ambacho kinatoka kwetu na hicho pekee kinatufunga sote sawa na hivyo kinaweza kubadilishwa na sisi wenyewe tu. Ajenda hii ya Katiba Mpya haiwezi leo kuwa ni ajenda ya CCM na wengine wanakaribishwa kama watoto wasio na kwao! Leo hii tumewaona wabunge wa CCM wakizungumza kwa jazba kana kwamba waliahidi hata mmoja wao kuwa wanataka Katiba Mpya.

Siyo Komba kwa kuimba wala Wasira kwa hasira aliyesimama mwaka jana kutaka Katiba Mpya ndani ya CCM. NONE. Leo wana ujasiri wa kubeza, kukebehi na hata kupiga mkwara wale wanaotaka katiba mpya kwa mfumo ulio wazi, wenye kuweka msingi juu ya wananchi siyo wabunge au Ikulu peke yake! Leo hii watu hawa wana ujasiri wa ulevi wa madaraka kwamba wako tayari kuamuru moto unye kama vile ulivyoteremka kule Sodoma na Gomora kisa tu tumewamua kuwageukia na kuwatazama! Na wapo watu wanaomini kabisa ati ajenda hii inaweza kuongozwa na CCM kwa vile tu CCM iko madarakani! Yaani, watu ambao juzi tu hawakuwa na wazo la Katiba mpya tena wakatubeza, na kutukebehi huku wakishindana kugongana wenyewe kwa maneno wanaweza kuandika mswada wa kusimamia uandishi wa Katiba tukaubali tu kwa vigelegele, ngoma na chereko chereko za vifijo.

Ngoja niliseme hili vizuri tu na kwa uwazi Ee Mungu nisaidie - maana tunazunguka mno - CCM haina uhalali wa madaraka ya kusimamia mchakato wa Katiba Mpya. Inaweza kushirikiana na wengine, inaweza kuzungumza na wengine, lakini yenywe peke yake haina hoja, uwezo, wala mandate (ridhaa) ya kufanya hivyo. Haimo kwenye ajenda yao, na Kikwete alipoamua kufanya hivyo mwishoni mwaka jana hakukuwa na kikao chochote cha Chama cha Mapinduzi ambacho kina madaraka ya kubadilisha sera za CCM. Hakukuwepo na kikao cha Halmashauri Kuu wala Mkutano Mkuu kilichofikia uamuzi wa kuandika Katiba Mpya. Huu ulikuwa ni uamuzi wa Ikulu na Ikulu peke na matokeo yake mswada mzima umezunguka Ikulu!

Wabunge wake hawakutakiwa hata kutoa maoni juu ya Katiba Mpya. Wangeweza kufanya hivyo tu kwanza kwa kukubali kuwa hoja hii ilikuwa inatoka nje yao (kwa wapenzi na wanaharakati) na kuwa kutokana na kutambua huko mchakato mzima kuanzia Alfa yake hadi Omega yake ungehakikisha kuwa watu wote wanashirikishwa siyo wanaburuzwa kwa mikwara ya kitoto na kejeli zisizo na kichwa wala miguu.

Kikwete sasa ametegwa. Kitendawili hiki ni yeye peke yake anatakiwa kukitegua. Alikipiga mwenyewe kwenye hotuba yake ya Disemba 31, 2010 alipotangaza na kutushtua kuwa hatimaye ameona mwanga na nuru ya ajabu ikimzukia na kuwa sasa serikali yake imekubali hoja ya Katiba Mpya . Jambo hili wengine tulilipokea kwa tahadhari tukihofia kile kinachotokea sasa. Tulihofia kuwa kwa vile hoja hii imechukuliwa na Ikulu (Kikwete) basi mchakato mzima utazunguka Ikulu na hivyo ndivyo ilivyokuwa na hapa ndipo kiini cha mgogoro wa sasa kilipo.

Wanaharakati na wanamageuzi nchini, wanayo haki ya kupinga, kukataa na kudhihaki mfumo ambao unapendekezwa na CCM na serikali yake ambao umepuuzia kwa makusudi au kwa sababu ya vimulimuli vya madaraka hoja zote tulizozitoa mwezi Machi. Watanzania ambao wamekuwa wakipigania mabadiliko ya Katiba kuanzia 1992 wanayo haki kabisa siyo tu ya kutoka ukumbini hata kusimama na kuanzisha mwamko wa kupinga kubambikiziwa Katiba Mpya kwa sababu tu watu wana madaraka. Kikwete asaidie kukitegua kitendawili hiki vinginevyo ni yeye ambaye atajiikuta anabeba lawama.

Ndugu zangu, kama sisi sote tutaweka miguu chini na kusema hatusogei na kuamua kugoma tulipo tutalazimishwa kuzungumza na kukaa pamoja wakati damu imemwagika. Hivi kwanini leo Kenya hawapigani mapanga? kwanini leo Zanzibar kuna muafaka, kwanini Zimbabwe kumetulia zaidi kuliko ilivyokuwa miaka michache iliyopita? Ni kwa sababu walifikia kwenye kilele cha kushindwa kuvumiliana. Pande mbili za hizo sehemu zote ziliweka miguu chini na kila mmoja aking'ang'ania upande wake na kukataa kuzungumza na mwingine wala kukubali kwamba yule mwingine yupo. Tangu uchaguzi mkuu wa mwaka jana nimetoa ombi wazi la kusema viongozi wetu wa kisiasa nchini wakae pamoja kuzungumza na siyo kuzungumza tu lakini pia kuwa tayari kukubali upande wa yule mwingine.

Kinachonisikitisha ni kuwa hadi hivi sasa inaonekana watu hawataki kukubali upande wa yule mwingine isipokuwa kwa lazima. "Kubalini msipokubali dola itumike!" wanasema waliolewa ugimbi ule wenye povu la madaraka. Wengine wanasema "msipokubali tutaandamana hadi msitawale" na wengine wanasema "mkiandamana tutawatia pingu hadi mkome" na wengine wanajibu "hamna pingu za kutosha wala magereza ya kufunga fikra". Matokeo yake - watalazimishwa kukaa chini na kuzungumza siku ile tutakapoamka na kusikia watu 50 wameuawa katika siasa! Mtasema tunachuria lakini ndivyo ilivyo mahali pote duniani!

Kikwete tegua kitendawili.

1. Usikubali mswada huu kama ulivyo. Hata wabunge wako waupitishe kwa mbwembwe. Upande wapili hautakubali. Na hamna namna ya kuwalazimisha watu milioni mbili kuukabali. Assadi hadi leo kashindwa anaua watu wake kila siku na bado wanasimama kumpinga. Risasi hazipo za kutosha. Bahati mbaya machozi hayana kikomo... Mkisema kuwa mtaendelea na mchakato na yeyote atakayepinga "atakiona cha moto" well.. mtakuwa mmetengeneza kundi kubwa la wanaowapinga na uzoefu unaonesha kuwa Watanzania nao ni wanadamu wakivuka mstari wa 'sina cha kupoteza isipokuwa utu wangu' tutalia na kusaga meno.

2. Pande mbili zikae chini kuzungumza na katika hili ni utayari wa Rais unasubiriwa. Pamoja na matokeo yale ya uchaguzi mwaka jana nilisema kaa chini na Dr. Slaa mzungumze. Nilimuuliza Dr. Slaa swali hili katika mahojiano na alisema yuko tayari wakati wowote kufanya hivyo. Lakini inaonekana kuna watu hawataki. Na hawa wasiotaka wanafanya hivyo labda kwa hofu kuwa ukikubali kuzungumza na Slaa (nyinyi wawili) basi utakuwa umempa ujiko au Kamati Kuu ya CCM na ile ya CDM vikikaa pamoja itakuwa mmeinua CDM. Well, je ni baya kiasi hicho? Kwamba mje kulazimishwa kukaa pamoja wakati miji inaungua, watu wanakimbiana na kukimbizana na polisi wametanda kila sehemu?

Kikwete tegua. Kitendawili hiki ni cha kwako, hakuna wa kukusaidia. Ulikianzisha mwenyewe na kwa namna nakuonea huruma kwa sababu historia inaweza ikakusamehe kwa mengi sana lakini hili la Katiba Mpya likivurundwa sidhani kama jina lako katika historia litakumbukwa kwa haiba nzuri hivyo. Lincoln anakumbukwa kwa mengi lakini la kutangaza emancipation ya watumwa kumemuweka kwenye level nyingine kabisa. Naamini jinsi utakavyosimamia mchakato wa Katiba Mpya bila kuonekana umeulazimisha ndivyo historia itakavyokukumbuka. Kwanini tufike huko kama tunaweza kuepuka kwa kukaa pamoja katika hali ya amani?

Kitendawili...
MMM

Asante sana kwa hii hoja. Nasubiri mweshimiwa atu tegulie hiki kitendawili.
If he will that is coz we all know him by now. He might just ignore everything.
 
Back
Top Bottom