Kitanda cha mpangaji mwenzangu

Kitanda cha mpangaji mwenzangu

Mkuu Daudi1 silali mpaka nijue mwisho wa hili sekeseke.
 
Last edited by a moderator:
Halima wewe Unataka kuonja vyote loooh.

Mama Tina msala huo.
 
Haya tuendelee wapendwa ili tuone mtanange kati ya Mama Tina na Halima unaishia wapi
 
KITANDA CHA MPANGAJI MWENZANGU- 11

ILIPOISHIA:
Mama Tina hakukubali, akatoka nje na kumpigia simu Halima...
“Eti huyo mjomba‘ako amelazwa wodi gani na anaitwa nani? Nataka kumpa pole maana nimekuja kumwangalia baba Tina.”
JIACHIE MWENYEWE…“


Yupo hapohapo we ulizia tu, utampata.”
“Anaitwa nani?”
“Mh! Mzee Semsela.”

Basi, mama Tina akaingia kwenye woda ya kwanza waliolazwa wanaume…
“Jamani wagonjwa samahanini sana, eti kuna mgonjwa anaitwa mzee Samsela humu ndani?”
Wagonjwa wote na wanaowahudumia walibaki kimya, kila mmoja akitembeza macho kwa mwenzake kama kuna atakayesema yeye ndiye mzee Semsela.

Mbaya zaidi, karibu wagonjwa wote hakuna aliyekuwa na vigezo vya kuitwa mzee.
“Mama nadhani hakuna, si umeona mwenyewe?” mgonjwa mmoja ambaye ni msela tu alisema.
Mama Tina akaondoka, akaenda kwenye wodi aliyolazwa mume wake…

“Samahani wagonjwa jamani!” aliposema hivyo mama Tina akamtumbulia macho mume wake, akawatumbulia wagonjwa wengine ili kuona kama wamepokea samahani yake, akaendelea…
“Eti kuna mgonjwa anaitwa mzee Semsela humu wodini?”

Kulikiwa na wazee wengine wawili mbali na mume wake, baba Tina lakini hakuna aliyesema yeye ndiye mzee Semsela…

“Una nini wewe kwani?” mumewe alimuuliza.
“Halima alileta chakula hapa leo, akasema mjomba wake amelazwa, kisa ana presha, sasa namuuliza huyo mgonjwa wake amelazwa wodi gani nimjulie hali, akasema niulizie mzee Semsela…

“Kwani lazima umuone huyo mzee Semsela?”
“Si mjomba wa mpangaji mwenzangu jamani!”
“Sitaki hiyo tabia mama Tina.”

“Basi kama hutaki ina maana Halima alikuja kukuangalia wewe?”
“Mimi sijamwona.”
“Ulimwona, unanidanganya tu.”

“Mama Tina hebu rudi nyumbani tafadhali sana.”
“Oke, oke. Lakini Halima atakwenda kuniambia ukweli leo,” alisema kwa ukali mama Tina huku akiondoka kwa hasira.

Katika maisha yake ya kuwa na baba Tina hakuwahi kujisikia wivu kama siku hiyo, hasa akizingatia kwamba, kama kweli mumewe atakuwa anatembea na msichana huyo basi ndoa yake iko hatarini kwa mambo mawili. Kwanza, Halima ni mwanamke malaya tu, hivyo Ukimwi njenje.

Pili, licha ya umalaya wake, lakini pia ni msichana mzuri sana. Ana sifa zote za kumvutia mwanaume anayejua wanawake warembo.

Alipokwenda hospitali alipanda Bajaj lakini wakati anarudi, ili kumuwahi Halima aliamua kupanda bodaboda huku akimwambia dereva wake kwamba, kama hawezi kukimbiza amshushe apande bodaboda nyingine…

“Suka vipi, mbona kama unapangusa meza iliyomwagikiwa uji wa mtoto, nishuke nipande nyingine nini?”
“Anti inakimbia sema tu kwa vile una haraka sana ndiyo maana unadhani haikimbii.”
“Mimi najua pikipiki ikikimbia na ikitembea kama yako, hii unatakiwa uiingize kwenye msafara wa magari ya kusindikiza harusi za kifahari.

***
“
Haloo baba Tina,” Halima alipokea simu ya baba Tina ambaye alipiga mara baada ya mke wake kuondoka…
“Mwenzako alikuja hapa, amekwambia?”
“Kaniambia, nikamyeyusha.”

“Sasa anakuja huko, utajua cha kumwambia, sawa?”
“Wala usikonde. Ye anadhani mimi na wewe tunaweza kuwa wapenzi kweli?”
“Hapana.”

“Sasa? Mi nilichukulia ubinadamu tu, wewe ni mpangaji mwenzangu kwa hiyo natakiwa kukuonesha ubinadamu wangu hasa pale nilipogundua kwamba, aliyekusababishia matatizo hayo ni yeye.”
“Kweli kabisa Halima.”

“Sasa kwa nini yeye anataka kuchukulia jambo hili kama vita?”
“Hata mi sijui.”

“We Halima!” aliita mama Tina akiwa ameshafika.
“Abee…baba Tina mkeo ameshafika, ananiita nje,” Halima alisema kwa sauti ya chini huku akitoka chumbani kwake.
Halima alikata simu ya kuongea na baba Tina, akawa ameshafika kumsikiliza mama Tina…
 
KITANDA CHA MPANGAJI MWENZANGU- 12

ILIPOISHIA:

“We Halima!” aliita mama Tina akiwa ameshafika.
“Abee…baba Tina mkeo ameshafika, ananiita nje,” Halima alisema kwa sauti ya chini huku akitoka chumbani kwake.Halima alikata simu ya kuongea na baba Tina, akawa ameshafika kumsikiliza mama Tina…
JIACHIE MWENYEWE SASA…“


Halima ulifuata nini hospitali alikolazwa mume wangu?”
“Kumwangalia mjomba ‘angu mzee Semsela.”
“Kalazwa wodi gani?”

“Khaa! Sasa mama Tina kwani ilikuwa lazima ukamwangalie mpaka unanijia kwa hasira hivi?”
“We uliyekwenda kumpelekea chakula ni mume wangu, uongo?”
“Uongo.”
“Kweli.”

“We una ushahidi gani?” aliuliza Halima huku akionesha dalili zote kwamba liwalo na liwe tu kuliko kunyanyaswa na mwanamke
mwenzake.

Mama Tina huku akiwa amejishika kiuno sasa, alijibu…
“Nimeona mabaki ya chakula chini ya kitanda cha baba Tina wakati anasema hajala na wewe ndiye uliyetoka hapa na chakula
ukasema unampelekea mjomba ako ambaye hayupo pale Palestina Hospitali.”

“Hayo mabaki ni ya chakula gani?”
“We ulipeleka chakula gani?”
“Ugali wa muhogo na kisamvu.”
“Muongo mkubwa wewe, ulipeleka ndizi za kupika na nyama, bisha.”
“Nabisha.”

“Halima...Halima kuwa makini sana na mume wangu, nakwambia kweli. Nikigundua...”
“Mimi nimeshagundua vingapi?”
“Kama vipi?”

“Iko siku utavijua tu,” alisema Halima huku akizama ndani kwake.
Mama Tina aliondoka akiwa na hasira sana. alitamani sana kumvaa msichana huyo hasa alipogundua amekuwa akimfuatafuata sana na

kumtangaza kwa watu kwamba anatembea na Os Anjelus.
***
Baba Tina alitoka hospitali na siku hiyo alikuwa nyumbani. Mpaka hapo hakuwa amemwambia mke wake maneno aliyoambiwa na Halima
kuhusu mpangaji mgeni, Os Anjelus.

Halima alikuwa akitoka kwenda kwenye saluni yake, akamuona baba Tina...
“Shikamoo baba Tina.”
“Marhaba, mzima?”
“Mimi ni mzima. Haijambo familia yako?”
“Ipo sawa. Naona unakwenda kuwajibika sasa?”

“Hivi Halima, mume wangu amekuwa wa kumzoea siku hizi siyo?” mama Tina aliingilia kati huku akitoka nje. Halima hakumjibu
kitu zaidi ya kumtumbulia macho tu, naye akaondoka zake.

Alipofika saluni aliwaza sana kuhusu hali ya mama Tina kwa sasa, akajiuliza yeye na mama Tina nani anastahili kuwa mkali kwa
mwenzake?
“Dawa yako inachemka, iko siku nitashikana naye mbele ya mtoto wake, nitamchakaza ile sura anayoringia,” alisema moyoni
Halima.

Mara meseji iliingia kwenye simu yake kutoka kwa baba Tina...
“Samehe kwa yote yaliyotokea Halima, huyu mwanamke kachanganyikiwa.”
Halima hakuijibu mapema meseji hiyo, lakini ulipofika wakati wa kujibu alisema...
“Nadhani hujamwambia kama umepata habari analala na mpangaji mgeni ndiyo maana anatamba mbele yangu.”

“Halima, sijamwambia. Kwanza nataka nisaidie jambo moja tu, hakikisha unawafuatilia kwa karibu hata kukulipa nitakulipa
ilimradi niwanase.”

“Hilo dogo kwangu, nipe siku tatu.”
Halima aliona amepwa dili, kwake suala si kulipwa bali ni kuhakikisha anamchomoa mama Tina kwenye ndoa yake.

***
Siku ya pili, saa kumi na moja jioni, Halima alirudi nyumbani akiamini Os Anjelus naye atakuwa amerudi. Alijua lazima mama
Tina atataka kuonesha kumjua sana kijana huyo na kuingia kwake.

Baba Tina alikuwa kazini siku hiyo, mama Tina alikuwepo nyumbani, Os Anjelus aliingia muda aliofikia Halima na walisalimiana.
Kuna wakati mama Tina alitoka ndani kwake, akaenda kwa Os Anjelus na aliingia bila kubisha hodi akijua kama angefanya hivyo
Halima angesikia...

“Baby nimekumisi ile mbaya, please kama hutajali leo tutoke kabla mume wangu hajarudi, humu ndani kidudu mtu ameshaingia
hatuwezi kufaidi chochote,” mama Tina alimwambia Os Anjelus.
 
Back
Top Bottom