KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 10,569
- 21,075
Nimeoa kwenye mkoa mmoja wa Kanda ya Kaskazini ambako huko kunatajwa na kuogopwa sana na watu wasio wa ukanda huo, kwani kunasifika kwa kuua mume akiwa na mafanikio.
Hii sio mara ya kwanza kuwatembelea wakwe zangu, na mara zote huwa naandaliwa chumba kizuri chenye kitanda kikubwa, rangi za kuta nyeupe na matandiko huwa ya rangi nzuri zilizotulia.
Sasa uchumi wangu umeongezeka sana, na Nina mafanikio sana kwenye uwekezaji wangu.
Wakwe wameniandalia chumba cha rangi ya zambarau, ambayo ni rangi ya msibani.
Mashuka na matandiko yenye rangi nyekundu, ambayo ni rangi inayoonyesha kumwagika kwa damu.
Pia kitanda nilichoandaliwa ni kidogo sana cha futi sita kwa mbili na nusu, utadhani kitanda cha kuoshea maiti.
Kwa kweli mapokezi haya yamenifikirisha sana, kuanzia Leo usiku nitaenda kulala Arusha, hawa wakwe nadhani wameona sasa wayatamatishe maisha yangu.
Wamenikosa