Kitambulisho kwenda Zanzibar

Kitambulisho kwenda Zanzibar

Mkuu sasa unaishije bila kitambulisho?
Kuna mdogo wangu mmoja alikua mgumu kama wewe juu ya kuwa na kitambulisho,siku moja yakamfika,akanipigia nimsaidie some amount,nikamrushia £350 kwa w.union,baada ya nusu saa nikampa MTCN No na Password nikamwambia nenda kachukue,kufika w.union anaambiwa lete kitambukisho cha mpiga kura,passport au driving licence,hakuwa nacho kati ya hivyo,akanipigia nikamwambia sina namna ya kukusaidia na wala siwezi kuivuta irudi ili nikutumie kwa mtu mwingine,nikamwambia wewe tafuta jitambulisho miongoni mwa hivyo kisha nenda kachukue pesa yako.Kwa bahati nzuri miezi miwili baadae kukawa na maboresho ya daftali la wapiga kura,akaenda kuchukua kitambulisho kisha akaenda kuvuta mpunga wake,ingawa cha moto akishakiona!
Ni sahihi sana mkuu.
Sidhani kwa mfano mikoa ya Kigoma, Katavi, Mwanza, Shinyanga na Tabora kwa wanaostahili kuwa na kitambulisho cha mpiga kura walizembea maana bila kitambulisho hupati tiketi ya treni.
 
Sio ujinga ni sahihi ki usalama, ili kukitokea ajali ni rahisi kugundua bado nani hajaokolewa na anatokea kata gani. Mbona hata kwenda mwanza au Safari yeyote kwa Ndege ni hivyo hivyo, yani lazima uwe na kitambulisho.
Unajaribu kutueleza kwamba ajali hutokea ukisafiri kwenda Zanzibar peke yake? Ukisafiri kwa mfano toka Dar kwenda Mwanza, huwezi kupata ajaili, ..na unahitaji hiyo barua ya serekali ya mtaa? ..ni wajibu wa chombo chochote kinachokusafirisha kuwa na taarifa zako muhimu, kwa madhumuni uliyoyataja!
 
Wewe unazungumzia nini au kitambulisho gani?
Mfano kitambulisho cha utaifa kinarekebishwa lini endapo kama nimehama mahali nilipojiandikishia? Vivyo hivyo kwa kile cha mpiga kura.
Je kitambulisho cha mtumishi kinaonesha makazi yake? Au hiki hakitakiwi!
Mkuu cheti cha kuzaliwa hakina sifa ya kuitwa kitambulisho.
That is my point!!
 
Unajaribu kutueleza kwamba ajali hutokea ukisafiri kwenda Zanzibar peke yake? Ukisafiri kwa mfano toka Dar kwenda Mwanza, huwezi kupata ajaili, ..na unahitaji hiyo barua ya serekali ya mtaa? ..ni wajibu wa chombo chochote kinachokusafirisha kuwa na taarifa zako muhimu, kwa madhumuni uliyoyataja!
Kwahiyo hapa unakataa au unaunga mkono?
 
Sisi watanzania tabia ya uongo hatuwezi kuacha.
Mtu kwao anajulikana kwa jina la John akienda kwingine anajulikana kwa jina la Juma, swala la kuweka utaratibu wa vitambulisho bandarini ni la msingi sana ili kupata majina halisi ya watu, tena ni vizuri utaratibu huu na mamlaka nyingine wauige ili kupunguza wimbi la watu ambao maiti zao hushindwa kutambulika na ndugu zao endapo ajali ikitokea
 
Wapige passport size afu waende kwa Uongozi wa mtaa au kijiji wapewe barua ya utambukisho. That's over Sir!
 
Back
Top Bottom