Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,037
- 9,927
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa mwananchi kuwa na kutambulisho cha NIDA haina maana kwamba hicho ndicho kinachoonesha uhalali wa uraia wake kwani vitambulisho hivyo hata wananchi wasiowazawa wa Tanzania wanavyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene
Waziri Simbachawene ameitoa kauli hiyo Bungeni Dodoma hii leo Juni 4, 2021, ambapo ameongeza kuwa hata yeye licha ya kwamba anatokea Dodoma ikitokea kuna wasiwasi kidogo juu ya uraia wake lazima atahojiwa juu ya uhalali wa uraia wake.
"Kupewa kitambulisho cha uraia wa Tanzania (NIDA) siyo mwarobaini kwamba wewe hauwezi ukaulizwa kuhusu uhalali na uhalisia wa uraia wako, vitambulisho hivi hata wakazi wasio raia wanavyo, hata mimi ninaweza nikaulizwa uraia na uhalisia wangu endapo utajitokeza wasiwasi wowote," amesema Waziri Simbachawene.