Kitakachotokea kesho bungeni

yaani nitakavyo lia kwa uchungu, kama wasipojadili ni mimi na nafsi yangu tu,
 
CC: kasenene

Nimesoma comment yako kwenye uzi fulani basi nikaona si vibaya nawe usome hii thread yangu.

Tuna safari ndefu sana watanzania.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hali ninavyoiona,nina mashaka makubwa kama ripoti ya CAG itajadiliwa bungeni siku ya kesho pamoja na ahadi ya mh.Spika.

Wadau hivi mmejiuliza ni kwanini mwenyekiti wa bunge amegoma kupokea muongozo wa mh.Lissu kwa kisingizio bunge halijapokea hukumu rasimi ya mahakama kuu?

Je, ni kwanini mwenyekiti wa bunge alishindwa kusisitiza kauli ya bosi wake kuwa bunge haliwezi kuingiliwa na lina kinga yake na badala yake akaishia kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu?

Labda niwaulize tu,kwani wakati Spika anatoa msimamo kuwa bunge halitazuiwa kufanya kazi yake kulikuwa na hukumu rasimi ya mahakama mezani kwa spika?

Alichofanya mwenyekiti wa bunge jioni hii ni ujanja ujanja tu kuepuka kuji-commit kwani bila shaka anajua kila kitu hivyo hakutaka kuja kunukuliwa siku ya kesho na akasingizia kuwa bunge halijapokea rasim hukumu hiyo ya mahakama.

Wadau,hii ni consipiracy tu na ni mkakati umepangwa kiufundi ili kuwahadaa wabunge.Alichofanya Spika ni kuwatia moyo wabunge tu pengine ili shughuli za leo zikamilike ila kesho ama atawageuka kwa kuwasomea hukumu rasimi ya mahakama au vile vile huenda kesho asikalie kiti na badala yake atamtuma mwenyekiti wa bunge huku akiwa na maelekezo maalumu ya kuzima mjadala.

Uwezekano mwingine ni kesho spika anaweza kuisoma hukumun hiyo mbele ya wabunge na kisha akaagiza kikao cha Kamati ya Uongozi kikae na kisha kitakuja na majibu ya kuahirisha mjadala huo kwa kisingizio cha ushauri wa kisheria na mambo ya aina hiyo.

Pia, Mwanasheria Mkuu wa serikali anaweza kutumika kwa kupewa nafasi ya kuongea bungeni hiyo kesho na kisha akaitumia nafasi hiyo kupotosha ukweli ili jambo hili lisijadiliwe na wabunge.

Naomba niseme tu kuwa sina imani hata kidogo na uongozi wa mihimili yote mitatu ya dola juu ya jambo hili na pia sina imani kabisa jambo hili litajadiliwa katika bunge hili.

Hata hivyo,mama Makinda leo una nafasi ya kipekee ya kuandika historia ambayo inaweza ikafuta makosa yako yote ya nyuma endapo tu,utasimama imara na kuruhusu huu mjadala kuendelea.

Narudia,spika Makinda hii ni "golden chance" kwako kuandika historia na utakumbukwa sana na watanzania licha ya makosa uliyoyafanya siku za nyuma.

Huu ni mtazamo wangu tu, nawe unaweza kuwa na maoni tofauti.

Akili ya kuambiwa,changanya na ya kwako.

wewe jamaa kama umeota vile,wamefanya kama ulivyosema.
 
Back
Top Bottom