Kitambulisho kwenda Zanzibar

Kitambulisho kwenda Zanzibar

Kitambulisho ni document yenye kukutambulisha wewe, kutokana na usafiri wa ndege au meli hutumika sana kwa sababu zilizowekwa na mamlaka husika, kama Zanzibar watu wangekuwa wanakwenda kwa basi naona vitambulisho visingetumika. SUMATRA waliikazia nidhamu ya kuonyesha kitambulisho pindi unaposafiri kutokana na ajali za baharini zinapotokea inakuwa vigumu kutambua waliyopata ajali wakina nani ikiwa hawajaorodheshwa na kampuni husika, vile vile na kwa ajili ya usalama pia kujua nani kaenda Zanzibar na nani katoka Zanzibar kaenda Dar. Tujaribu kuheshimu taratibu zilizowekwa na mamlaka husika ni kwa ajili ya manufaa yetu.
Kwenye ajali.vitambulisho vinahusika vipi?kikubwa ni taarifa za abiria.kwani kitambulisho wana Baki nacho wao.?si naingia nacho kwenye boti.kitambulisho kitanisaidiaje kwenye ajali
 
Hivi huo ujinga wa kwenda Zanzibar na vitambulisho haujafutwa tu?
Huo sio ujinga bali ni moja kati ya measure zilizochukuliwa baada ya kutokea ajali mfululizo zilizopelekea mamia ya watu kufariki na wengine b8la kutambulika na ndugu zao, wameweka utaratibu huo ili kuwa na majina halisi ya watu wanaosafiri ili endapo ikitokezea ajali majina ya waliokuwemo kwenye boti yatangazwe ili ndugu zao waweze kuwatambua.

NB
Watu wengi walikuwa wakisafiri kwa kutumia majina feki
 
Kwenye ajali.vitambulisho vinahusika vipi?kikubwa ni taarifa za abiria.kwani kitambulisho wana Baki nacho wao.?si naingia nacho kwenye boti.kitambulisho kitanisaidiaje kwenye ajali
Wewe umapossfiri Mamlaka wanakuwa na manifest ya wasafiri wote, tena kwa majina halisi waliyochukua kwenye vitambulisho.
 
Kwa hyo nisipo kuwa na kitambulisho nitawaongopea jina langu?
Ndio. Ni wengi sana wameshafanya hivyo, mwisho wa siku inapotokea ajali maiti zao huwa zinakosa kutambuliwa na ndugu zao.
 
Ndio. Ni wengi sana wameshafanya hivyo, mwisho wa siku inapotokea ajali maiti zao huwa zinakosa kutambuliwa na ndugu zao.
Poa sio mbaya.Mimi kitambulisho sina.ntakwenda kupanda jahaz bagamoyo
 
Sio ujinga ni sahihi ki usalama, ili kukitokea ajali ni rahisi kugundua bado nani hajaokolewa na anatokea kata gani. Mbona hata kwenda mwanza au Safari yeyote kwa Ndege ni hivyo hivyo, yani lazima uwe na kitambulisho.
Watu wanakariri tu we subiri itafika kipindi na nadhani ni wakti sasa hata mabasi na treni zifanye utaratibu huo
 
Cheti cha kuzaliwa kinatosha.
Zanzibar kwasababu watalii ni wengi ndio maana wanatumia mfumo huo
Cheti cha kuzaliwa sii kitambulisho mkuu!!
Cheti cha kuzaliwa kinaweza kukutambulisha makazi yako?
Toa comment yenye kusaidia na usitoe yenye kupotosha.
Kwa mfano mimi nimezaliwa Mkoani Mveya na cheti changu kinaonesha hivyo,but naishi Dar na mimi asili yangu ni Mara,na Mbeya nilipozaliwa babangu alikua mtumishi serikalini,but 99% ya ndg zangu ni Musoma,jee ikitokea nimetumia cheti cha kuzaliwa na ajari imetokea nikafariki jee ntapelekwa Mbeya nilipozaliwa ili ndg zangu waje kunitambua?yani watokee Musoma?
 
Tatizo kama hauna si watakuzuia ndo sisi tunachopinga.ina maana kama hauna kitambulisho hauingii Zanzibar?
Kama huna zipo taratibu mbadala kupitia serikali yko ya mtaa!na usikariri kwenda Sanzibar hata aliyeko Zanzibar pia hatoki ila kwa utaratibu huo huo na hata nyumbani kwako unapoenda chumba cha watoto shart ujitambulishe japo kwa hodi na sauti huingii tu kwa kywa ni nyumba yako na ni watoto wako !
 
Kwenye ajali.vitambulisho vinahusika vipi?kikubwa ni taarifa za abiria.kwani kitambulisho wana Baki nacho wao.?si naingia nacho kwenye boti.kitambulisho kitanisaidiaje kwenye ajali
Kitambulisho chako kitasaidia kurecord taarifa zako(jina kamili,makazi yako au unapofanya kazi)hii ni faida kwako na ndg endopo imetokea ajari mkuu.
 
Kama huna zipo taratibu mbadala kupitia serikali yko ya mtaa!na usikariri kwenda Sanzibar hata aliyeko Zanzibar pia hatoki ila kwa utaratibu huo huo na hata nyumbani kwako unapoenda chumba cha watoto shart ujitambulishe japo kwa hodi na sauti huingii tu kwa kywa ni nyumba yako na ni watoto wako !
Nitapanda jahazi bagamoyo.
 
Kitambulisho chako kitasaidia kurecord taarifa zako(jina kamili,makazi yako au unapofanya kazi)hii ni faida kwako na ndg endopo imetokea ajari mkuu.
Mimi kukaa foleni kusubiri kitambulisho kulinishinda.uwa siwezi kabisa.
 
Mkuu WATU WENGINE HAWAJUI NINI MAANA YA KUA NA KITAMBULISHO.AKIOMBWA ATI ANAJISIKIA KAMA KADHALILISHWA.KWELI NCHI HII KAZI IPO.
NDIO MAANA HATA MKUU AMESEMA ANAJUTA HATA KUWA RAIS WA NCHI.
Hajakatazwa kujiuzulu.
Mpumbavu pekee ndio ataamini maneno hayo.
 
Mimi kukaa foleni kusubiri kitambulisho kulinishinda.uwa siwezi kabisa.
Mkuu sasa unaishije bila kitambulisho?
Kuna mdogo wangu mmoja alikua mgumu kama wewe juu ya kuwa na kitambulisho,siku moja yakamfika,akanipigia nimsaidie some amount,nikamrushia £350 kwa w.union,baada ya nusu saa nikampa MTCN No na Password nikamwambia nenda kachukue,kufika w.union anaambiwa lete kitambukisho cha mpiga kura,passport au driving licence,hakuwa nacho kati ya hivyo,akanipigia nikamwambia sina namna ya kukusaidia na wala siwezi kuivuta irudi ili nikutumie kwa mtu mwingine,nikamwambia wewe tafuta jitambulisho miongoni mwa hivyo kisha nenda kachukue pesa yako.Kwa bahati nzuri miezi miwili baadae kukawa na maboresho ya daftali la wapiga kura,akaenda kuchukua kitambulisho kisha akaenda kuvuta mpunga wake,ingawa cha moto akishakiona!
 
Cheti cha kuzaliwa sii kitambulisho mkuu!!
Cheti cha kuzaliwa kinaweza kukutambulisha makazi yako?
Toa comment yenye kusaidia na usitoe yenye kupotosha.
Kwa mfano mimi nimezaliwa Mkoani Mveya na cheti changu kinaonesha hivyo,but naishi Dar na mimi asili yangu ni Mara,na Mbeya nilipozaliwa babangu alikua mtumishi serikalini,but 99% ya ndg zangu ni Musoma,jee ikitokea nimetumia cheti cha kuzaliwa na ajari imetokea nikafariki jee ntapelekwa Mbeya nilipozaliwa ili ndg zangu waje kunitambua?yani watokee Musoma?
Wewe unazungumzia nini au kitambulisho gani?
Mfano kitambulisho cha utaifa kinarekebishwa lini endapo kama nimehama mahali nilipojiandikishia? Vivyo hivyo kwa kile cha mpiga kura.
Je kitambulisho cha mtumishi kinaonesha makazi yake? Au hiki hakitakiwi!
 
Back
Top Bottom