Kitanzi Cha vitambulisho vya ujasiliamali

Witmak255

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2019
Posts
3,264
Reaction score
5,450
Kutoka kwa kada mtiifu was ccm
Magoiga SN.

Hivi ni kweli tunataka mpaka wanaookota makopo wawe na vitambulisho vya machinga??

Wiki kadhaa zilizopita niliandika kuhusu utaratibu usiokuwa wazi unaotumika kugawa vitambulisho vya wamachinga ktk baadhi ya maeneo nchini, katika andiko hilo niliandika kuhusu Mbarali baada ya kusikia kuwa vibarua wa mashamba ya mpunga, bar maidss, waendesha power tillers nk wanalazimishwa kuwa na vitambulisho hivyo.

Hoja yangu ilikuwa wazi kuhusu dhamira ya vitambulisho husika na aina ya watu wanaolazimishwa kuwa na hivyo vitambulisho, mpaka leo siamini kama mhudumu wa baa ni mtu sahihi kupewa hiki kitambulisho unless kama kuna lengo jingine ambalo halifahamiki kwa umma.

Leo nimesoma habari inayosema kuwa "WAOKOTA MAKOPO KUPEWA VITAMBULISHO RUVUMA'

Kwa mujibu wa habari hiyo, inasema mkuu wa mkoa wa Ruvuma amenukuliwa akisema kuwa, “Tunawagawia wote…mpaka wale wanaookota makopo barabarani,” Kwa mujibu wa taarifa hiyo, RC wa Ruvuma, Ndugu Christina Mndeme akizitaka Halmashauri zote za Mkoani humo kuhakikisha zina gawa vitambulisho kwa watu wote wenye sifa kuanzia wenye mtaji wa chini ya million nne, wakiwemo wakulima na waokota makopo barabarani.

Naomba nirudie kusema kuwa, ikitokea hivi vitambulisho vikagawiwa hovyo bila kufuata lengo lake mahususi kama ilivyowahi kutangazwa na Mh Rais, ipo siku hivi vitambulisho vitageuka kuwa kitanzi

Tena vitakuwa kitanzi kibaya sana maana sasa hivi tunataka kuwalazimisha hata wasiohusika wawe sehemu ya hivi vitambulisho
 
ukizusha jua kisushiwa ww.imelipwa bei gani kuongea uongo dhidi ya taratibu za mh.rais
Kwani we una tatizo kichwani? Jinsia yako ni ipi? Mbona imekaa ki KE kwani lazima uchangie mada? Jaribu kujenga hoja kama kiumbe hai basi
 
ww mwanamke achana na k ww fanya yako hapa kamfundishe mmeo sio mm nitakupiga mimba faster.

ficha ujinga wako hujaja hapa kufundisha ebohh
Kumbe una mimba changa sikulijua hilo pole sana
 
hakuna shida.wajasiriamali wanamppngeza jpm kwa wazo zuri la ujenzi wa taifa
Mpeni ushauri mzuri mh. Rais kama kweli mnampigania na mnampenda, muokota makopo barabarani ni mtu anayesaidia kuondoa takataka hatari za plastic barabarani, hivi wakiacha kuokota wataajiri waokota makopo?, hebu muwe mnatoa ushauri mzuri sio ushabiki usio na maana
 
Kwani we una tatizo kichwani? Jinsia yako ni ipi? Mbona imekaa ki KE kwani lazima uchangie mada? Jaribu kujenga hoja kama kiumbe hai basi
Huyo USSR achananaye, kila Uzi huwa anakoment PUMBA, sijui lengo lake lipi.
 
Nafikiri lengo kuu ni kukusanya mapato tu

In God we Trust
 
Jana nilikuwa sehemu fulani likapita gari linatangaza kuwahimiza wauza karanga,wachonga kucha,wauza supu wote kwenda kuchukua vitambulisho

In God we Trust
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…