Kitakachotokea kesho bungeni

Kwa hali ninavyoiona,nina mashaka makubwa kama ripoti ya CAG itajadiliwa bungeni siku ya kesho pamoja na ahadi ya mh.Spika.

Wadau hivi mmejiuliza ni kwanini mwenyekiti wa bunge amegoma kupokea muongozo wa mh.Lissu kwa kisingizio bunge halijapokea hukumu rasimi ya mahakama kuu?

Je, ni kwanini mwenyekiti wa bunge alishindwa kusisitiza kauli ya bosi wake kuwa bunge haliwezi kuingiliwa na lina kinga yake na badala yake akaishia kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu?

Labda niwaulize tu,kwani wakati Spika anatoa msimamo kuwa bunge halitazuiwa kufanya kazi yake kulikuwa na hukumu rasimi ya mahakama mezani kwa spika?

Alichofanya mwenyekiti wa bunge jioni hii ni ujanja ujanja tu kuepuka kuji-commit kwani bila shaka anajua kila kitu hivyo hakutaka kuja kunukuliwa siku ya kesho na akasingizia kuwa bunge halijapokea rasim hukumu hiyo ya mahakama.

Wadau,hii ni consipiracy tu na ni mkakati umepangwa kiufundi ili kuwahadaa wabunge.Alichofanya Spika ni kuwatia moyo wabunge tu pengine ili shughuli za leo zikamilike ila kesho ama atawageuka kwa kuwasomea hukumu rasimi ya mahakama au vile vile huenda kesho asikalie kiti na badala yake atamtuma mwenyekiti wa bunge huku akiwa na maelekezo maalumu ya kuzima mjadala.

Uwezekano mwingine ni kesho spika anaweza kuisoma hukumun hiyo mbele ya wabunge na kisha akaagiza kikao cha Kamati ya Uongozi kikae na kisha kitakuja na majibu ya kuahirisha mjadala huo kwa kisingizio cha ushauri wa kisheria na mambo ya aina hiyo.

Pia, Mwanasheria Mkuu wa serikali anaweza kutumika kwa kupewa nafasi ya kuongea bungeni hiyo kesho na kisha akaitumia nafasi hiyo kupotosha ukweli ili jambo hili lisijadiliwe na wabunge.

Naomba niseme tu kuwa sina imani hata kidogo na uongozi wa mihimili yote mitatu ya dola juu ya jambo hili na pia sina imani kabisa jambo hili litajadiliwa katika bunge hili.

Huu ni mtazamo wangu tu, nawe unaweza kuwa na maoni tofauti.

Akili ya kuambiwa,changanya na ya kwako.

Hapana mkuu asubuhi hakukua na habari ya Mahakama, miongozo yote ililenga juu ya halihalisi ya pale Dodoma wbunge kupenyezewa makabrasha ya report na kuhusu mtu aliyeshikwa na polisi lakini ndio makinda alikataa wabunge kujadili hilo. Lakini kuhusu kujadili report ya kamati alisema ipo pale pale na aliagiza kurudufiwa kwa copy za ile report ili kesho iwezwe kusomwa nadhan ccm kweli walikuwa na jitihada za kila namna kuzuia lakini ukweli ni kwamba walichelewa kidogo kuzuia na siku zikawa zimefika sasa wamekuwa hawana jinsi mana ile mianya yooote waliyotaka kupita kuzuia ilikuwa inagundulika kabla bungeni wanaisema sasa wamekuwa hawana mpenyo. me nadhan kesho watatafuta namna kuifanya hiyo report isiwe na uhalali katika kujadili alradi kuwe na mazonge mazonge kuwe msitosito fulani ivi.
 
kwa hali ninavyoiona,nina mashaka makubwa kama ripoti ya cag itajadiliwa bungeni siku ya kesho pamoja na ahadi ya mh.spika.

Wadau hivi mmejiuliza ni kwanini mwenyekiti wa bunge amegoma kupokea muongozo wa mh.lissu kwa kisingizio bunge halijapokea hukumu rasimi ya mahakama kuu?

Je, ni kwanini mwenyekiti wa bunge alishindwa kusisitiza kauli ya bosi wake kuwa bunge haliwezi kuingiliwa na lina kinga yake na badala yake akaishia kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu?

Labda niwaulize tu,kwani wakati spika anatoa msimamo kuwa bunge halitazuiwa kufanya kazi yake kulikuwa na hukumu rasimi ya mahakama mezani kwa spika?

Alichofanya mwenyekiti wa bunge jioni hii ni ujanja ujanja tu kuepuka kuji-commit kwani bila shaka anajua kila kitu hivyo hakutaka kuja kunukuliwa siku ya kesho na akasingizia kuwa bunge halijapokea rasim hukumu hiyo ya mahakama.

Wadau,hii ni consipiracy tu na ni mkakati umepangwa kiufundi ili kuwahadaa wabunge.alichofanya spika ni kuwatia moyo wabunge tu pengine ili shughuli za leo zikamilike ila kesho ama atawageuka kwa kuwasomea hukumu rasimi ya mahakama au vile vile huenda kesho asikalie kiti na badala yake atamtuma mwenyekiti wa bunge huku akiwa na maelekezo maalumu ya kuzima mjadala.

Uwezekano mwingine ni kesho spika anaweza kuisoma hukumun hiyo mbele ya wabunge na kisha akaagiza kikao cha kamati ya uongozi kikae na kisha kitakuja na majibu ya kuahirisha mjadala huo kwa kisingizio cha ushauri wa kisheria na mambo ya aina hiyo.

Pia, mwanasheria mkuu wa serikali anaweza kutumika kwa kupewa nafasi ya kuongea bungeni hiyo kesho na kisha akaitumia nafasi hiyo kupotosha ukweli ili jambo hili lisijadiliwe na wabunge.

Naomba niseme tu kuwa sina imani hata kidogo na uongozi wa mihimili yote mitatu ya dola juu ya jambo hili na pia sina imani kabisa jambo hili litajadiliwa katika bunge hili.

Huu ni mtazamo wangu tu, nawe unaweza kuwa na maoni tofauti.

Akili ya kuambiwa,changanya na ya kwako.

mkuu kwa mawazo uliyowasilisha hapa ni thahiri kabisa yote yanaweza kutokea.je ninataka kujua je kunauwezekano wa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na kiti cha spika hiyo kesho?
 
Upinzani hawajui tu kuna wakati mkidundana na kutwangana heshima inakuwepo angalia nchi zilizopigana watu wanavyo heshimiana huu uhuru tulioupata kama pipi sometimes umetuharibu ustahimilivu wetu si wa binadamu wa kawaida ni kama kuna kitu tumelishwa vile. Wao wanakinga ya kutoshtakiwa wakisema au kufanya chochote bungeni

Mkuu, hapo umenena sana. Kesho Sugu, Lema, Filikunjoombe, Nassari, Lissu, Machali, Kafulila na wengine wengi waliopo mjengoni....wawape kibano hao maccm na mafisadi wa escrow mpk wasome hiyo report.

Hapo wataheshimiana..
 
Bunge halina ujanja zaidi ya kutii mahakama kwa swala hili. Kuna sababu kuu moja naiona mimi ambayo inafanya hoja ya bunge kutokuwa na jinsi zaidi ya kuitii mahakama. Sababu kubwa ni tofauti ya strategies kati ya bunge na mahakama katika suala hili. Mahakama naona katika hili imetumia sheria wakati bunge linaonekana kutumia siasakatika kudai power yake. Ntafafanua, Bunge lilijua kuwa kuna uwezekano wa mahakama kuweka zuio lakini bunge halikujiandaa kwa hoja za kisheria katika jambo hili.

Tatizo la bunge letu ni kuwekeza sana kwenye kusema kwa ukali bila kujali sana matokeo. Ningetemea wanasheria wa bunge tangu walipopata tetes za zuio wange andaa legal team na hoja na mipango ya kuwaongoza kupita hapa walikokwama. Lakini wao walipambana na miongozo. Sasa mahakama ikatae kupokea malalamiko ya mtu? si ndio kazi yake? Ishu hapa si mahakama kulibana bunge ila ni mahakama kufanya kazi ilizoletewa na mlalamikaji.Sasa ina maana mahakama ilitakiwa ispokee kesi? IS IT REAL?? Can any law maker argue for this?

Nadhani haki inatafutwa mahakamani sio bungeni. Kama mahakama imepokea kesi tatizo liko wapi? Na KAMA MAHAKAMA HAINA UWEZO HUO KISHERIA SI WANASHERIA WA BUNGE WAENDE MAHAKAMANI WAONYESHE HIYO OVERSIGHT YA MAHAKAMA? Bora huko mahakamani maana maamuzi yake yanaweza kutekelezwa kuliko maneno makali ya wa bunge yanayo burudisha nafsi lakini matokeo ni kuunga mkono hoja.
 
Hivi tunataka kuona nini hiyo kesho au masaa machache yaliyobaki?
Wahusika tunaotarajia kuwasikia wengine majina yao yanajulikana na hawajachukia hatua zozote mpaka mda huu. Kwa mtuhumiwa ambaye dhamira yake iko hai, angeshafanya maamuzi siku nyingi. Hata yule mama Tibaijuka ambaye amejitaja mwenyewe asingetakiwa kusubiri mpaka mda huu.
Tutegemee lugha za kukashifiana na kutukanana humo alafu wawili au watatu wanakuwa kondoo wa sadaka na game inaisha. Msitarajie mambo makubwa yatakayokuwa na tija kwa taifa maana dhamira za hawa wenzetu zimesha kuwa SUGU
 
Mkuu, hapo umenena sana. Kesho Sugu, Lema, Filikunjoombe, Nassari, Lissu, Machali, Kafulila na wengine wengi waliopo mjengoni....wawape kibano hao maccm na mafisadi wa escrow mpk wasome hiyo report.

Hapo wataheshimiana..

uliona wapi ngedere anampinga nyani .
 
Bunge halina ujanja zaidi ya kutii mahakama kwa swala hili. Kuna sababu kuu moja naiona mimi ambayo inafanya hoja ya bunge kutokuwa na jinsi zaidi ya kuitii mahakama. Sababu kubwa ni tofauti ya strategies kati ya bunge na mahakama katika suala hili. Mahakama naona katika hili imetumia sheria wakati bunge linaonekana kutumia siasakatika kudai power yake. Ntafafanua, Bunge lilijua kuwa kuna uwezekano wa mahakama kuweka zuio lakini bunge halikujiandaa kwa hoja za kisheria katika jambo hili.

Tatizo la bunge letu ni kuwekeza sana kwenye kusema kwa ukali bila kujali sana matokeo. Ningetemea wanasheria wa bunge tangu walipopata tetes za zuio wange andaa legal team na hoja na mipango ya kuwaongoza kupita hapa walikokwama. Lakini wao walipambana na miongozo. Sasa mahakama ikatae kupokea malalamiko ya mtu? si ndio kazi yake? Ishu hapa si mahakama kulibana bunge ila ni mahakama kufanya kazi ilizoletewa na mlalamikaji.Sasa ina maana mahakama ilitakiwa ispokee kesi? IS IT REAL?? Can any law maker argue for this?

Nadhani haki inatafutwa mahakamani sio bungeni. Kama mahakama imepokea kesi tatizo liko wapi? Na KAMA MAHAKAMA HAINA UWEZO HUO KISHERIA SI WANASHERIA WA BUNGE WAENDE MAHAKAMANI WAONYESHE HIYO OVERSIGHT YA MAHAKAMA? Bora huko mahakamani maana maamuzi yake yanaweza kutekelezwa kuliko maneno makali ya wa bunge yanayo burudisha nafsi lakini matokeo ni kuunga mkono hoja.
Mkuu, ulichoongea ni kweli ingawa inasikitisha.

Kamati ya Uongozi pamoja na wanasheria wa bunge watamshauri spika asitishe mjadala huo.

Najua bunge litalipuka lakini mwenye maamuzi ni spika hivyo ataliahirisha bunge huku kukiwa na zogo kubwa la spika kuzomewa.
 
Kabisa mkuu, watu wanapenda saana nafuu ya muda mfupi kupitia maneno matamu ya hasira za wabunge lakini si kila tatizo linamalizwa kwa mijadala tu. Ishu hii bunge lingejipanga kupambana kisheria haswa na huko ndo lingeenda kufumua ishu nzima. Lingekubali kwenda mahakamani na kuonyesha udhaifu wote wa kisheria katika ishu hii na hapo ndo bunge lingewashughulikia wezi na mawakala wao. Uzuri wa mahakamani adhabu inaendana na kushindwa ila ushindi wa mijadala ya bunge inampandisha mtu hadhi ya kisiasa lakini suluhisho ni dogo au hakuna.
 
What? Mtu kasema hana imani na serikali. Kwa nini ahame? Kwani nchi hii Mungu amewapa watu wa serikali tu. Ni arrogance ya namna hii ndiyo inayotupeleka pabaya. The government should answer to the people. Kama haiwatendei haki wananchi kama ilivyo dhahiri kabisa, basi tukae kimya au tuhame nchi. Have you taken leave of your sense?
Umeusemea Moyo wangu!
 
Katibu ajapokea amegoma..

Kikao cha kamati ya uongozi kimeitishwa asubuhi hii kama nilivyosema.

Kama spika anajiamini,hicho kikao ni cha nini kama sio kupitia hiyo hukumu na kisha waje na maamuzi tofauti?

Subiri tu yatimie niliyoyasema.
 
Kwa Kumuona Huyo Zungu Hapo ... Kwa hakika Ni Ishara rasmi Taifa linaingia kwenye Kiza Kizito ... huko aliko Makinda na Kama Ya Uongozi HAKITAKUA CHEMA MBELE YA MTANZANIA
 
Kikao cha kamati ya uongozi kimeitishwa asubuhi hii kama nilivyosema.

Kama spika anajiamini,hicho kikao ni cha nini kama sio kupitia hiyo hukumu na kisha waje na maamuzi tofauti?

Subiri tu yatimie niliyoyasema.

Huu ni mtizamo mmoja ... alternative. ?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom