Kitambi kigumu kama jiwe chaashiria nini?

Kitambi kigumu kama jiwe chaashiria nini?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,502
Reaction score
911,255
610x350


Truths, lies and antiretrovirals

Myth 4: ARVS give you a thin face and deform your body
Until recently, the most commonly used ARV regimen at government hospitals included an ARV known as d4T. If d4T is used for longer than a year, it can change a patient's body shape, causing fat loss in the arms, legs or face or depositing fat in the stomach, back of the neck or breasts (in men and women). In April 2010, d4T was replaced by a drug known as Tenofovir, which has none of these side effects.



Nchi hoehae kama zetu kitambi ni mali!
Kitambi huwadobosha walalahoi pekee!
Kitambi huthibitisha kuwa anazo "chenji"!
Kitambi huwatambia wasizonazo mlo anao!
Kitambi hakihusishwi na afya, walakini kamwe!
Kitambi kigumu kama jiwe chaashiria nini?

Wasizonazo hutamani sana umiliki wake!
Walalahoi hukisaka hata kile cha taputapu!
Walalanjaa hushindia pumba kukikirimu kitambi!
Wenzetu wa majuu, kitambi ni balaa kubwa!
Wang'ambo viashiria vya vijisenti siyo tumbo!
Kitambi kigumu kama jiwe chaashiria nini?

Wanyanyaapaji wake walonga hizo ni safura tupu!
Wenye navyo hujihami kuwa hizo ni porojo za mkosaji!
Vibosile wetu wengi hujivunia vitambi vyao bila zengwe!
Wanene hao kwenye hotuba zao hawaachi kuvipapasa!
Kila wakisimama balbu zao haziaachi kuvichungulia tuli!
Kitambi kigumu kama jiwe chaashiria nini?

Nimekutana na mama mtu mzima akilia na kitambi!
Kero yake ni kuwa tumbo lake halikuwa hivyo kabisa!
Sasa kukicha tumbo lake na hohoho vinakua kwa kasi!
Mgogoro na shari hii ilianza baada ya kumeza zile punje!
Tangia siku alipoanza kuzimeza zile punjepunje za "AVR"!
Kitambi kigumu kama jiwe chaashiria nini?

Mwanamama kabla ya hii balaa alikuwa bomba sana!
Taswira yake ya awali mzungu aliita mafiga manane!
Lakini siha yake sasa yashabihiana na umbo la "S" hivi!
Wapambe nuksi hawaishi kumkejeli kuwa ana uja wepesi!
Wanyanyapaaji wako wengi na wanamwongezea maumivu!
Kitambi kigumu kama jiwe chaashiria nini?



 
Kinaashiria utapia mulo

TIQO sijui nisemeje........maana hata hujasoma achilia mbali kuelewa ujumbe wenyewe.....................rudia kusoma polepole kabisa.......
 
Kinaashria kifo

Angel Msoffe mbona wewe unapokea tu "likes" na hujawahi kumprudishia yeyote..........acha uchoyo...."mwaya"....................kwenye hii mada hakuna ulazima wa kifo wapo wenye vitambi hivyo vya "AVR" hata miaka 20..........................ila vina mateso ayke siyo lazima kufa ila kutaseka sana........
 
Rutashubanyuma unacho kitambi hicho? Nimependa shairi lako.

Tata nikitoe wapi wakati bunduki yangu haina risasi itaua namna gani? On serious note Kaunga is waiting for this response with abated breath................asingekutupia "like" kama hujagusa hisia zake.I know she is a beauty & exotic 2, ....... though she may be.........................she is cunning too........
 
Nimesoma title mkuu, au title na content tofauti?

TIQO nimekupata lakini uhondo ni kwenye ufupisho wa khabari au khabari yenyewe? Do not judge a book by its cover.................read it and then judge for yourself............
 
Tata nikitoe wapi wakati bunduki yangu haina risasi itaua namna gani? On serious note Kaunga is waiting for this response with abated breath................asingekutupia "like" kama hujagusa hisia zake.I know she is a beauty & exotic 2, ....... though she may be.........................she is cunning too........

Nimempa 'like' coz amenisaidia kuuliza swali nililotaka kuuliza. LOL
ila somehow l knew you dont have it, kwani usingekisagia the way you did!

Haya back to the swali, nafikiri kitambi kinaashiria some level of ignorance kwenye societies ambazo zinakishabikia.

Kwenye red, unamaanisha??????
 
Back
Top Bottom