Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Yawezekana watu wengi wanashangaa kwa nini hali imeendelea kuwa shwari toka Mh. Tundu Lissu atue nchini. Binafsi nawapongeza Watanzania wenzangu, asanteni Watanzania popote mlipo.
Watanzania kwa mamia na maelfu wameweza kujitokeza kwa wingi na kuandamana kwa amani bila misukosuko yoyote kutoka kwenye chombo chenye jukumu la kulinda amani, asanteni Jeshi la Polisi.
Kwa sasa tungetakiwa kutafakari polisi wetu kila mara kuzuia mikusanyiko huru ya wananchi inatokana na hofu gani? Hiyo hofu ya polisi kuzuia maandamano huru ya wananchi inatokana na nini?
Nina hakika kama polisi wetu wangeingilia hii mikusanyiko tuliyoishuhudia kama kawaida yao, wananchi wengi wasio na hatia wangekuwa vilema wakiuguza majeraha yaliyotokana na vipigo kutoka jeshi hilo.
Je, kama Watanzania tumejifunza chochote kutokana na hali hii? Binafsi naadhani jibu limepatikana...
Kilichodhihirika wazi ni kwamba polisi wetu badala ya kutekeleza jukumu lao kulinda amani wanatumika na chama tawala CCM kuvuruga amani kama kigezo cha kuwanyima wapinzani uhuru wao wa kikatiba.
Hakika adui nambari wani wa taifa hili ni CCM!
...