KITENDAWILI CHA MAENDELEO (MAGUFULI KAFELI)

guzman_

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,063
2,000
Ukweli Mchungu.
Hata tujenge madaraja kila mto, tujenge barabara za lami mpaka vijijini, tununue ndege kila halmashauri yake n.k hakuna maendeleo ya maana tutafikia bila kuwa na ELIMU BORA inayoandaa nguvu kazi yenye tija katika tafiti, technologia, afya n.k. Kwa mantiki hio elimu bure haina maana kama baada ya miaka takribani 60 ya uhuru kuna shule wanasomea nje, hawana madawati, hawana vitabu, hawana maabara, hawana waalimu wenye ujuzi na motisha ya kuipenda kazi na matatizo lukuki.
Kimsingi shule za kata zinazalisha ujuzi unaofanana kwa 70% yaani ujuzi wa kuendesha bodaboda. Wito wangu serikali irudi tena ifanyie mabadiliko makubwa sekta ya elimu.
 

guzman_

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,063
2,000
Maendeleo yamebaki kwenye karatasi tu.


Maendeleo hayawezi kuja yakitaka ni lazima yafanyiwe mchakato. Vietnam jana tu walikuwa kwenye vita vikali ila kwa muda mchache tu washatuacha mbali sana. Siri kubwa walionayo ni uwekezaji kwa watu kupitia elimu na utumiaji maliasili vizuri. Sasa sisi wanafunzi wanakaa mchangani wanasoma halafu utegemee huyo ndo aje kuwa daktari bingwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom