Kitanda chako na mke au mume Wako

Kitanda chako na mke au mume Wako

Habari MMU!!
Nina swali moja tu! Tuchukulie umeoa/kuolewa. Je, ni sahihi kutumia kitanda unachotumia na mke/mume wako pamoja na wageni endapo mwenza wako hayupo???
Kwa mfano tuseme wife/husband hayupo na umepata mgeni wa jinsia yako. Ni sahihi kulala naye kitanda kimoja unachotumia na mke/mume wako?

NB: Mgeni anaweza kuwa ndugu yako wa damu au swahiba wako wa karibu.
Tujadili!!!!!!!!

Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi, sio heshima wala adabu kumlaza mtu mwingine kwnye kitanda cha mume na mke hata kama una chumba kimoja
 
Nooooooo!
Chumba kile ni lazima kipewe heshima yake, haifai hata kupiga stori na mgeni ikiwa kuna sebule or chumba kingine!
Haifai kumpa mtu asiehusika mipangilio na hali ya chumba cha wakubwa!
Ni lazima kuekwe mikakati ya kuenclose siri za chumba!
Kwa mawazo yangu: kuhadithia tu chumba kikoje na mpangilio wake haifai!
Kuna baadhi ya me hujiona wako sahihi pale wanapolalama wake zao ni wachafu na kuelezea hata hali ya chumba chao
...
Kwa kufungia: hata chumba kimeremete kuliko almasi haipaswi kumuingiza mgeni, isipokuwa, hakuna sehemu nyengine!

nimekuelewa vizuri kabisa mkuu
 
Kwa kweli sio vema kushare kitanda chako na mume/mke na rafiki yako, kwanza chumbani kwako ni sawa na theater (chumba cha upasuaji) huwa hakiingiliki hovyo hovyo na watu ambao sio wahusika, chumba chako ni siri yako na mume/mke wako tu, kinawahusu nyie wawili tu hata housegirl haruhusiwi kuingia wala kufanya usafi huko, ni marufuku jamani. Pale ni chumba special cha operation ya wawili wapendanao. Kwa mimi naheshimu sana chumba changu na mpenzi wangu, no entry kwa yeyote.

umenena vyema sana Pendaneni!!!
 
Nooooooo!
Chumba kile ni lazima kipewe heshima yake, haifai hata kupiga stori na mgeni ikiwa kuna sebule or chumba kingine!
Haifai kumpa mtu asiehusika mipangilio na hali ya chumba cha wakubwa!
Ni lazima kuekwe mikakati ya kuenclose siri za chumba!
Kwa mawazo yangu: kuhadithia tu chumba kikoje na mpangilio wake haifai!
Kuna baadhi ya me hujiona wako sahihi pale wanapolalama wake zao ni wachafu na kuelezea hata hali ya chumba chao
...
Kwa kufungia: hata chumba kimeremete kuliko almasi haipaswi kumuingiza mgeni, isipokuwa, hakuna sehemu nyengine!

ikiwezekana kiwekwe kiashiria cha No Entry si ndio?
 
....madhali kitanda chenu kipo chumbani kwenu, #SiVizuri !

Binafsi, chumba changu na mke wangu napenda pawe ni #Mpaka (No Entry!) ila iwapo mamsap nae ndio asili ya kwao hapo mtihani!

Mwingine unamkuta kajilaza huku kavaa na nguo za mkeo na zinampendeza mashaallah kuliko mkeo... Haya, si mtihani huo chumbani kwako #RijAl !

#MosKwito !
 
Kwa kweli sio vema kushare kitanda chako na mume/mke na rafiki yako, kwanza chumbani kwako ni sawa na theater (chumba cha upasuaji) huwa hakiingiliki hovyo hovyo na watu ambao sio wahusika, chumba chako ni siri yako na mume/mke wako tu, kinawahusu nyie wawili tu hata housegirl haruhusiwi kuingia wala kufanya usafi huko, ni marufuku jamani. Pale ni chumba special cha operation ya wawili wapendanao. Kwa mimi naheshimu sana chumba changu na mpenzi wangu, no entry kwa yeyote.

Sawasawa kabisa, sijui AshaDii Nyamayao King'asti MwanajamiiOne nyumbakubwa Kaunga na watu wazima wengine watalitolea tamko gani jambo hili...

#MosKwito !
 
Last edited by a moderator:
Kama ni nyumba ya kupanga na una chumba kimoja tu, hakuna jinsi na hasa kama huyo mgeni ni ndugu yako au rafiki yako wa karibu akiwa wa jinsia moja na wewe unaweza lala nae chumbani kama mwenzi wako hayupo. Ila hakikisha yale mambo ya siri yenu na mkeo hayawi exposed kwa huyo mgeni. Ila kama una nyumba yenye zaidi ya chumba kimoja, basi si vema kutumia chumba chako na mkeo/mumeo kumleta huyo mgeni. Kama una huruma sana na unataka kumpa company huyo rafiki/ndugu yako mkalale nae chumba cha wageni au sebuleni. Vinginevy ni kujishushia heshima wewe mwenyewe na mwenzi wako pia.
 
safi kabisa. maneno yako yana reflect avatar yako. asante mkuu
 
Kama nyumba ni kubwa kuanzia vyumba viwili haitakiwi kabisa,kama nyumba ndogo siyo mbaya,jaman achen tu! Kuna ndugu wanakujaga bila taarifa no way inabid umpishe tu.
 
ujue wengine ukimpeleka chumba kingine anaona umemdhalilisha!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom