Kitendawili cha mji wa arusha: Naomba mchango! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitendawili cha mji wa arusha: Naomba mchango!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Nyumbu-, Jul 29, 2009.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  ARUSHA: A HOME FOR NO BODY?
  Hi Friends,
  Naomba niulize Swali: Hivi Arusha kuna nini?
  Huu ni mji wa ajabu sana, kwani inaelekea kila uongozi serikalini ukitaka kula basi ni Arusha. Hivyo wakurugenzi wengi hupangwa kwa ajili ya kufanikisha hilo (mtizamo wangu). Haingii akilini , kwa mji wenye vivutio vingi vya utalii kama Arusha kuwa katika hali kama ilivyo. Ni mchafu, hauna barabara (zaidi ni ile moja tu iliyoachwa na wakoloni), na hakuna juhudi zozote za kuundeleza.
  Kila kitu ni ghali, si kwa sababu panatakiwa hivyo, ila ni kwa mji kukosa miundo mbinu , mipango na ulafi uliokithiri. Wabunge na viongozi wa siasa ni wale wale , au walio na mahusiano yaleyale.Ili kudhibiti mabadiliko ya uongozi, huwa wanajitahidi kutoandikisha wanachama wapya wa CCM bila kujua kama watawasaidia au la. Hivyo, mji kama huu ambao una wamasai wengi wanaoheshimu maboma yao, ukidhibiti wanachama walio nje ya zile Boma zinazokupenda, umefanikiwa kupita ngwe nyingine , kiasi kwamba mtandao wao huwezi kuuingilia kamwe. CCM inabidi itafakari haya. Hii ndio moja ya siri ya jeuri za kina Mrema. Wana jeuri isiyo kifani.
  Unashangaa mji kama huu hauna viwanja vilivyopimwa zaidi ya Njiro na Ngaramtoni. Na hata vilivyopimwa havigawiwi kwa wananchi, bali viongozi hugawana wenyewe kwa wenyewe wakitumia majina ya bandia ili kuonekana kama vimegawiwa wananchi. Matokeo yake, hawaviendelezi, bali husubiri mtu anayehitaji kujenga ili wamuuzie kwa bei ya kuruka. Na hata kuuza kwenyewe ni mpaka huyo aliyehodhi atake, kwani hawauzi mpaka awe na shida!
  Matokeo yake, viwanja hivyo hununuliwa na watu wenye pesa tu, kiasi kwamba eneo la Njiro linaitwa eneo la matajiri wakati si maana yake. Kwanini kuitwe kwa matajiri wakati lengo ilikuwa wanachi wauziwe? Inaingiaje akilini hata raisi wa nchi anathubutu kusema Njiro ni eneo la matajiri, wakati anajua halikutakiwa liwe hivyo? Au kwa vile nyumba nyingi ni za mawaziri na maktibu wa wizara? Nini maana ya yote haya? Mbona miji mingine hupima viwanja tena huvitangaza ili watu wapeleke maombi, lakini si kwa Arusha?
  Matokeo yake ni watu kutafuta viwanja visivyo pimwa na kujenga holela , maana serikari inawapimia viwanja matajiri tu. Hivi kweli tumefikia hapo?
  Mpaka Arusaha inanyimwa hadhi ya jiji ni kwa sabau ya huo ubovu na kukosekana kwa miundo mbinu. Na tatizo moja ni kwa sabau ya Jumuiya y Afrika Mashariki.
  Kila bajeti ikija, watu hupiga dana dana, wakigawana hizo pesa, kwan i wanategemea EAC itatoa pesa siku yoyote ili wafiche maovu yao huko. Ni jambo la aibu sana.
  Naomba mnisaidei: Nini tatizo la Arusha?
  Ina kuwaje mji mdogo kama huu maji hayatoshelezi wakati kuna maji mengi mno mlima Meru?. Inaingiaje akilini sehemu zingine zinapata maji kila siku , lakini sehemu zingine mgawo mara moja kwa wiki au mwezi? Ni vigezo gani hutumika? Ili watu wakatoe pesa idara ya maji wachimbiwe visima? Hivi nini kinaendelea hapo.
  Tanesco -Arusha Bomu, Maji Bomu, Halmashauri Bomu, kweli? Hivi Kenya wangepewa Kisumu iwe ndio EAC ingezembea kiasi hiki? Mji wa kimataifa , uongozi wa kihuni.
  No, Let us say NO!!!!
   
 2. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Nyumbu inaonekana umetoka Arusha siku nyingi au hujawahi ishi bali unaisikia Arusha tu.Mimi Arusha nimekaa na nimeweka makazi zaidi ya miaka 15 sasa. Dar nimekaa na nimefanya kazi tena mwishoni mwa 2007 ndo nimetoka Dar.Kwa ufupi madai yako kuhusu Arusha yamekuwa makali mno kuliko hali halisi yenyewe. Arusha kuna matatizo lakini kwa kukusaidia tatizo kubwa la Arusha siyo maji wala umeme wala viwanja bali ni miundombinu ya barabara tu. ukweli ni kwamba barabara sio mbovu bali ziko chache ukilinganisha na magari yanayotumia barabara. Barabara za kuingia mjini ni mbili tu yaani ile ya old Arusha road kuanzia pale impala hotel hadi clock tower na ile ya Arusha-Moshi au Nairobi road.

  Problem nyingine kubwa ya Arusha ni uongozi haswa ule wa wawakilishi wa wananchi yaani madiwani na wabunge. Kwa ufupi hii jamii ya wamasai na waarusha hawana kabisa ile spirit ya kuwasaidia wenzao kama zilivyo jamii nyingine za watanzania. Angalia Lowassa hakuwasaidia kabisa wamasai bali aliwanyanganya ardhi na kuwatumia kama daraja la yeye kuwa na hali nzuri.Kuna Waarusha na wamasai wachache mno ambao wana maono ya kuwainua wenzao. Mji wa arusha unajengeka kwa kasi sana lakini investors wakubwa ni Wachagga na Wahindi. Vijana wengi wa Kiarusha huwa wanavizia na kuomba wazazi wao wafariki ili wauze viwanja na kutanua kwenye kumbi za starehe kama Triple A na Mawingu.

  Lakin Arusha kama mji bado ni msafi kuliko Dar na hauna matatizo mengi ya huduma za jamii kama Dar.Mji unapanuka kwa kasi na unaweza kununua kiwanja popote kama una pesa zinazofikia bei ya kiwanja. Mimi kwa miaka niliyokaa hapa nimejenga vizuri ni na shamba la eka 5 na viwanja vitatu vyote nimenunua kwa sababu mimi hapa nimekuja kutoka mkoa jirani.

  Matatizo yaliyoko Arusha ni ya kwaida kama yaliyoko Dar, mwanza, tanga na kwingineko. bei za vitu vya madukani kama nguo na vifaa vya elekronics ndo bei iko juu lakini si sana. price margin kati ya vitu ya dar na arusha kwa vitu vingi haizidi 5000. Nyumba pia ni ghali lakini za kiwango cha kati ila nyumba ikishakuwa na rooms 3 na sebule na garage bei zake zinakuwa ndogo kuliko Dar kwani arusha haina wapangaji wengi wa kiwango hicho.

  Kwa hiyo nyumbu kama unajambo lingine kuhusu arusha uliza tukufafanulie.
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,118
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Naomba thread ihame!!!
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nakuiba yaani kuna sehemu wanasubua kweli hasa maeneo ya Ilbolu
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Sii kweli hata kidogo. Inaonekana aither umetokea Manispaa, Tanesco, au Maji.

  Mimi nina makazi Arusha na Dar pia. Mji wa Arusha ni mdogo ukilinganisha na Kinondoni kwa mfano. Lakini ni mchafu kupindukia . Hebu anzia Shoprite kuelekea AIR port uone sehemu ya Ngarenanaro ambayo iko mjini kabisa ilivyokaa. Haifai hata kidogo ,then ndio njia wanapita wakuu wote na watalii pia. AIBU

  Kuna hao AUWSA ambao hawafanyi lolote kuboresha huduma ya maji mjini. Huko milimani kuna vyanzo vingi sana vya maji ambapo Arusha ingekuwa mfano wa huduma bora ya maji kati ya mikoa yote nchini. Lakini wapi bwana. La ajabu zaidi ni pale wanapoingia garama ya kuweka bomba jipya kama walivyofanya eneo la Moshono -Suye halafu maji yote wanayadirect KARAMA Logde kiasi kwamba wananchi wanapata maji siku moja au mbili tu wiki.Utashangaa Wazungu wanavyowaifluence Wabongo wote waliopo kwenye hiyo Taasisi ikiongozwa na Munisi.

  Hiyo Tanesco ndio usiseme. Toka mwezi wa 5 hadi sasa Arusha kuna mgao wa umeme. Mbaya zaidi wanapiga kimya kimya.

  Hata baada ya kuingiza LUKU ambazo wananchi walizipenda badala ya zile walizokuwa wanabambikiza bili, inakuwa taabu kufungiwa .Ni hadi rushwa kupewa luku. Si aibu hii jamani?

  Hiyo Manispaa haijawahi kuwa na uongozi thabiti wenye kuona mambo kwa mapana yake. Mara alikuja Job Laizer ambaye ni Mwarusha aliyewekwa na Lowasa akavurunda vurunda hapo weeee akaishia kustaafu. Aliyepo sasa naye hawezi kuwa na jipya maana alikuwa hapo hapo kama Afisa utawala. The same circle. Sasa usiombe uende huko Mipango Miji na Ardhi usikie akina mama wa mipango miji wanavyoargue . Huwezi kuamini waliwahi kufika hata darasa la tano. Aibu tupu.

  Mimi nakubaliana na mleta hoja kwamba Ar . ni mji uliooza .Bora Tanga na Moshi. Uongozi ni wa kuunga unga tu kwa maslahi ya wakuu. Barabara ni mbovu na ni moja tu kuingia na kutoka hasa Njiro -Town. Beside inahost International Institutions nyingi tu ambao wakikaa wanasema kweli Watz hawana akili hata kidogo.

  Habari ya viwanja Arusha ni muziki mzito. Kwanza hawapimi, na wakipima kupata ni mbinde. Watu hujinunulia viwanja toka kwa wenyeji na hujijengea bila utaratibu maalumu maaa kama nilivyosema hapo juu mipango miji Arusha literary hawapo.
  Matokeo yake ni uharibifu wa maeneo na kuendea kuongeza squaters tu japo za nyumba nzuri. By the way kama hujui Arusha ndio mji unaoongoza kwa squater Tanzania Nzima. Unga LTD , Matejo, Kambi ya Fisi, Kijenge, sehemu za Mbauda to mention just a few.

  Ukiacha tu hali ya hewa na kamzunguko ka hela Arusha is the worst town in in the real sense of towns per se.
   
 6. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sasa naona tunapata uwiano mzuri wa hali ilivyo AR.
   
 7. Mr. Miela

  Mr. Miela JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2009
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kweli arusha ilistahili kupewa hadhi ya zizi na si jiji
   
Loading...