Kitendawili cha Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania...

Katika wote hao wanaohangaika na pilika pilika za kutaka Urais mimi sioni candidate hata mmoja anayetufaa....
 
Kitendawili = Tega. Jee, unamjuwa Rais wa awamu ya Tano?

Kuna wengi sana leo hii wameshaamini kuwa fulani au fulani au fulani ndiyo atakuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya tano. Lakini ukweli ni kuwa bado ni kitendawili.

Mimi nnasema, mbio za sakafuni huishia ukingoni, Rais ajae hajajitambulisha wala hajatajwa bado, ingawa wapo wanaojuwa kitendawili hiki jibu lake ni nini lakini sidhani kama ni wengi.

Kuna wengi sana wanadhani kuwa Lowasa atakuwa Rais ajae, mimi nnasema, ng'oo! Lowasa hatakuwa Rais, na msije kushangaa Lowasa akijitokeza kumtangaza huyo Rais ajae na akawataka wote wanaomuunga mkono yeye basi wampigie kura huyo Rais wetu ajae. Tena nnahisi moja kati ya sababu zake (za kutogombea yeye Lowasa) itakuwa ya Kiafya. Ukiyapenda, haya, usipoyapenda, haya. Huwa sikisii.

Jee, unaweza kujaribu kumfahamu ni nani? Sitegui kitendawili kwa kwa sasa kwa sababu za kiufundi na kitakuwa si kitendawili tena, ila awezae kukiteguwa ajaribu, wale ambao wanadhani kuwa wana jibu la kitendawili hiki ukumbi ni wenu, jaribuni kukitegua:
Mbona hicho tusha kitegua siku nyingi sana.
Kama si wewe basi nahama Tanzania, una sifa zote hasa ya kijinsia.
 
well huu ni ugonjwa mbaya sana kwasabb hautibiki lkn pia tusimsemee sana manake nimeona kama hizi hbr nyinbgi zinatoka mitandaoni tuu yeye mwenyewe hajasema kitu.

atembelee Mayo Clinic nafkiri nio neurosurgeon wa kwanza kwasasa duniani kote wanaweza kupunguza degree za symptoms kama ziko critical.
Mungu amponye namuombea nafuuu ya haraka zaidi

Tunamuombea Mwenyeezi Mungu amponye na amsitiri yeye nasi pia. Amin.
 
Naam, na wewe unakubali hilo, au unakataa?
Niweke wazi, swala la Lowasa kugombee au kutogombee huko ccm halinihusu kabisa. Wana taratibu zao za kuwapata wagombea wao, so far, Lowasa ameonekana kukubalika sana ndani ya chama chake. Ninachopinga ni hila zinazotaka kutumiwa kumzuia kugombea kama hiyo unayoleta ya afya. Waacheni wanachama waamue, aletwe ulingoni wazalendo tumchinjie mbali.
 
Mbona hicho tusha kitegua siku nyingi sana.
Kama si wewe basi nahama Tanzania, una sifa zote hasa ya kijinsia.

Acha utani wewe...Nchi ya nani iongozwe na huyu Jihadist?

Kwanza hana sifa yoyote kwa kuleta thread kwa kuongozwa na hisia.

Huyu hater wa Nyerere kamwe hawezi kuongoza nchi hii.....No matter ni nani yeye
 
Tatizo wengi mnawaza kiCCM CCM tu. Go beyond CCM and tell us your proposal together with reasons au mtoa uzi unataka watu wapige ramli?
 
Kitendawili = Tega. Jee, unamjuwa Rais wa awamu ya Tano?

Kuna wengi sana leo hii wameshaamini kuwa fulani au fulani au fulani ndiyo atakuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya tano. Lakini ukweli ni kuwa bado ni kitendawili.

Mimi nnasema, mbio za sakafuni huishia ukingoni, Rais ajae hajajitambulisha wala hajatajwa bado, ingawa wapo wanaojuwa kitendawili hiki jibu lake ni nini lakini sidhani kama ni wengi.

Kuna wengi sana wanadhani kuwa Lowasa atakuwa Rais ajae, mimi nnasema, ng'oo! Lowasa hatakuwa Rais, na msije kushangaa Lowasa akijitokeza kumtangaza huyo Rais ajae na akawataka wote wanaomuunga mkono yeye basi wampigie kura huyo Rais wetu ajae. Tena nnahisi moja kati ya sababu zake (za kutogombea yeye Lowasa) itakuwa ya Kiafya. Ukiyapenda, haya, usipoyapenda, haya. Huwa sikisii.

Jee, unaweza kujaribu kumfahamu ni nani? Sitegui kitendawili kwa kwa sasa kwa sababu za kiufundi na kitakuwa si kitendawili tena, ila awezae kukiteguwa ajaribu, wale ambao wanadhani kuwa wana jibu la kitendawili hiki ukumbi ni wenu, jaribuni kukitegua:

Mama Faiza usiseme "Raisi wa Awamu ya Tano" bali "Mgombea Urais wa CCM wa Awamu ya Tano"! Siku zimebaki chache ila bado upinzani ukijipanga vizuri wana nafasi kubwa sana ya kushinda nafasi ya "Uraisi"! Na kama ndio hivyo jibu la Kitendawili chako ni ABDUL RAHMAN KINANA! Mizunguko anayofanya sio ya bure na pia kauli aliyoitoa Monduli kwa Lowassa ilikuwa na malengo maalum!
 
Kitendawili hujajaribu basi hata kukijibu? Usiogope, jaribu.
Tatizo ni kwamba, sisi wanachi kazi yetu sio kupendekeza nani agombee urais na nani asigombee, ila anapojitokeza katiba imeturuhusu kumchagua kupitia mchakato wa kura. Kwa muktadha huo, hiki kinabaki kua kitendawili kwa sababu hatujui nani na nani wana nia ya kugombea urais.

Naweza kuuliza kwanini umemtaja Lowasa peke yake licha ya kuwepo watu wengi walio onyesha nia ya kugombea urais? Ni katika kuboresha hoja tu. Shukran
 
Nijuavyo mimi kitendawili huwa ni fumbo linaloelekea kwenye ukweli...

Mf. Hausimami wala hausimiki Mkufu

Sasa wewe unatuletea kitendawili Hewa tukitegueje bibie..? Wewe ungechora ramani kuelekea kwenye ukweli then utachie sisi kutoa jibu. Ulichokifanya ni kanakwamba ulikuwa huna kazi ya kufanya ukaamua kujifurahisha tu hapa jukwani.

Anyway haki ni yako kuanzisha thread na hulipii kodi yoyote kwa kufanya hivyo zaidi ya kuteketea kwa Mb ambazo nazo ni zako mwenyewe.!!!

Asante kwa kuanzisha thread.

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom